Kanuni za mkutano wa Bandung

Kanuni za mkutano wa Bandung

Kanuni kumi za AAPSO

AAPSO ni Shirika la Mshikamano wa watu wa Afro_Asia, ambalo ni kifupi cha "Afro_ Asian people solidarity organization" uanzishi wake ulitangazwa mnamo Januari 1958, kama Shirika la kimataifa lisilo la serikali, linadokeza zaidi kanuni za ukombozi wa kitaifa na mshikamano wa watu wa nchi zinazoendelea, nalo ni Shirika moja lililoibuka  kutoka mkutano wa Bandung huko Indonesia, uliofanyika mnamo Aprili 1955, lililokuwa na mwitikio wa mwito wa wakuu wa serikali za India, Buruma, Pakistan, Ceylon na Indonesia katika uamuzi wa Bogor la Indonesia mnamo1954, ambapo ulijumuisha kuzialika nchi za Asia na Afrika; kuhimiza ushirikiano na maelewano kati ya raia wao, kujadili matatizo yake yanayotokana na ukoloni na ubaguzi wa rangi; kwa hivyo likawa na kamati za kitaifa katika zaidi ya nchi 90 huko Asia na Afrika, na lina  kamati za wajumbe huko Ulaya na Amerika ya Kusini.

Na mkutano huo ulikuwa moja ya uratibu na ushirikiano kati ya watu wa mabara huru ya Asia na Afrika, ambapo harakati za watu hao ilikuja katika mazingira ya kimataifa yenye magawanyiko na vuguvugu baada ya vita vya pili vya Dunia, matokeo makali ya vita yalisababisha kugawanya ulimwengu kwa pande mbili zinazokinzana kati ya mfumo wa kibepari uliongozwa kwa Marekani na mfumo wa ukomunisti kwa uongozi wa umoja wa Kisovieti, wakati watu wengi wa Asia na Afrika wakiteseka kutoka ukoloni uliobaka ardhi zao, kunyonya utajiri wao, kuzorotesha kiuchumi, umaskini na migogoro yaliopo kati yao.

Pia mkutano wa Bandug ni uzinduzi kwa kile kilichoitwa baadae kwa

 " Harakati ya Kutofungamana kwa Upande wowote, ambapo  sera za mwafaka chanya na kutofungamana kwa upande wowote ni mwelekeo ambayo viongozi kadhaa wa serikali walielekea kukubalika kueleza uhusiano na msimamo wa mzozo wa kimataifa, na katika kukabiliana sera ya ubaguzi.

Na mnamo mkutano waliamua kutekeleza kanuni kumi maarufu, nazo ni: 

1_ Kuheshima haki za kimsingi za binadamu, malengo na kanuni za Hati ya Umoja wa Mataifa.

2_ Kuheshima uongozi wa nchi zote na Amani ya ardhi zake.

3_ Kujiepusha kutoka uingiliaji wowote katika mambo ya ndani ya nchi nyingine.

4_ Kuheshima haki ya kila nchi katika kujitetea peke yake au pamoja na wengine; kwa mujibu wa Hati ya Umoja wa Mataifa.

5_ Kujiepusha kutoka kutumia mashirika ya ulinzi ya ujamaa; ili kuhudumia masilahi ya binafsi ya nchi kubwa yoyote.

6_ Kujiepusha vitendo, vitisho na matumizi ya nguvu dhidi ya Amani ya kikanda au uhuru wa kisiasa wa nchi yoyote.

7_ Kusuluhisha migogoro yote ya kimataifa kwa njia za Amani kama mazungumzo au upatanishi.

8_ Nchi yoyote inajizuia kufanya shinikizo dhidi kwa nchi nyingine.

9_ Kuendeleza masilahi na ushirikiano wa pamoja.

10_ Kuheshima uadilifu na wajibu wa kimataifa.

Ni vyema kutaja kuwa AAPSO linashikamana na linashirikiana na mashirika yote ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayothamini Uhuru na Amani; kwa ajili ya kupata ulimwengu usio na vita na Ghasia, na maendeleo mapya yoyote katika mabadiliko ya kisasa ni kama kanuni elekezi kwa shughuli za Shirika.