Ishara ya Kihistoria ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Ishara ya Kihistoria ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

"Uwiano, Haki, Utaratibu, Hekima, Maarifa, Ukweli."... Ma'et ni ishara ya Udhamini wa Nasser 

Mmisri huyo wa kale alichukua kutoka kwa Ma'et kanuni za maisha yake, ambapo aliona ndani yake Utaratibu, Uwiano, Mwanzo, Mwisho, Lengo na Mwisho kabisa, aliisifu kama mwanamke mwenye mabawa mawili -  ndiyo siri ya Uwiano wake - na Usawa wa uthabiti wa kitu chochote na mpangilio wa ulimwengu, na Ma'et ni ishara ya Ukweli, Haki na Uadilifu, ambayo ni kauli mbiu ya mahakama katika Misri ya kale.

Sheria za Ma'et zilijumuisha maadili ya kibinadamu katika sura zake maalum, na zilionesha wazi ufahamu wa Wamisri wa kale wa ulimwengu, kama alivyoona ndani yake ishara ya ukweli, haki na utaratibu, hivyo kanuni za Ma'et zilikuwa mwongozo wa kuishi katika jamii na zilitiiwa na mfalme na watu.

Ma'et pia ilijumuisha mfumo wa ulimwengu ambao Mungu Ra alimkabidhi mfalme  kuanzisha katika utawala wa Dunia. 
Mfalme alipaswa kufanya hivyo, na kufanya ibada ya kuwasilisha "Ma'et", mfano wa yote hayo, na alihusishwa na sanamu "Chahoti", Mungu wa hekima na maarifa, na alijulikana kama mkewe, na alionekana pamoja naye katika eneo la uzito wa moyo wa marehemu, na pia alionekana kwenye mashua ya Bwana wa Jua "Ra". Ma'et alihusishwa na mfalme, aliyekuwa na jukumu mbele ya mabwana kwa kuanzisha utaratibu na haki, na kuanzisha Ma'et mahali pazuri palipoumbwa na mabwana kwa ajili ya ulimwengu. 

Moja ya mambo muhimu yaliyotufanya tuchague mrengo wa Ma'et kama kauli mbiu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni kuunganishwa kwa sheria za Ma'et na kanuni na nyaraka nyingi tunazoamini na kutegemea Udhamini na kutafuta taratibu za kuiamsha, ikiwa ni pamoja na, tena muhimu zaidi, kwa ujumla na ya kina zaidi ambayo ni kile kilichoelezwa katika sheria za Ma'et, kama inavyosema:  

1- Sikuwaibia wengine mali zao kwa ugomvi.

2. Sijafunga masikio yangu kutokana na kusikia maneno ya ukweli.

3- Sijamudhia mtu yeyote.

4- Sijaumiza hisia za wengine.

5- Sijabaka ardhi ya mtu yeyote.

6- Sijamtisha mtu yeyote.

7- Sijatishia Amani. 

8. Sijatoa mawazo/maneno/au vitendo vibaya.

9- Sijanyakua chakula na mdomo wa mtoto.

10- Sijaharibu majengo ya dini (mahekalu) 

Mungu wa (Ma'et) alibeba udhihirisho mkubwa zaidi wa mfano wa Kimungu wa dhana za kufikirika zilizogundua maana ya ukweli na Haki, iliyooneshwa na lugha ya Kale ya Misri kwa neno moja nalo ni (Ma'et) na Mungu anayebeba jina hili,  lililoonekana tangu nasaba ya pili picha katika umbo la kibinadamu la lililobeba kichwa chake (manyoya ya mbuni) na Mungu wa (Ma'et) kama tulivyosema ni binti wa Mungu wa jua (Ra), anayetawala kulingana na kanuni zilizowekwa vizuri za Haki na Ukweli zilizoamuliwa na sheria ya jumla, na kwa hivyo kila wakati tunaona Mungu huyo amesimama mbele ya boti ya Jua Takatifu iliyoambatana na Ra wakati wa safari yake angani, tuliichukua kama kauli mbiu ya toleo letu la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambayo kupitia uongozi wake wa vijana iliyoweka kutuma maadili ya amani na haki ya kijamii Duniani kote.