Al_Fustat.....Mji Mkuu wa Kwanza na Kongwe zaidi wa Kiislamu

Al_Fustat.....Mji Mkuu wa Kwanza na Kongwe  zaidi wa Kiislamu

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky

Miali mbili takriban kutoka Kairo, kwenye pwani ya Nile katika upande wake wa Kaskazini_Mashariki, haswa karibu na Ngome Babylon, kuna mji mkuu wa kwanza na kongwe zaidi wa kiislamu, ambao ni "Al-Fustat". Waarabu  Waislamu walipofika Misri kwa uongozi wa Amr Bin Al_Aas, walikuta Miji miwili mikubwa ndani yake ambayo ni  Alexandria, kwenye pwani ya Bahari ya Mediterania, unazingatiwa mji mkuu wa kwanza, kwa sababu ukaribu wake na Milki ya Roma ya Mashariki, yenye utawala wakati huo, wa pili ni Bablyon, ambayo iko katika kichwa cha Delta  ili kuangaza Bahrain, Al-Bahri na Al-Qibli, na pwani ya Nile, ambayo hurahisisha mawasiliano yake na maeneo yote ya Misri, vilevile iko katikati ya Nile upande wa magharibi_ambayo ni rasilimali ya maji isiyokwisha_ na kati ya Mlima wa Mokattam, ambao ni kikomo cha asili cha kuulinda.


Baada ya kushikwa kwa Amr Ibn Al_Aas ndiye ni mshini mwislamu wa kiarabu, kwa ngome ya Babylon _kama wanahistoria waarabu wa kwanza wanavyoiita _ aliacha kundi la ulezi ndani yake na kuelekea kwenye Alexandria, Mji Mkuu wa nchi, na kutekwa baada ya kuizingira kwa muda wa miezi sita, baadaye Amr alilazimika kuchukua mji mkuu ili kukaa pamoja na askari wake waliomyeka, mwanzoni, mshindi mkuu hakutaka kujisumbua na ujenzi, kwa hiyo alichagua Alexandria alipozikuta nyumba zake tayari, nakasema, “Tumezifunika kwa nyumba.” Lakini Khalifa Umar ibn al-Khattab alikataa kuchukua mji wa Alexandria kama mji mkuu wa nchi - ambayo ilikuwa mji mkuu wa Misri wakati wa awamu ya Ptolemies na Warumi. Amr Ibn Al_Aas alichagua eneo lisilo na ujenzi na usanifu, isipokuwa  kwa ngome ya Kirumi, kuanzisha mji mkuu mpya, na kuuita "Al-Fustat", kuwa msingi wa nchi na nyumba ya emirate, mnamo mwaka wa Hijri  21, na miladi  641.

Ujenzi wake ulianza kujenga Msikiti wa Amr Ibn Al_Aas, ulioitwa baadaye " Msikiti wa Kale". Makabila ya Waarabu waliounda jeshi lake walijipanga kuzunguka msikiti, hivyo kila kabila kilipewa " Mpango" likishuka nayo, idadi ya watu katika kambi hiyo ilifikia 15,500 kwa ujumla, ambayo ni idadi ya askari walioshiriki katika ushindi huo. Na Upanuzi wa miji uliendelea katika jiji hilo hata vichochoro na njia zilikuwa nyingi. Neno Fustat inamaanisha Kambi, huitwa kwa jina hilo, kwani Amr wakati alieleke kufungua Alexandria alipenda njiwa ambaye alitaga juu ya hema lake, aliweka hema kwa ajili yake hadi aliporuda. Ili kujenga mji mkuu wa kwanza wa Misri ya kiislamu.

Wanahistoria hawakubaliani kuhusu ni nani aliyepanga mji wa Fustat, Al-Baladhuri alisema katika ushindi wa nchi kuwa yeye ni Al-Zubayr bin Al-Awam, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na akamjengea nyumba katikati yake, ambamo alitengeneza ngazi yake aliyopanda kuifungua ngome ya Bablyon, Ilisemekana kwamba ilichukuliwa hata na baraza la ushauri lililoundwa na Amr bin al-Aas, pamoja na wanachama wa Muawiya Bin Khadij Al-Tajibi, Shrek Bin Samar Al-Ghaifi, Amr Bin Qazam Al-Khawlani, na Jibril Bin Nashira Al-Ma'afari, kwa mujibu wa kile mwanahistoria Ibn Duqmaq alichosimulia katika kitabu chake “Ushindi kwa Wasita Aqd Al-Amsar.” 

Al-Maqrizi pia katika mipango yake alieleza hali ya ardhi ya Fustat kabla ya kujengwa kwa mji huo, na akasema: “Jueni kwamba eneo la Fustat, ambalo leo linaitwa mji wa Misri, lilikuwa ni uwanja na mashamba kati ya Nile na mlima wa mashariki, unaojulikana kama Mlima Mokattam,
hakuna kitu ndani yake katika suala la ujenzi na uendeshaji isipokuwa kwa ngome, ambayo baadhi yake inajulikana leo kama Ikulu ya Mshumaa na Al-Muallaqa. 

Jengo la Al-Fustat liliongezeka, na upanuzi wake  unafikia kwenye ukingo wa Mto Nile ukafikia maili tatu, na liliwakilisha jengo la Baghdad, mji mkuu wa dunia wakati huo, kama ilivyotajwa na mwanajiografia Ibn Hawqal katika “Picha ya Ardhi”. Iliundwa kutoka kwa mipango 12 au vitongoji, vitongoji hivi viligawanywa kuwa makazi ya makabila ya Waarabu kati ya Nile upande wa magharibi hadi Ain al-Sira upande wa mashariki, na kutoka Mlima Yashkar kutoka kaskazini hadi mashariki, na Mlima wa Al -Rasd unaojulikana kama Stabil Antar  , na mipango hii ni :Mstari wa watu wa bendera, Mstari wa Mahra, Mstari wa Tajib, Mstari wa Lakhm, Mstari wa Lafif, Mstari wa watu wa al-Zahir, Mstari wa Waalan, Mstari ya Waajemi , Mstari ya Khawlan, Mstari ya Maafir, Mstari ya Warumi na Wayahudi, Mstari ya Copts, na kwa kupita muda muundo wa Fustat uliunganishwa hadi kufikia kilele cha ukamilifu katika karne ya kumi,  na  karne nne Hijri, na ulibakia kuwepo kwa nguvu kwenye ramani ya kuanzisha miji hata wakati ambapo cheo cha mji mkuu kiliondolewa humo kwa ajili ya mji wa Al-Askar, uliojengwa mwaka 133 Hijri. Bani Abbas, na mji wa Al-Qatai, ambao ulijengwa na Ibn Tulun mwaka wa 256 Hijiri, au Kairo mwaka 358 Hijiri.

Al-Fustat ilijumuisha kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa ulinzi na nidhamu, pamoja na kuiwasha kwa taa tangu zama za Khalifa wa Fatimid Al-Aziz Billah na mwanawe Al-Hakim bi-Amr Allah, na karne tatu kabla ya hapo, Al- Fustat ilijumuisha vikosi vya zima moto; Ili kusaidia kupambana na moto, tangu zama za  Abdul Aziz bin Marwan Al-Umayyad (65-85 Hjria). 

Kuchimbwa kwa mfereji wa zamani uitwao Mfereji wa Trajan unaounganisha Mto Nile na Bahari Nyekundu pia ulisaidia kukuza harakati za biashara huko Fustat, lakini ushindi wa Kiislamu wa Misri ulipokuja, mfereji huo ulijazwa, hivyo Amr bin al-Aas akachimba tena, na iliitwa “Ghuba ya Amirul-Mu’minin,” ili meli zilizosheheni chakula na nafaka zipite hadi Hijazi,na kwa sababu ya eneo lake kwenye Mto Nile, baadaye ikawa kituo kikuu cha biashara ya baharini ya nje, na bandari ya biashara inayotoka "China, India, Yemen na Ulaya," pamoja na kuwa kituo kikuu cha usafiri wa maji, na Misri hii Ghuba iliendelea kutekeleza jukumu lake hadi 1897/1898,  Sehemu ya Ghuba ndani ya kairo ilijazwa na nafasi yake ikachukuliwa na Al-Khaleej Al-Masry Street, ambayo iliitwa barabara ya Port Said  mnamo 1957 . 

Bin Said al-Maghribi aliielezea bandari hii ya kibiashara iliyoshamiri katika safari yake ya Misri wakati wa zama za Ayyubid, akisema: “Ama kile kinachokuja Fustat kutoka kwenye hifadhi za bahari ya Alexandria (Mediterania) na bahari ya Hijaz (Nyekundu), kinazidi kile inafafanuliwa, na kuna mkusanyiko wa hayo, si katika Kairo, na kutoka humo yanatayarishwa hadi Kairo na kwingineko la nchi.”

Fustat ilibakia kuwa jiji lenye kushamiri hadi lilipokabili hatari ya  Msalaba, wakati mfalme wa Yerusalemu, Amalric, “Mwamori, mfalme wa ufalme wa Krusedi wa Yerusalemu, alipokuja kuivamia Misri,” na kusimama kwenye Fustat katika mwaka wa 565 Hijri.
Waziri wa Fatimiyyah, Shawar, Waziri wa khalifa, Al-Aaded Billah, aliogopa kuanguka kwa mji huo, hivyo akaamuru  uchomwe moto katika mji huo. 

 Maqrizi anaelezea  kuchomwa kwa mji huo, akisema: "Shawar alituma chupa  elfu 20 za mafuta na mienge elfu 10 ya moto, ambayo ilitawanyika,  moto na moshi wa moto ukapanda mbinguni, na ikawa ni mandhari ya kutisha, na moto ukaendelea kufika kwenye makao ya Misri muda wa siku hamsini na nne kamili.” Fustat ilibaki kuwa mji mkuu wa Misri kwa miaka 113.

Mji wa Fustat sasa hivi umegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya mashariki inayopakana na Mlima wa Mokattam, na hapa ndipo moto huo ulitokea na haujumuishi majengo mengine isipokuwa Msikiti wa Amr bin al-Aas na Kasri la Mishumaa, ambamo wanaakiolojia uchimbaji ulianza kuchimba magofu ya jiji lililoteketezwa, na sehemu ya magharibi karibu na Nile, ambayo leo inajulikana kama Misri al-Qadima.

Hivi sasa, eneo hili linajulikana kama "kitongoji cha Misr al-Qadima", na ni moja ya mtaa kongwe huko Greater Kairo, na maeneo mengi ya kiakiolojia hujumuisha mabaki ya Kale pamoja na Hekalu la Kiyahudi la Ben Ezra, makanisa ya zamani ya Misri,  Msikiti wa Amr Ibn al-Aas, uchimbaji wa magofu ya mji wa Fustat, Nilometer katika kisiwa cha al-Rawdah, na Kasri la Manasterly.Na kasri ya Muhammad Ali huko Manial. 

 Vyanzo 

Kitabu cha  "Kairo: Mipango Yake na Maendeleo ya Miji" cha mwanahistoria Dkt. Ayman Fouad. 

Tovuti ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri.