Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wazindua fomu ya maombi ya toleo la nne
Leo Jumanne asubuhi, Wizara ya Vijana na Michezo imetangaza kuzindua fomu ya usajili kwa toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, pamoja na kauli mbiu ya “Vijana Wasiofungamana kwa Upande Wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini”, nao unawalenga vijana viongozi wenye taaluma tofauti za kiutendaji tena vijana wenye ushawishi katika jamii kutoka mabara yote ya Dunia, na unatarajiwa kufanyikwa Juni ijayo.
Kwa upande wake, Mwanzilishi na Mratibu mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , Bw.Hassan Ghazali, alieleza kuwa Udhamini huo unakuja ikiwa ni moja ya taratibu za utekelezaji wa mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri; kusaidia uwezo wa Vijana waafrika, na kuwawezesha kuunda maoni ya kina na muhimu kuhusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya Maendeleo Endelevu, pamoja na kusaidia fursa za kukuza Nafasi ya Misri Duniani kote, akisisitiza kwamba unakuja ndani ya mfumo wa utekelezaji wa Dira ya Misri ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Ushirikiano wa Kusini - Kusini.
Na Ghazali aliongeza, akibainisha kuwa Udhamini huo unawalenga vijana wa kiume na wa kike kutoka nchi zote zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki ambao ni watoa maamuzi katika sekta ya umma, wahitimu wa Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi watendaji katika sekta binafsi, wawakilishi wa matawi ya kitaifa ya Mtandao wa Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, wanaharakati wa asasi za kiraia, wakuu wa Mabaraza ya Vijana ya Kitaifa, wanachama Mabaraza ya Mitaa, viongozi wa vyama vya vijana, Wanazuoni katika Vyuo Vikuu, watafiti katika vituo vya Tafiti za kimkakati na fikra, wanachama wa vyama vya wafanyakazi, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, wajasiriamali wa kijamii, na wengine.
Ghazali alihitimisha, akionesha kwamba wale wanaotaka kushiriki au kufahamu maelezo zaidi kuhusu kujiandikisha na kujaza fomu wanaweza kutembelea kiungo kifuatacho: