Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa yaongoza Tamasha la Nane la Uvumbuzi kwenye Durban, Huko Afrika Kusini

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa yaongoza Tamasha la Nane la Uvumbuzi kwenye Durban, Huko Afrika Kusini

Imefasiriwa na/ Sara Saed
Imeharirwa na/Mervat Sakr 

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana,Pearl Mafumulu, aliongoza majadiliano ya kimkakati kuhusu ufumbuzi wa vitendo ili kuunda mazingira ya uvumbuzi wa baadaye mnamo Novemba 15 katika Tamasha la Nane la Uvumbuzi lililofanyika kwenye Hoteli ya Hilton Garden Inn huko Durban, Afrika Kusini, mkutano wa uvumbuzi wa kuongoza kwenye mkoa wa KwaZulu-Natata, kuleta pamoja viongozi wa mawazo ya uvumbuzi, wanaharakati wa kijamii, watunga sera, viongozi wa sekta ya umma, pamoja na wajasiriamali kuchunguza na kukuza uvumbuzi katika kanda.

Katika muktadha unaofanana, mada ya Tamasha la mwaka huu ilikuwa chini ya kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni 'Uvumbuzi Kesho, Fungua Leo', majadiliano ya ufunguzi wa kikao hicho kilichoongozwa na Lulu Mafumulo, wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Afrika Kusini, na mjasiriamali kazi yake ya awali imeyejaa kazi mbalimbali wakati wa kazi yake na serikali na mashirika ya maendeleo yaliyojikita kwenye sekta ya ujasiriamali, vijana na namna ya kutengeneza ajira endelevu.

Katika muktadha mwingine, Pearl Mafumulo alialikwa kushiriki kama kiongozi wa mawazo kwenye jopo lingine kwenye tamasha hilo, 'Kuanzisha mkoa kama kitovu cha uvumbuzi', iliyojumuisha wataalam kutoka Manispaa ya Itiquini na Idara ya Maendeleo ya Uchumi, Utalii na Mazingira ya KwaZulu-Natala waliojadili kwa kina kubuni, maendeleo na utekelezaji wa mfumo sahihi wa kusaidia na kuboresha mazingira ya uvumbuzi wa ndani.

Kwa upande wake, Kansela Feliciwe Ndlövo, mwakilishi wa serikali za mitaa kwenye Jamhuri ya Afrika Kusini, alisisitiza umuhimu wa uvumbuzi kwenye kuunda mustakabali wa manispaa, na haja ya kujitolea kwa jiji kusaidia mazingira ya ubunifu, akibainisha umuhimu wa juhudi za ushirika katika kufikia hili, na kuonesha dhamira ya serikali ya kusonga mbele kuelekea hatua za vitendo na mikakati muhimu ili kuongeza ufahamu wa dhana za uvumbuzi wa baadaye na mazingira ya mazingira yetu.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulizinduliwa mnamo Juni 2019 na utekelezaji wa Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri na chini ya ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kama moja ya utaratibu wa utendaji wa kuamsha Dira ya Misri 2030, Kanuni Kumi za Mshikamano wa Afro-Asian, Ajenda ya Afrika 2063, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini wa Umoja wa Mataifa, pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Umoja wa Afrika wa Uwekezaji kwenye Vijana na Mkataba wa Vijana wa Afrika.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy