Chini ya kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", Udhamini waNasser kwa Uongozi wa kimataifa wazindua fomu ya kushiriki kwa kundi la pili

Chini ya kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", Udhamini waNasser kwa Uongozi wa kimataifa wazindua fomu ya kushiriki kwa kundi la pili

Chini ya ulinzi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dokta. Ashraf Sobhy, inazindua kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa chini ya kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini , ”Kwa kushirikiana na Chuo kitaifa cha Mafunzo , Wizara ya Mambo ya nje ya Misri na Shirika kadhaa za kitaifa.

Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kuzindua fomu ya kusajili kwa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa, unaolenga viongozi vijana wenye taalum mbalimbali za kiutendaji na vijana washawishi katika Jamii za kiraia katika mabara matatu ya Afrika, Asia na Marekani ya Kusini.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unakuja kama moja ya misingi ya kutekeleza Mtazamo wa Misri 2030 , Ajenda ya Afrika 2063 na kwa kufuata kanuni kumi za Shirika la Umoja wa Afro-Asia, Hati ya Vijana wa Afrika, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, vile vile kama Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pamoja na ramani ya barabara ya Umoja wa Afrika kuhusu kuwekeza ndani ya vijana. Kwa mfano mmoja tu, udhamini huo unatoa nafasi sawa kwa jinsia mbili zote.

Pia, lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 laashiria uwezeshaji wa vijana, na ushirikiano katika nyanja tofauti, sio barani tu, bali Duniani, kama yaliyomo ndani ya lengo la kumi na saba la malengo ya maendeleo endelevu. .

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya Misri baada ya Urais wake wa Umoja wa Afrika mnamo 2019, ikitekeleza mchango wake wa kukuza jukumu la vijana waafrika kupitia kutoa misaada ya kila aina, ukarabati na kutoa mafunzo, Mbali na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kupata faida kutoka kwa uwezo na maoni yao, na hiyo ndiyo iliyoidhinishwa na kutangazwa na Rais El-Sisi wakati wa shughuli za Mkutano wa Vijana Duniani katika toleo lake la pili la 2018 na toleo la tatu la 2019, wakati ambapo aliita kwa utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika 2021 kuwaandaa vijana milioni moja kwa uongozi.

Ikumbukwe kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi umetekelezwa mnamo Juni 2019 chini ya uangalizi wa Waziri Mkuu wa Misri Dokta. Mustafa Madbouly, na miongoni mwa tija zake muhimu zaidi ilikuwa "Harakati ya Vijana wa Nasser", ambayo iko katika nchi nyingi za Afrika, zikitumia kanuni zilizoidhinishwa na baba waanzilishi wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika na kuomba Umoja na mshikamano kati ya watu wa Kiafrika na watu wenye urafiki waliounga mkono bara la Afrika, kama watu wa Asia na Marekani Kusini.

Kiungo cha Fomu:

https://www.emys.gov.eg/youth/Nasser_Leadership_Fellowship