Mkakati wa Ushirikiano  kwa ajili ya  Kusini-Kusini 

Mkakati wa Ushirikiano  kwa ajili ya  Kusini-Kusini 

Ushirikiano wa Kusini-Kusini unamaanisha Ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi zinazokuwepo kusini mwa Dunia katika nyanja za kisiasa au kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kimazingira au kiufundi, pamoja na kubadilishana maarifa  , uzoefu, ujuzi, masuluhisho tofauti na teknolojia, kuunda  fursa za kazi, Miundombinu na kuimarisha  biashara Katika nchi za Kusini, na hiyo ni  mojawapo ya sura za  mshikamano kati ya  raia na nchi za Kusini, linalochangia  kutekeleza  ustawi wao wa  kitaifa , na kujitegemea kitaifa na kikundi  .Ushirikiano huo umechangia ongezeko la kiwango cha biashara, mtiririko zaidi  wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, na hatua  za kukwenda kwa  ushikamano  wa kikanda kati ya nchi za Kusini. inawezekana pia  Ushirikiano huo  uwe kati ya nchi mbili au  kikanda au baina ya kanda tofauti, na unaweza kujumuisha nchi mbili au zaidi kutoka kwa nchi zinazoendelea.

Pia kuna ushirikiano wa pande  tatu, na ushirikiano  huo ambapo nchi zilizoendelea na mashirika ya kimataifa hurahisisha   mipango kati ya nchi za Kusini, kwa kutoa Ufadhili, mafunzo,  idara  na mifumo ya teknolojia, pamoja na aina  nyingine za misaada . Ushirikiano wa pande tatu hujumuisha nchi mbili au zaidi kutoka nchi zinazoendelea kwa ushirikiano na upande wa tatu, kwa kawaida huwa ama nchi iliyoendelea au shirika la kimataifa, ambalo huchangia katika kubadilishana ujuzi na rasilimali zake.

Malengo makuu ya Ushirikiano kati ya nchi za Kusini yanafupishwa kama ifuatavyo

Kwanza: Kuhimiza nchi zinazoendelea kwa kujitegemea  kupitia kuimarisha uwezo wa kibunifu wao  wa kupata masuluhisho kwa matatizo yao ya kimaendeleo, kulingana na matarajio na mahitaji yao na uwezo pia.

Pili : kuhamasisha na kukuza kujitegemea wengi ndani ya nchi zinazoendelea kupitia kubadilishana Uzoefu, na kupata faida kutoka kwa Vyanzo vyake vya kiufundi kikamilifu, pia kuimarisha uwezo wake; uwe usaidizi mkuu.

Tatu: Kuimarisha uwezo wa nchi hizo zinazoendelea  wa  kuainisha  na kuchambua kwa pamoja masuala makubwa, kutilia mkazo kwa kuziendeleza na kuunda mikakati muhimu ya kuendesha, kuwezesha na kuunga mkono mahusiano yao  ya kiuchumi ya kimataifa .na hivyo inatekelezwa kupitia kukusanya maelezo yanayopatikana katika nchi hizo na taasisi husika zinazokuwepo ziangalie masomo ya pamoja kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kiuchumi wa kimataifa.

Nne: Kuongeza Ushirikiano wa kimataifa kwa upande wa Kiwango,kuuimarisha kwa upande wa Ubora, na kuboresha ufanisi wa Vyanzo husika kwa ajili ya  Ushirikiano wa kina wa kiufundi, na hivyo  kwa kuunganisha uwezo.

Tano: Kuimarisha uwezo wa kiteknolojia uliopo sasa  hivi katika nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na sekta ya kijadi, kuboresha ufanisi wa kutumia uwezo huo na kuunda  uwezo mpya, na  kutilia maanani  katika upande huo,   kwa kuhimiza uwasilishaji  wa teknolojia na ujuzi unaosambamba  na kile kilichopatikana katika nchi zinazoendelea kutoka  rasilimali na nguvu za kimaendeleo kwa namna inavyopeleka  kuimarisha uwezo wao wa kujitegemea binafsi na wa pamoja.

Sita: Kuongeza na kuboresha mawasiliano kati ya nchi zinazoendelea, linalosababisha kuunda maelewano zaidi kwa matatizo ya pamoja na kuongeza fursa za kupata maarifa na uzoefu unaopatikana, pamoja na kuunda ujuzi mpya kwa lile linalohusiana na  kutatua matatizo ya maendeleo.

Saba: Kuboresha uwezo wa nchi zinazoendelea  wa kupokea na kuwezesha teknolojia na uzoefu ili kukidhi mahitaji  maalum  ya maendeleo yao;

Kujua  matatizo na mahitaji ya nchi za maendeleo ya chini zaidi , nchi zisizo na Ufukwe, visiwa vinavyoendelea na nchi zilizoathirika zaidi.

Hatimaye, kuziwezesha nchi zinazoendelea kufikia kiwango kikubwa cha kushiriki katika shughuli za kimataifa za kiuchumi, na kupanua Ushirikiano kati ya nchi.