Taasisi ya kitaifa ya Uandishi wa Habari

Taasisi ya kitaifa ya Uandishi wa Habari

Mamlaka ya Kitaifa ya Uandishi wa Habari - Baraza Kuu la Uandishi wa Habari  hapo awali- ilianzishwa mwaka 2016 kama chombo huru kinachofurahia utu wa kisheria katika kutekeleza majukumu na taaluma zake, na hairuhusiwi kuingilia masuala yake, Makao makuu yake yako Mkoa wa Kairo, na hiyo ilitokea  ambapo Rais Abdel Fattah El-Sisi alipotoa maagizo ya Jamhuri 158,159, na 160 kwa uratibu wa Baraza kuu la Vyombo vya Habari, Taasisi ya kitaifa ya Uandishi wa Habari, na Taasisi ya kitaifa ya Vyombo vya habari, na hivyo kwa mujibu wa aya za Sheria Na.92 kwa mwaka wa 2016, inayosema kuunda Baraza, na Taasisi zilizotajwa hapo juu kuhusu Uratibu wa Taasisi za Uandishi wa Habari na Vyombo vya habari, pamoja na kushikilia Taasisi hiyo usimamizi wa Taasisi za Uandishi wa Habari zinazomilikiwa na Nchi.

Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari ina uhusiano na Taasisi kadhaa za kitaifa, zikiwemo: Taasisi ya Al-Ahram , Taasisi ya Akhbar Al-Youm, Dar Al-Hilal kwa Uandishi wa Habari na Uchapishaji, Shirika la Habari la Mashariki ya Kati, Kampuni ya Kitaifa ya Usambazaji, Dar Al-Tahrir kwa Uchapishaji na Usambazaji, Dar Rose al-Yusuf kwa Uandishi wa Habari na Uchapishaji, na Dar Al-Maarif kwa Uandishi wa Habari na Uchapishaji.