Jawaharlal Nehru " Mwanzilishi wa Hindi ya kisasa"
"Mara Nyingi Mafanikio Huja kwa Wale Wanaofanya Kazi na Ujasiri, Lakini ni nadra kwa Wale Waasi Wanaogopa Misimamo na Matokeo yao".
Jawaharlal Nehru amezaliwa 1889 mjini mwa Allahabad katika familia ya wastani, Baba yake alikuwa Mwanasheria kutoka tabaka la Barahma ambapo alisoma katika shule ya Harrow, ni shule kwa wavulana tu huko mji wa Harrow kwenye Capitol Hill, kisha akasoma sheria katika Vyuo Vikuu vya Uingereza haswa katika Kitivo cha Trinity katika Chuo Kikuu cha Cambridge.
Alirudi tena nchi yake baada ya kumaliza masomo yake na kuzunguka nchi za Ulaya, lililoongeza upana wa macho yake, ili kujiunga kwa kikundi cha kitaifa pamoja na kiongozi wake wakati huo Mahatma Gandhi alimzingatia kama msaidizi wake wa kwanza, Hiyo ndiyo ilimingiza Gerezani mara kadha.
Alijiunga na mahakama kuu ya Allahabad na akaonesha kupendezwa na Siasa ya kitaifa iliyochukua nafasi ya kutekeleza taaluma yake ya sheria, alikuwa mtu mzalendo aliyejitolea tangu ujana wake, akapata umaarufu mkubwa katika siasa za India wakati maandamano ya 1910.
Akawa kiongozi maarufu wa vikundi vya mrengo wa kushoto katika Mkutano wa kitaifa wa India wakati wa kipindi cha 1920 Mkuu wa Seneti ( Bunge la wazee ) na kubali kamili kutoka mshauri wake Mahatma Gandhi, alipoteuliwa Mkuu wa Seneti 1929 akataka uhuru kamili kutoka utawala wa Kiingereza na akahimiza kuhamisha kwa seneti upande wa kushoto.
Nehru na Baraza la Wazee wakatawala siasa za Kiindia wakati wa kipindi cha 1930 wakati wa kuelekea nchi hiyo kwa uhuru, wazo lake la kuwa nchi ya kitaifa lisilo la kidini lililoshindwa kwa udhahiri baada ya seneti kushinda kikubwa uchaguzi wa mikoa ya Kiindia mwaka wa 1937 na kuunda serikali katika mikoa kadha.
Hakukubali kushiriki India katika Vita vya pili vya Duniai na akawahimiza wafungwa jambo hilo basi akakamatwa na kuwekwa Gerezani miaka mitatu, na Uingereza baada ya kumaliza Vita hivyo ililazimishwa kutambua Uhuru wa India.
Seneta mwenzake wa zamani akawa mpinzani akidai Muungano wa waislamu, na Muhammad Ali Jinnah akaanzisha udhibiti wake kwa siasa za Kiislamu nchini India, Majadiliano ya kugawanya kati ya seneti na Muungano wa waislamu yalishindwa, iliyosababisha ugawanyaji wa India wa kidamu na uhuru wake 1947.
Seneti ilimchagua Nehru kuchukua madaraka kama Waziri Mkuu wa kwanza wa India huru, kupitia kipindi cha urais wake, Nehru aliazimia kufikisha maoni yake kwa India, alitoa katiba ya India 1950, baada ya hapo alianza mipango ya mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa , Alisimamia mabadiliko ya India kutoka koloni hadi Jamuhuri, huku akikumbatia vikundi na mfumo wa vyama vingi, ama kuhusu siasa ya nje, alichukua nafasi ya uongozi katika Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, akiangaza India kama eneo kubwa katika Asia Kusini.
Siasa yake ilitegemea na kanuni ya ujamaa na akaitaka nchi isiyohusiana na Dini, kufikia usawa kati ya matabaka mbalimbali yaliyojenga jamii ya Kiindia, alikuwa kutoka watetezi maarufu kutoka maadili ya Usawa na Amani Duniani, akajulikana na jukumu lake la muhimu na Jamal Abdel Nasser na Tito katika kuongeza harakati iliyoitwa na nchi zisizifungamana na upande wowote, katika wasaidie watu na nguvu iliyoachie huru Duniani dhidi ya dhuluma na ukoloni tangu mkutano wa Bundung 1955 ambayo iliyokuwa kama nguzo ya kwanza kwa harakati hiyo. Harakati hiyo kwa hakika iliyothibitisha uwepo wake na heshima yake na ikafanikia kikubwa katika kujitenga nguvu ya ukoloni na kufichua mipango yao.
Nehru alikuwa mwandishi mahiri katika Kiingereza na aliandika idadi ya vitabu, kama vile Ugunduzi wa India , Dondoo za Historia ya Dunia , Wasifu wake na kitabu cha Kuelekea Uhuru (1936 ).
Mnamo1955, Jawaharlal Nehru alipewa Bharat Ratna, heshima ya juu zaidi ya kiraia katika Jamhuri ya India, Rais Rajendra Prasad alimtunuku cheo hicho cha heshima, bila kuchukua ushauri wa Waziri Mkuu kama utaratibu wa kawaida wa kikatiba.
Alikuwa na mara nne za kujaribu za kumuua
na watu wasiojulikana. Jaribio la kwanza lilifanywa wakati wa Mgawanyiko wa Uhindi1947 wakati wa ziara yake katika Jimbo la Frontier Kaskazini Magharibi ndani ya gari. La pili lilikuwa wakati alipomdungwa na Dereva kwa mnamo 1955. La tatu lilikuwa Bombay (Maharashtra ya sasa) mnamo 1956. La nne lilikuwa jaribio bure la kulipua bomu kwenye njia ya treni ya Maharashtra mnamo 1961.
Licha ya vitisho kwa maisha yake, Nehru alilalamika kupata ulinzi mkubwa karibu naye.
Afya ya Nehru ilianza kuzorotesha polepole baada ya 1962, na akaendelea miezi kadhaa kupata nafuu huko Kashmir mnamo 1963, akaaga Dunia Mei 27, 1964, akiwa na umri wa miaka 74.