Ziara ya Rais AbdelNasser Kwa Ufalme wa Saudi Arabia mnamo Mwaka 1956

Ziara ya Rais AbdelNasser Kwa Ufalme wa Saudi Arabia mnamo Mwaka 1956

Imetafsiriwa na/ Naira Abdelaziz 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 


Rais Gamal AbdelNasser aliwasili mnamk Septemba 22, 1956, kwenye Uwanja wa Ndege wa Dhahran kupitia ziara rasmi ya Ufalme wa Saudi Arabia, na akapokelewa na Mfalme Saud Bin Abdulaziz ,Rais wa Syria Shukri al-Quwatli, na umati mkubwa wa wana wafalme na watu mashuhuri wa Saudia huko nchini Saudi Arabia.

Muziki wa kijeshi ulipiga wimbo wa kitaifa wa nchi hizo mbili, likahama maandamano la Marais  kutoka  Uwanja wa Ndege  katikati ya jiji kati ya umati wa watu, walikuwa zaidi ya raia elfu kumi, Marais hao walitumia usiku  mmoja mjini Dammam, kisha kuelekea katika mji mkuu wa Riyadh.
Walipokelewa na wanafamilia kifalme na viongozi wa Saudia nje ya eneo la uwanja wa ndege,  hukutana na watu zaidi ya 20,000 kwa mailikio mkubwa iliyofika angani kumsalimia Mfalme na Marais Gamal Abdel Nasser na Shukri Al-Quwatli.

Marais walifanya mijadala na mikutano kadhaa kuhusu masuala ya kisiasa na kijeshi yanayoihusu nchi. mwanzoni mwa mijadala hii ilikuwa ni suala la Mfereji wa Suez, na kulikuwa na makubaliano kamili juu ya uungwaji mkono kamili wa Misri katika misimamo yake yote.

Jioni, taa za Ikulu ya Mfalme Saud ziliangazia usiku katika mji mkuu kusherehekea uwepo wa Rais Nasser na Rais Quwatli,  chakula cha jioni kilifanyika kwa heshima yao, kilichohudhuriwa na wanafamilia na wakuu wa ufalme .


Alasiri ya siku ya pili, Mfalme Saud aliandamana na Rais Gamal Abdel Nasser hadi Uwanja wa Ndege wa Riyadh kumuaga baada ya kumalizika kwa ziara yake rasmi katika Ufalme wa Saudi Arabia na kurejea Kairo.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy