Mohammad Al-Feel.. Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Mohammad Al-Feel.. Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Imefasiriwa na / Aya Nabil


Ana shahada ya kwanza katika Uhandisi wa Anga, Chuo Kikuu cha Kairo.

• Aliishi nchini Uhispania na alifanya kazi pamoja na Mashirika ya kimataifa ya UN, Save the children na EU katika kuendeleza Programu za kielimu za  ubunifu katika nchi nyingi kama Uhindi, Nepal, Uhispania na Ujerumani kwa manufaa ya wakimbizi na walioathiriwa kwa majanga. 

• Alifanya kazi na Runinga ya Amerika ya Kusini Telesur na Uandishi wa Vyombo vya Habari vya Uhispania na Cuba kama mfasiri.

•Alifundisha Kihispania nchini Uhindi,Uhispania na Misri kwa kutumia Elimu ya Gamification.

Mwanzilishi wa Chuo cha Al-Tayer (Warsha) cha kufundisha Kihispania nchini Misri, na Kiarabu kwa wageni.

• Alishiriki katika kuandaa mipango ya kielimu kwa watoto nchini Misri, Uhindi na Uhispania.

• Alifanya kazi kama Mshauri wa Miradi na  UNHCR kwa kuunganisha watoto wakimbizi katika jamii ya Misri.