Misri ni lango la Afrika la kuisafirisha China

Misri ni lango la Afrika la kuisafirisha China

Imetafsiriwa na/ Mahmoud Ragab
Imehaririwa na/ Fatma Elsayed

Katika maadhimisho ya miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, tunakumbuka hatua muhimu zaidi za maendeleo ya mahusiano ya Misri na China, kwani Misri inachukuliwa kuwa nchi ya ishirini na tatu kwa kutambua Jamhuri ya Watu wa China na ya kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika.

Mnamo tarehe Aprili 1955, Gamal Abdel Nasser na kiongozi wa China Xu Enlai, waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa China, walikutana Bandung, Indonesia, wakati wa mkutano wa kilele wa Afrika na Asia kujadili njia za ushirikiano.

Mnamo tarehe Mei 1956, mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulianza baada ya serikali za Misri na China kutoa taarifa ya pamoja kuhusu kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia katika ngazi ya balozi kati ya nchi hizo mbili, na hatua hii ilikuwa hatua muhimu katika mahusiano ya kimataifa wa China, kwani jukumu la Misri katika ngazi za Kiarabu na Afrika lilikuwa na athari kubwa kwenye uwanja wa kimataifa, na Jamhuri ya Watu wa China ilitambuliwa baada ya hapo.

Mnamo tarehe Julai 1956, China iliunga mkono uamuzi wa Rais Gamal Abdel Nasser wa kutaifisha Mfereji wa Suez na kulaani vikali uchokozi wa mara tatu dhidi ya Misri, na msaada wa watu wa China kwa Misri uliibuka wakati moja ya maandamano makubwa nchini China yalitoka kulaani uchokozi na kuunga mkono mapambano ya watu wa Misri.

Misri pia ilitaka kupatanisha mgogoro wakati wa Vita vya Indo-China vya 1962, na Rais Nasser alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Xu Enlai na Lal Bahadur Shastri, Waziri Mkuu wa India.

Xu Enlai pia alitembelea Misri mnamo tarehe Desemba 1963, wakati ambapo alifanya mazungumzo na Rais Gamal Abdel Nasser na kutoa hotuba aliyosema: "Hii ni mara ya kwanza kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu na mara ya kwanza nimetembelea bara la Afrika, na ningependa kuelezea, kwa niaba ya watu wa China, salamu zangu za joto na heshima kubwa kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu."

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili na ushirikiano katika nyanja mbalimbali pia umeendelea, kupitia kubadilishana ziara za ngazi ya juu na kubadilishana wanafunzi, wataalamu, utamaduni na wajumbe wengine.

Kwa upande wa kiuchumi, China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Misri, na Misri ni mshirika wa tatu mkubwa wa kibiashara wa China barani Afrika, na kiasi cha ubadilishaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili kiliongezeka kutoka dola milioni 12.2 mwaka 1954 hadi dola milioni 452 mwaka 1955, na kisha kufikia zaidi ya dola bilioni 10 mwaka 2013, ikimaanisha kuwa imeongezeka mara elfu moja katika kipindi cha miaka sitini iliyopita.


 Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy