Harakati ya Nasser kwa Vijana

Harakati ya Nasser kwa Vijana

Utangulizi:

Mapinduzi Matukufu ya Julai 23 yalikuwa mwanzo wa uhuru wa Misri kutoka kwa ukoloni na ujenzi mpya wa serikali, hiyo ndiyo iliyosababisha mabadiliko makubwa na huru katika viashirio vya sera ya kigeni ya Misri, ambapo Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser aliona kuwa Ukombozi wa Misri ulikuwa hatua ya kwanza Kuelekea ukombozi wa Asia,Afrika,na Amerika ya kusini ( Nchi za Dunia ya tatu), ambayo ni hatua muhimu iliyoifuata, kwa hivyo alishughulikia kuunga mkono harakati za ukombozi wa kitaifa na mapambano yake ya uhuru, wakati wa kupatikana mazungumzo ya usawa na ya heshima na nchi za Dunia ya kwanza, na pia alikuza ujenzi wa mfumo wa kisasa wa kitaifa, mfumo huo uliotekelezwa huko Misri na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  ulizinduliwa ili kuuhamishia kwa Vijana wa Dunia.

Kwanini Gamal Abdel Nasser

Harakati hiyo ilishika jina la Kiongozi Marehemu/Gamal Abdel Nasser, akizingatiwa kama mmoja wa viongozi muhimu kwa watu wa nchi zinazoendelea (Afrika - Asia - Amerika ya Kusini), pamoja na kuwa mmoja wa viongozi muhimu wa kipekee,na labda kwa hivyo Kiongozi Gamal Abdel Nasser alistahili jina la "Baba wa Afrika", pia ni kuthibitisha kwa kile kilichopendekezwa na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063, katika azma ya kwanza, iliyoweka umuhimu wa kutoa Shukrani na heshima zetu kwa waanzilishi wa Taasisi ya Umoja wa Afrika.

Pia Abd elNasser ni mfano bora wa kisiasa na kihistoria wa dhana ya uongozi wa mabadiliko na Raia wa Ulimwengu mzima, basi kwa nafasi yake ya uongozi, alitafutia kuunga mkono harakati za ukombozi wa Afrika haswa na Harakati za Dunia ya Tatu kwa ujumla hadi walipopata uhuru wao, na wakati wa zama yake Misri pia ilichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa mashirika yenye ushawishi mkubwa Duniani nayo kwa mujibu wa utaratibu wa kihistoria:

• Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote (1955), iliyokuwa na mchango muhimu katika kudumisha Amani na Usalama wa kimataifa, nayo ililenga kuunda mkondo usioegemea upande wowote - na usio na sera za mataifa makubwa - kwa nchi wanachama unaoelezea mitazamo yao kuhusu  masuala ya kimataifa na maendeleo.

• Shirika la Mshikamano wa Watu wa Afrika na Asia" 1957, ambalo tangu kuanzishwa kwake limekuwa likipigania Amani, na lilisimama haswa kupinga ukoloni, ubaguzi wa rangi na vita.  Pia lilitoa msaada kwa mapambano ya watu wa Afrika, Asia na Amerika Kusini.

• Umoja wa Nchi Huru za Afrika" 1963, linalozingatiwa Shirika la kwanza kuunda mfumo wazi wa Ushirikiano wa Afrika, ambao baadaye ulijulikana kama Umoja wa Afrika.  Ajenda ya Afrika ya 2063, katika kipengele chake cha kwanza kwa jina la "Sauti za Watu waafrika" ilionyesha Shukrani kubwa kwa Waasisi Waanzilishi wa Umoja wa Afrika kwa mafanikio yao ya ukombozi yaliyoondoa utumwa, ukoloni na ubaguzi wa rangi.

• Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu, lililoanzishwa baada ya kuchomwa moto Msikiti wa Al-Aqsa mwaka 1969, kwa ajili ya ushirikiano kati ya Nchi za kiislamu, nalo sasa ni Shirika la pili la kiserikali Duniani baada ya Umoja wa Mataifa kwa idadi ya nchi wanachama.

• Harakati ya Nasser kwa Vijana  (moja ya mapendekezo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa): 

Harakati ya Nasser kwa Vijana ndiyo  mojawapo ya mapendekezo ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ", ambao toleo lake la kwanza lilifanyika mnamo Juni 2019, na ulipokea Ufadhili Waziri Mkuu, Dkt. Mustafa Madbouly, na Udhamini huo haujakuwa programu ya mafunzo tu bali badala yake ulikuwa na nia ya kudumisha uendelevu kwa washiriki baada ya mwisho wa Muda wa Udhamini huo, na kwa kuwekeza katika uwezo wa wahitimu, wahitimu walizindua kwa uhuru harakati ya kimataifa ya vijana wa Nasser.

Matawi yake Barani Afrika yamekuwa yakifanya kazi ya kuzindua shughuli za kuwaendeleza vijana na kuinua ujuzi wao kupitia mafunzo na sifa, pamoja na kuunda ushirikiano na kutafutia njia za ushirikiano kati ya nchi za bara hilo zenye diplomasia safi ya vijana, lililosababisha mafanikio makubwa, yaliyofanya sifa yake kuwa maarufu mahali pote , na mnamo Juni 2021, baada ya kumalizika kwa toleo la pili kutoka kwa Udhamini wa Nasser, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi, Rais wa Jamhuri, Harakati ya Nasser ilipanua ikawa huko nchi za Asia na Amerika ya Kusini, kufikia toleo lake la tatu,lililofanyika Juni 2022, ambapo vijana wa Nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki walishiriki, hadi matawi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana yalipofikia hadi sasa karibu na  nchi 52 Duniani kote.

Rejeo la Harakati ya Nasser kwa Vijana

Harakati ya Nasser inakuja kama moja ya mienendo iliyozinduliwa kutoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa mujibu wa Dira ya 2030 ya Misri, kuamsha matarajio ya Ajenda ya 2063 ya Afrika, na masharti na malengo ya "Hati ya Vijana wa Afrika" huu mfumo wa kisheria wa uwezeshaji wa vijana, na sambamba na ramani ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya uwekezaji kwa vijana, pamoja na Kuamsha Kanuni Kumi za Mshikamano wa Afro-Asia "Kanuni za Bandung"pamoja na kuwa mojawapo ya mbinu za kuamsha Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pamoja na kushughulikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, basi kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana inazingatiwa kama Jukwaa la kimataifa linalokusanya Vijana; kukuza ujuzi wao na kuinua ufanisi wao pia kuwawezesha vijana viongozi kufikia Maendeleo, ikifanya "Raia wa Ulimwengu mzima" mshawishi zaidi.

Malengo ya Harakati ya Nasser kwa Vijana:

1-Kukuza viunganishi vya kihistoria na kusaidia mahusiano ya pande mbili kati ya Misri na nchi nyingine ndugu na rafiki.

2-Kutambulisha ajenda za maendeleo, mikataba ya kikanda na kimataifa katika ngazi ya watu wenyewe (Mkataba wa Biashara Huria), na Mkakati wa Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa (Kusini – Kusini).

3- Kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi Duniani, na watoa maamuzi na wataalam wa ndani, kikanda na kimataifa.

4- Kuamsha mipango iliyozinduliwa na Umoja wa Mataifa, Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, Shirika la Mshikamano wa Watu wa Afro-Asia na Umoja wa Afrika haswa katika vipengele vinavyohusiana na vijana, wanawake, hali ya hewa, elimu, amani na usalama, utawala na ujasiriamali.

5- Kuunda jukwaa la kimataifa la vijana kwa kuongeza kanuni za Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na Mshikamano wa Afro-Asia.

6- Kubadilishana uzoefu wa vijana Duniani kote ili kujumlisha wanamitindo waliofanikiwa, kwa kuzingatia tofauti za ndani.

Matawi ya kitaifa ya Harakati ya Nasser kwa Vijana iliyozinduliwa na waamini wa wazo hilo:

 Harakati ya Nasser kwa Vijana ni kielelezo cha maendeleo kilichozinduliwa tangu miaka mitatu iliyopita, tangu Julai 23, 2019 ili kuunda mtandao mpya wa kuunganisha vijana na unaoweza kufanywa upya, wa maadili, mshikamano, na kutofungamana kwa upande wowote, hivyo Harakati hiyo kupitia waratibu wake iliweza kuhakikisha ushawishi mkubwa ndani ya karibu na nchi 53 hadi sasa ndani ya Mabara manne , Asia, Afrika, Amerika ya Kusini. na Australia, ambapo kila mmoja wao alifanya kazi ndani ya uwanja wake ya ushawishi na uwezo wa nchi yake, na kwa mujibu wa mahitaji ya jamii yake, akiwasilisha kwao ikisiri ya uzoefu wa Misri katika maendeleo na kujenga taasisi za kitaifa, basi walizindua mipango kadhaa ya maendeleo katika uwanja wa uwezeshaji na ukarabati wa vijana na ujasiriamali ili kuhudumia wana wa nchi yao.

Mgawanyiko wa kijiografia

A) Bara la Afrika, linalogawanywa katika kanda 5, ambapo Harakati ya Nasser yaenea katika nchi zake kadhaa:

1- Kanda ya Afrika Kaskazini, ambayo ni pamoja na matawi ya Harakati huko (Algeria - Morocco - Tunisia - Libya - Mauritania – Sudan).

2- Afrika Mashariki (Rwanda - Burundi - Uganda - Sudan Kusini - Somalia - Djibouti  Kenya -Tanzania).

3- Kanda ya Afrika ya Kati (Chad - Congo - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – Camerun).

4- Afrika Magharibi (Nigeria - Niger - Cote d'Ivoire - Sierra Leone - Ghana - Guinea - Senegal - Togo ).

5- Afrika Kusini (Malawi - Namibia - Afrika Kusini - Zimbabwe - Zambia).

B) Bara la Asia: ambapo Harakati ya Nasser kwa Vijana yaenea katika nchi za : (Azerbaijan - Uzbekistan - Kazakhstan - Pakistan - Bangladesh   - Afghanistan - Indonesia - India - Vietnam - Thailand – Armenia )

C) Ama kwa nchi za Ulimwengu wa Kiarabu, matawi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana hadi sasa yamefika katika nchi (Iraq - Palestina - Lebanon - Saudi Arabia - Jordani - Usultani wa Oman - Yemen - Saudi Arabia).

D) Nchi za Amerika ya Kusini, hadi sasa inajumuisha (Ecuador – Colombia – Brazil ).

Moja ya hadithi muhimu za mafanikio ya Harakati ya Nasser kwa Vijana

 Kwa kuamini kwa Vijana wa Harakati hiyo kwa Jukumu kubwa la  umuhimu wa kutoa nafasi kwa ubunifu wa kiakili na maarifa, na umuhimu wa kuweka kumbukumbu za shughuli zote za uwanjani, kufufua urithi wa kihistoria wa Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser katika roho ya kisasa na ya ujana, tovuti rasmi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana (https://nasseryouthmovement.net/) ilizinduliwa katika lugha tano (Kiarabu - Kiingereza - Kifaransa - Kiswahili - Kihispania), imekabidhiwa kuwa jukwaa la kimataifa la vijana, kuweka kumbukumbu na shughuli za Harakati ya Nasser katika  mahali popote, na kufuatilia athari zao, na aidha kuruhusu vijana, washawishi, viongozi, watafiti na wanafikra kutoka Duniani kote katika nyanja mbali mbali, Kutoa maoni na uchambuzi wao, na kushiriki nakala zao za kisayansi na michango ya kifasihi kupitia jukwaa lenye kichwa "Makala na Maoni" lililoundwa ndani ya sehemu ya "Raia wa Ulimwenguni mzima", liko wazi daima kupokea Ushiriki kupitia kupeleka makala ili kuchapishwa kupitia barua pepe:

 Articles@nasseryouthmovement.net

Kujiunga kwa  Harakati ya Nasser kwa Vijana

Ikumbukwe kwamba kazi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana haiishii hapo tu, bali inaweza kukua zaidi na iendelee na kazi yake kwa mujibu wa nyaraka na marejeo ambayo tunayategemea na kwa mujibu wa mipango ya maendeleo ya Jumuiya. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Shirika la Watu wa Afro-Asia, hivyo mlango wa kujiunga na Harakati ya Vijana ya Nasser bado uko wazi Mbele ya vijana wote kutoka pande zote za dunia wenye shauku ya mabadiliko na wanaoamini katika kanuni za kuto- usawa na umuhimu wa umoja na mshikamano kwa ulimwengu wa amani na usalama.

Vijana wanaojiunga na Harakati ya Vijana ya Nasser pia wananufaika kutokana na mitandao na kufanya kazi pamoja na viongozi wa vijana wenye nguvu na ushawishi wa kimataifa, kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana utaalamu, uzoefu na tamaduni.

 Kwa taarifa za hivi karibuni....

"Mmoja kwa ajili ya Wote .. na Wote kwa ajili ya Mmoja."