Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini

Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini
Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini
Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini
Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini
Boma la Qaitbay… Mlinzi wa Misri mwa kaskazini

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled

" Nani alinda Misri kutoka kwa wavamizi mwa kaskazini...waturuki wapo mashariki na wazungu wapo magharibi “ na hayo yaliyosemwa na Sultani Al-Ashraf Abu Al-Nasr Qaitbay aliposimama ufukweni mwa Alexandria akiangalia vifusi vya husuni zake baada ya kutukia tetemeko gumu zaidi la ardhi kwa hiyo aliamuru kuanzisha boma hilo ili kuulinda mji huo wa Alexandria kutoka kwa uvamizi wa nje haswa Milki ya Osmani iliyoanza kubadilisha mwelekeo wa vita vyake kutoka Ulaya kuelekea mashariki kwa hivyo Sultani Qaitbay alijaribu kuyalinda mapengo ya Misri na lilijengwa kamili baada ya kupita miaka miwili ndani ya mwaka 884 hijiria/1497 , na lilijengwa juu ya ukubwa wa kilometa 17555 mita mraba kwa gange pamoja na kuimarisha mnara kwa baadhi ya nguzo za marumaru zilizobaki kutoka mnara wa kuongozea meli, na juu ya ukubwa huo zilijengwa kuta za nje na za ndani za boma hilo na mnara mkuu, ambapo kuta hizo zilijengwa ili kukuza nguvu za boma, na zilijengwa kwa mawe makubwa, na kuhusu umbo lake la nje boma hilo linajumuisha kwanza kuta za nje, ambapo kulikuwa na kuta za nje katika mielekeo minne mikuu ya dira, upande wa mashariki: ukuta wa nje unaangalia bahari moja kwa moja, na upana wake ni takribani mita 2 , na urefu wake takribani ni mita 8, na ukuta huo hauna minara yoyote na aghlabu ya sehemu zake ziliporomoka halafu zilikarabatiwa tena hivi karibuni, na upande wa magharibi unaangalia bandari kale ya mashariki, na ndani ya majengo yake kuna mbao , na vigogo vya mtende , na pia kuna minara mitatu wazi na yenye umbo la nusu duara na ina mapengo ya kurushia mishale, na sehemu hii inazingatiwa kama sehemu kuukuu zaidi kuliko zingine ukutani kwa ujumla, na ndani yake kuna lango kuu la boma mwishoni mwa upande wa magharibi mwa kusini.

Upande wa kaskazini, unaangalia bahari moja kwa moja, na una sehemu mbili, sehemu ya chini ni kivuko kikubwa kinachopanua katika urefu wa ukuta kutoka mashariki mpaka magharibi, vinaitwa kwa vivuko vya baharini, na kilijengwa juu ya mwamba , na kilitobolewa mapengo kwa umbo la  miraba , kila moja lina pengo lenye mviringo linaloangalia nje na yalitumika kama mapengo ya mizinga , na yalifikia mapengo 20, na mwishoni mwake kuna nyumba ya farasi, na sehemu ya juu ya upande huo ni vivuko vyenye mapengo ya kubana yanayoangalia  bahari na yanatumiwa kama nafasi za kurushia mishale , na upande huo ulikarabatiwa tena , na upande wa kusini ni wa muhimu zaidi kwa kuta za nje , kwa sababu unaangalia moja kwa moja bandari ya mashariki, na unapanua kutoka upande wa mashariki mpaka upande wa magharibi katika safu moja , na una minara mitatu wazi ya mviringo, na pia ina baadhi ya mapengo ya kubana ya mviringo, na katikati yake kuna lango la sasa la boma.


 boma hilo lina mnara mwenye umbo la nane linalopatikana katika kuta za nje kutoka upande wa kaskazini mwa magharibi, na lina umbo la nane,  na ulikuwa na lengo la usimamizi na kuweka nguvu , na pia ulikuwa lango la asili la boma ambalo halitumiki kwa sasa , na linapatikana katika upande wa kusini mwa magharibi kutoka ukuta wa nje,  na ina pengo la mstatili linalozungukiwa na mnara wazi na mwenye pande za duara, na lango hilo linapelekea kivuko cha kuingia bomani kwa njia ya mlango unaoelekea ua wa boma , na mapengo mengine yanayoelekea eneo linalopatikana kati ya kuta mbili, na lango hilo sasa linatumiwa na wizara ya utafiti wa kisayansi kama jumba la sanamu , lakini lango la sasa la boma linapatikana kati kati ya upande wa kusini wa kuta za nje za boma , na ni pengo ambalo juu yake kuna tasa inayofungwa mlango mkubwa wa ubao mwenye pande mbili, lakini umbo lake la mbele kuna mkufu usiokamilika , na mbele ya lango hilo kuna pengo linaloelekea ukuta wa ndani wa boma , na lina umbo la mkufu wa nusu duara, unaoelekea chumba chenye nusu silinda  kilicho chini ya ardhi ambacho kipo katikati ya safu ya vyumba maalumu vya wanajeshi, na mwishoni mwake kuna ua wa boma , na juu ya lango hilo kuna mchoro  wa marumaru ambapo una azimio la Sultani  Qansuh Al-Ghuri mwaka 907 hijiria/1501 akionya kwa kutoa silaha kutoka boma akitishia kwa kitanzi mtu yeyote anafikiria hilo. 


Umbo la boma la ndani linawakilishwa katika kuta za ndani, zilizojengwa kwa mawe makubwa ya chokaa , yanayozunguka mnara kutoka pande zake zote isipokuwa upande wa kaskazini, na kuta hizo zinatumika kama safu ya pili ya ulinzi ili kukuza mnara mkuu, na zinatengwa na kuta za nje kwa umbali wa takribani mita 5 au 10 , na hivi karibuni kuna baadhi ya pande zinazokaribiana ziliongezwa kwa kuta hizo, pande hizo zilianzishwa baada ya kujengwa kwa boma, na labda hurejea zama ya utawala wa Mohamed Ali , na idadi zake ni 36 zilianzishwa kama ili kuwa kama makazi ya askari, na zina umbo la mstatili, na zinaangalia moja kwa moja ua wa boma kwa milango yenye mapengo ya mstatili ina milango ya ubao ina kilango kimoja, na mbele yake kuna mapengo madogo ya kuingiza hewa na mwanga , na pia kando ya mlango huo kuna dirisha la mstatili lenye mbao mbili , na zinaangalia ua wa boma ili kuingiza hewa , na sehemu hizo ziliezekwa kwa baa la silinda , na moja ya sehemu hizo iliundwa ili iwe mfano wa kuuza sanamu zilizoigwa na kuundwa katika kituo cha kutengeneza mabaki kinachohusiana na wizara ya mabaki .

 Ua mkuu huo wa boma , una nafasi kubwa ya mraba inazungukia mnara mkuu kutoka upande wa kaskazini, na katika upande wa mashariki inapatikana ngazi yenye madaraja 22 yanaelekea kuta za nje,  na katika upande wake wa kusini wa magharibi kuna mteremko unaoelekea kuta za nje, na nafasi hiyo ilitumika wakati wa nyuma ili kufanya mazoezi ya kupambana kwa askari, na ndani ya yaliwekwa majeneza mengi yanayorejea zama na maumbo tofauti, kama umbo la kinu kwa Armstrong, na pia madhabahu ambayo ni mojawapo ya maeneo makuu bomani , na inapatikana katika upande wa magharibi nje ya mnara mkuu, na iligunduliwa wakati wa ukarabati uliofanyika mnamo kipindi cha katikati, mnamo1982-1984 , na ilijengwa kwa mawe mekundu, yaliyofunikwa kwa kuba 10 kubwa za matope zinasimama kwenye mikufu , na upana wa madhabahu hiyo unafikia takribani sentimita 4,5 na urefu wake ni 13,10 kuzidisha sentimita 5,5 , na mchanganyiko huo wa sementi na mchanga mwenye rangi ya waridi ulitumika kuimarisha kuta zake , na kuhifadhia maji safi kwa muda mrefu zaidi , ambapo lengo kuu la madhabahu hiyo ni kuhifadhia maji kwa , kutokana na kutokuwepo kwa chanzo cha kudumu cha maji , na madhabahu hiyo ilijazwa maji yaliyobebwa na ngamia na pia kwa mvua zinazoingia katika mapengo yake , na inasafishwa baada ya kupita kwa miezi mitatu, kupitia kivuko cha nje kinachoelekea madhabahu kupitia ngazi iliyochimbwa kutani, na pia kuna kivuko kingine ndani ya mnara ili kurahisisha kufikia kwa maji mnarani. 


 Kuhusu mnara mkuu unaopatikana katika upande wa kaskazini mwa mashariki ndani ya kuta za ndani za boma, na ulijengwa juu ya vifusi vya mnara wa Alexandria wa kuongezea meli , ambapo ni jengo lenye umbo la mraba na lina maghorofa matatu , urefu wa ncha yake ni mita 30 , na urefu wake ni mita 17 , na wakati wa kuujenga lilijaliwa sana kuwa ncha zake zielekea mielekeo minne mikuu ya dira, na kila upande kutoka pande zake una mnara wa silinda mrefu zaidi kuliko mnara wa asili , na unasimama juu ya mawe makubwa, idadi zake chini ya kila mnara ni 12 , na upana wa kila mnara ni mita 6 , na katika kila ukuta wa mnara huo kuna madirisha matatu yanayoangalia ua wa nje wa kila mnara na yapo mbele ya madirisha ya mnara mkuu, na mnara huo uliimarishwa kwa baadhi ya nguzo zilizobakia kutoka mnara wa kuongozea meli, ili kuimarisha kuta za mnara , na katikati mwa lango la sasa la mnara katika upande wa kusini kuna lango la msingi, baada ya kutotumia vilango vya pande , na ni lango linalokuwa na ukubwa zaidi ya mita 3 juu yake kuna mkufu mwenye ncha,  kati yake kilango cha mstatili, kina mlango mkubwa wa mawe, na juu ya yake mkufu mwenye shanga, na kutoka pande zake na juu yake pia kuna baadhi ya mawe ya matale yenye rangi ya waridi, (huenda kuwa ni msingi wa mnara ) na katika pande mbili za mlango kuna vinara viwili kila kinara ni sentimita 80, na pande za kaskazini na za mashariki za nje zinafanana na lango kuu , na maandishi ya sheria yaliandikwa kwa kutumia mawe na juu yake yanapatikana safu za mawe zenye umbo la yai .

