Kikao cha mazungumzo (Maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa)

Kikao cha mazungumzo (Maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa)
Kikao cha mazungumzo (Maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa)
Kikao cha mazungumzo (Maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa)
Kikao cha mazungumzo (Maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa)

Shughuli za siku ya sita ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" zilianza kwa kikao cha mazungumzo kiitwacho "Maamuzi ya Sera ya Kitaifa ya Nje kwa Kuzingatia Changamoto za Kikanda na Kimataifa", kwa mahudhurio ya Balozi Sherif Eissa, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa masuala ya Afrika, na Balozi Amal Abdel Qader Salama, Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Makundi na Mashirika ya Asia-Asia. Majadiliano hayo yaliongozwa na Dkt. Mahmoud Labib, mmoja wa washiriki wa Udhamini.

Balozi Sherif Issa alielezea furaha yake ili kukutana na Vijana wa Udhamini wa Nasser, akieleza kuwa Mahusiano ya Misri na Afrika ni ya zamani kama ilivyokuwa safari ya kwanza ya kibiashara Barani Afrika, na kuwa sasa Misri inaanzisha mahusiano makubwa pamoja na magharibi na kusini mwa Afrika kwa kuzingatia jukumu kubwa aliloifanya Rais Abd El Fatah El-Sisi alihakikisha idadi kubwa zaidi ya ziara Barani Afrika tangu mwanzo wa uongozi wake hadi sasa, kwa kuzingatia kutazamia kuhakikisha utulivu na maendeleo Barani Afrika.

Katika hotuba yake, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika alizungumzia jukumu na sifa za mwanadiplomasia aliyefanikiwa anayepaswa kuwa na ufahamu kamili wa masuala ya msingi ya nchi yake haswa yale yanayohusu usalama wa nchi yake wa kitaifa, kwa hiyo ni lazima awe kioo cha kweli na cha kujieleza cha jamii anayoiwakilisha na kuweka mbele ya macho yake mafanikio ya nchi yake, na anapaswa kuwakilisha jamii kwa dhati na kuchangia kueleza faida zake zenyewe na kuondoa hasi zozote zinazoweza kuwa akilini mwa mpokeaji na kurekebisha itikadi potofu, pamoja na uwezo wake wa kusimamia mahusiano nguvu na nia yake ya kuhamisha uzoefu wa nchi yake anayoiwakilisha katika nyanja mbalimbali ya kiutamaduni, kiuchumi, kibiashara, kijeshi na kiusalama, ambapo lengo la mwanadiplomasia huyo ni kuunda imani kati ya nchi hizo mbili, kubadilishana taarifa na kuchangia pendekezo la ushirikiano kati ya nchi yake na nchi anayoiwakilisha.

Kwa upande wake, Balozi Amal Abdel Qader Salama aliwakaribisha wajumbe wote wa vijana walioshiriki katika Udhamini huo kutoka mabara matatu, akisisitiza umuhimu wa Udhamini huo na kubadilishana mahusiano na ziara kati ya Vijana, akiongeza kuwa Mahusiano ya Misri na Asia ni mahusiano muhimu na ya kihistoria, kwani Misri ina Mahusiano ya kihistoria na baadhi ya ustaarabu katika bara la Asia la kale yanadumu kwa takriban maelfu ya miaka, na kwamba Mahusiano ya Misri na Asia ni ya zamani sana tangu marehemu Rais Gamal Abd El Nasser na kuanzishwa kwa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, mnamo miaka ya sitini ya karne iliyopita, iliyolenga kuimarisha Mahusiano na ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kuwa mahusiano ya Misri na Asia ni Mahusiano yanayozingatia urafiki na heshima kwa uhuru wa nchi na kufanya kazi ya kuimarisha Mahusiano katika nyanja mbalimbali.

Katika hotuba yake hiyo, Salama ameongeza kuwa Mahusiano ya Misri na Asia yameshuhudia ongezeko kubwa sana la mahusiano ya nchi hizo mbili, haswa tangu Rais Abd El Fatah El-Sisi ashike Madaraka ya Misri, ambako kumekuwa na ziara nyingi za kidiplomasia na kubadilishana ziara kwa kiwango cha urais au mawaziri na katika ngazi ya biashara pia. Na China ilizindua Mpango wa Ukanda na Barabara ili kufungua matarajio mapya ya ushirikiano, na kuna jitihada kubwa na kutia moyo kwa uwekezaji na kubadilishana biashara za Asia kati ya nchi hizo mbili, akiashiria umuhimu wa mwelekeo wa kiutamaduni na jukumu muhimu lililofanywa na Al-Azhar Al-Sharif huko Asia, kwani ni mwanga wa maarifa na hutoa mafundisho ya kidini kwa njia ya wastani na inatoa wito wa uvumilivu, na kuna nyanja nyingi za ushirikiano, haswa na India, Pakistani, Korea Kusini na Indonesia, na sera ya nje ya Misri kwa ujumla inategemea kuhakikisha Uwiano na nchi zote za Dunia.

Baada ya kumalizika kwa kikao cha mazungumzo ya matukio ya siku ya sita ya Udhamini huo, uliohusu maamuzi ya sera ya nje ya kitaifa kwa kuzingatia changamoto za kikanda na kimataifa, washiriki wa Udhamini huo walielekeza idadi ya maswali na maamuzi kwa Balozi Sherif Issa na Balozi Amal Abdel Qader Salama, walioshughulikia masuala yanayohusiana na masuala nyingi kama vile kuimarisha Mahusiano na Kameron, Tunisia na Pakistan, tatizo la Mto Nile, kutengwa kwa kiutamaduni ambayo Palestina inakabiliwa nayo, na mpango wa Rais Abd El Fatah El-Sisi wa kutibu raia milioni waafrika na masuala mengine yaliyotolewa wakati wa mkutano wa mazungumzo, kisha washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipiga picha za kumbukumbu katika hali ya kusisimua, kukaribisha sana na furaha ya wote ya kikao hicho cha kipekee.