kumbukumbu ya uhuru wa Pwani ya Dhahabu ... Ghana

kumbukumbu ya uhuru wa Pwani ya Dhahabu ... Ghana
Ghana ilipata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa Uingereza mnamo Machi 6, 1957, baada ya Uvamizi uliodumu kwa zaidi ya miaka 60, na uhuru ukahakikishwa na kiongozi Kwame Nkrumah aliyekuwa akiamini kwamba uhuru wa Ghana uliunganishwa na uhuru wa Afrika, na alieleza katika hotuba yake Siku ya Uhuru, akisema: "Uhuru wetu haukuwa na maana isipokuwa imeunganishwa na ukombozi kamili wa bara la Afrika. "
Tarehe ya uhuru ya Ghana ilianza tena katika mkutano wa Umoja wa Pwani ya dhahabu mnamo 1947, uliokuja kutaka mapambano ya uhuru, na mkutano huo uliongozwa na Nkrumah, lililosababisha kukamatwa kwake mnamo 1948, na baada ya kuachiwa huru kizuizini, Nkrumah aliunda Chama cha mkutano cha watu (CPP) kwa ajili ya kufikia uhuru wa Ghana Mnamo 1950 Nkrumah alikamatwa tena, na chama chake kilishinda uchaguzi wakati alikuwa gerezani, na akaachiliwa, ili Nkrumah akawa waziri mkuu mnamo 1952.
Mnamo Machi 1957, uhuru wa Ghana ulitangazwa na katiba iliidhinishwa, na Kwame Nkrumah alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana.
Ghana iliitwa "Pwani ya Dhahabu" wakati wa Ukoloni, na ilipewa jina la Ghana baada ya uhuru wake.
Ma mahusiano kati ya Misri na Ghana yana sifa ya asili maalum, wakati ambapo nchi hizo mbili zinaunganishwa kwa mahusiano ya kihistoria yenye kina , ynayorejea enzi za kabla ya uhuru, na wakati harakati za ukombozi zilijitokeza barani Afrika, Misri ilisaidia Ghana kwa njia ya kuunga mkono na nguvu ya kupata uhuru wake, na Ghana inapokea umakini mkubwa kutoka kwa upande wa Misri, kulikuwepo urafiki mkubwa kati ya Rais Gamal Abd El Nasser na Rais Nkrumah, na kwa sababu Nkrumah alikuwa akihusishwa sana na Misri, alioa mwanamke Mmisri, "Fathia Nkrumah", na Rais Abd El Nasser alikuwepo kukamilika kwa ndoa hii. Na Bibi Fathia alikuwa mke mmisri wa kwanza wa kiongozi mwafrika baada ya uhuru wan chi za kiafrika , alipata Wana watatu, miongoni mwao ni Gamal, aliyeitwa kufuatia jina la rais Gamal Abd El Nasser.
Watu wa Ghana waliunganishwa zaidi na Misri baada ya kiongozi wao alioa na "Bibi wa Mto wa Nili", kama watu wa Ghana walivyomwita Bibi Fathia.
Misri ilikuwa moja wapo ya nchi za kwanza zilizoanzisha mahusiano mazuri ya kidiplomasia pamoja na Ghana.Misri pia inatoa msaada katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, na pia katika suala la usalama, afya, utalii, vyombo vya habari na mafunzo ya vijana.