Kipindi cha nne "Jukumu la Diplomasia ya Vijana katika Kukabiliana na Migogoro ya Kimataifa"

Kipindi hiki kinazingatia Diplomasia ya vijana, jukumu lake wakati wa migogoro ya kimataifa na changamoto zake kuu, haswa wakati wa Janga la virusi vipya vya Corona.

Kipindi hiki kilimkaribisha mmoja wa wanaharakati mashuhuri wa Urusi, Dkt. "Roman Shikov", Mwanachama  Mwanzilishi wa " Marafiki wa uongozi, na hii ni mtandao wa Makada wa vizazi wajao wa kimataifa, na wenye miradi ya kijamii; ili kubadilishana mbinu za utekelezaji bora zaidi. Yeye pia ni Mwenyekiti wa uongozi wa Kituo cha kuendeleza mipango ya Kimataifa (Ruspromo Foundation).

Wakati wa Mazungumzo yake yanayohusu Diplomasia ya Vijana, Dkt "Roman Shekov" alisema: "Ni njia na mbinu kwa vijana; ili washirikiana , iwe katika ngazi ya pamoja au pande mbalimbali. Mashirika yoyote ya kikanda au kimataifa, kama Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika. au Umoja wa Mataifa unaojumuisha mazungumzo  ya vijana yanaweza kuchukuliwa kama  uungaji mkono wa vijana.

Kipindi kilishuhudia mwingiliano mkubwa kutoka hadhira; kwani maswali mengi ya mada ya kipindi yalipokelewa, na kujibiwa.

Ni vyema kutambua kuwa, Orodha ya wenyeji wa Programu ya " Raia wa Ulimwengu mzima " inawajumuisha waundaji uamuzi na viongozi wa vijana kutoka nchi mbalimbali Duniani na katika nyanja mbalimbali;  kwa lengo la kufikisha ujumbe chanya kwa vijana Duniani ili kuunda uhusiano kati ya vijana na wafanya uamuzi.

Vipindi vya programu hiyo vinasimamiwa na Mwandishi wa habari wa Gazeti la " Al_ Egyption" ,

" Amira Sayed" , ambalo ni gazeti la kwanza la lugha ya Kiingereza katika Mashariki ya Kati, pamoja na kuwa mwakilishi wa Misri katika Bunge la Vijana la Kimataifa la Maji, na alishiriki katika kuandika shughuli nyingi za kimataifa katika ndani na nje ya Misri.