Samora Mashel: Kiongozi wa Mapinduzi

Samora Mashel: Kiongozi wa Mapinduzi

"Miongoni mwa tuliyoyafanya, Historia itakumbuka njia ya kubadilisha mapambano yenye silaha kwa mapinduzi ya kimaendeleo, yaliyochangia kujenga jamii mpya; basi kwamba Vita vya Ukombozi tulivyoshikilia havikuwa kwa ajili ya kubadilisha dhuluma ya kireno kwa dhuluma ya kisumbiji, au dhuluma ya kiulaya kwa dhuluma ya kiafrika, wala hata dhuluma ya kizungu kwa dhuluma ya kitaifa, basi Umoja na Ushindi ni lengo moja."

( Kutokana na hotuba ya kiongozi msumbiji Samora Mashel mbele ya nchi yake.)

"Samora Musis Mashel", mwenye lakabu ya rais Samora", alizaliwa tarehe ya 29,mwezi wa Septemba (9), mwaka wa 1933,kwenye kijiji ndani ya Kata ya Ghaza, kusini mwa Musumbiji, alikufa tarehe ya 19, mwezi wa Oktoba (10), mwaka wa 1986, kutokana na familia fukara inayofanya kazi ya Kilimo. Na ili kuweza kuendelea katika Elimu yake, alifanya kazi mchana kama Muuguzi wa Hospitali moja ya Musumbiji, ili kuweza kusoma usiku katika shule moja, mpaka alihama nchi zake, na alijiunga Mapambano ya kitaifa. Alijulikana kwa Askari mgumu, Msemaji mwenye Ushawishi,basi yeye ni mtu wa kijeshi na mtu wa Mapinduzi na Ujamaa dhidi ya Ubaguzi na Ukabila, kama yeye ana lakabu nyingi, miongoni mwao ni ( Kiongozi wa Mapinduzi).

Kabla ya kuwa rais wa kwanza wa jamhuri huru ya Musumbiji mwaka wa 1975, - baada ya Uvamizi wa kireno ulioendelea hivi karne nne na nusu -, alijiunga kama mwanaharakati katika kando ya Ukombozi ya kimusumbiji kwa Uhuru kutokana na Ureno, na inayojulikana kwa Jina la ( Alferlimo), iliyopelekwa kwa Misri na Algeria ili kupata mafunzo ya kijeshi, na baadaye alikuwa rais na kiongozi wake mwaka wa 1969, pamoja na msaada wake kwa harakati za Ukombozi barani, khasa harakati za Ukombozi katika kusini mwa Afrika na Zembabwe. Basi akida yake ngumu ilikuwa kama Imani kubwa kwamba Musumbiji haitapata Uhuru wake wa kweli ila baada ya kuwakomboa wanyonge - siyo katika bara jeusi tu, bali nje yake pia - na kwa ajili ya itikadi yake hii, Musumbiji ilikuwa kimbilio yenye Amani kwa harakati zote za Ukombozi.

Anazingatiwa mwanzishi mmoja wa Taasisi ya Umoja wa kiafrika -Umoja wa kiafrika hivi sasa-, ulioundwa baada ya mwaka mmoja wa mapendekezo ya ( mkutano wa Adis Ababa) , mwezi wa Mei(5), mwaka wa 1962, na Adis Ababa ulichaguliwa kama kituo cha Taasisi hii mnamo 1963, kupitia kutia saini mkataba wake mkuu.

Pia inatajwa kwamba yeye alifanya marekebisho mengi kwa ajili ya kurudisha Usalama wa kitaifa kwa nchi zake, basi aliangalia Afya, Elimu, na alifanya maendeleo katika taasisi za kielimu na hospitali. Na kulingana na harakati za Nasser nchini Misri, Samora alizitaifisha ardhi zote za taifa na Rasilimali za nchi; lililomfanya kuwana umaarufu mkubwa wa nchi yake, pia lilisababisha kumheshimu toka nchi yake baada ya kifo chake, kupitia kuunda masanamu kadhaa kwake katika medani zote, na kuyabeba mabango tofauti yenye kauli kama:(Samora hajafa, bali yumo moyoni mwetu), na kutoa Jina lake kwa mabarabara na taasisi nyingi. Inatajwa pia kwamba yeye alipata Tuzo na Nishani kadhaa, nazo ni kama: Tuzo ya (Lenin) kwa Amani, Nishani ya Msalaba adhimu kutokana na cheo cha kustahiki kwa jamhuri ya kiitalia, na Nishani ya Khose Marti.

Mnamo Agano la rais mmisri aliyekufa "Gamal Abd Elnaser ", Misri ilizikaribisha harakati za Ukombozi za kimusumbiji hata kabla ya kuungana kwa Jina la (Ferlimo), pia ilifungua ofisi ya Umoja wa kidemokrasia wa kitaifa kwa Musumbiji, na kushughulika ndani yake Makada wake wa vyombo vya habari na siasa. Na Misri ilichukua jukumu la kuwawezesha, kuwafundisha, na kutoa njia zote za msaada wa kisiasa na kisanaa mpaka Musumbiji ilipata uhuru wake, Misri ilikuwa ya kwanza ya kuitambulisha. Na Misri imefungua Ubalozi kwake kwenye mji mkuu ( Maputu); basi ulikuwa Ubalozi wa kwanza wa kiarabu nchini Musumbiji, na baadaye imetia saini mikataba tofauti pamoja, nayo ni kama: mkataba wa Ushirikiano kati ya sanduku la kimisri na Ushirikiano wa kiufundi pamoja na Afrika na Musumbiji mwaka wa 1985.