 Umbo la ndani la mnara mkuu lina maghorofa matatu yanayotofautiana katika umbo na urefu, ambapo urefu mdogo wa maghorofa haya unafikia mita 7 na seneti 20 , na ghorofa la kwanza lina maeneno muhimu sana kama mfano:  kilango kinachofuata lango kuu, na ardhi ilisakafiwa na marumaru mweupe mwenye nakshi, na sakafu hii inazungukiwa na wigo mweusi wa marumaru, na pia inapakana na vizingiti vya mawe kutoka  pande 3, na juu ya kila kilango kuna vilango viwili.

• Kabati za ukutani, na pengine jambo muhimu zaidi ghorofani ni  uwepo wa  msikiti kwa ajili ya kufanya ibada, Kwa wale wa askari  wanaoishi katika ngome, mpangilio wa msikiti huu unajumuisha ua na Iwan  , na sakafu ya ua wake ni  ya marumaru yenye umbo la sahani kubwa ya nyota.  Na kati kati ya mahali mwa imamu ni kishubaka kilichozungukwa na nguzo mbili za marumaru.Pia mwanzo wa   iwan ya kaskazini ya magharibi ni chumba cha mstatili kilichokuwa kikitumika kuhifadhi zana za msikiti huo, ikiwa ni pamoja na mikeka na mafut, na.Katika iwan ya kaskazini mashariki kuna  chumba kinachotumika kwa ajili ya makazi ya imamu. Ya msikiti.Ghorofa hii ina ukumbi unaowakilisha kivuko  kidefu kinachoendana na kuta za kaskazini na  kivuko  cha magharibi kina upenyo wa kisima cha silinda chenye wigo wa marumaru unaoelekea kwenye madhabahu inayo nje ya mnara. Ili kurahisisha jambo la   kuleta maji ndani ya mnara,Na chumba cha kusagia katika upande wa kusini katika kivuko cha magharibi, ambacho ni chumba chenye umbo la mraba, kama ilivyoonyeshwa na mwanahistoria Ibn Iyas, na chumba hiki kiliteuliwa kwa ajili ya kusaga nafaka zinazohitajika kwa ajili ya kuliwa na askari, ambayo kiko upande wa kulia wa ndani ya mlango mkuu wa mnara, kinapakana na vyumba vitatu vidogo vya mstatili.Ghorofa hii pia linajumuisha ngazi ya mawe inayoongoza kwenye ghorofa la  pili.

• Ghorofa la pili linafikiwa kupitia ngazi ya mawe yenye madaraja ya juu, Inajumuisha vivuko  vya kando kando ya pande hizo nne, na vivuko vidogo vinaunganisha  vivuko na minara ya kona, Kuta za ghorofa hilo  lina mashimo ya kurushia  mishale dhidi ya maadui,  Katikati mwa ghorofa hilo kuna vyumba vidogo vinavyozunguka, mhimili moja, unajumuisha  dirisha la kati, ambalo linapatikana juu ya ukumbi wa msikiti kwenye ghorofa la kwanza.Ghorofa hili linajumuisha kutoka upande wake wa kusini, mtego wa mafuta, ambao ni upenyo mwembamba wa mstatili juu ya lango kuu la mnara, na ulitumika kama njia ya ulinzi kwa kudondosha mafuta yanayochemka na mada nyingine juu ya adui akipenyeza kuelekea mnara mkuu, na njuga (kipuli cha hewa), kilicho katikati ya upande wa kusini, kilitumika kama njia ya mawasiliano. Kati ya ghorofa la kwanza na ghorofa la pili, pamoja na njia ya ulinzi ikiwa kuna haja.

• Na kuhusu ghorofa la tatu, linafikiwa kupitia ngazi ya   mawe yenye madaraja ya juu, ghorofa hilo  lina  baadhi ya vivuko  vinavyozungukwa na safu ya  vyumba  28   vya mraba, ambavyo vingine vinatazama nje kupitia uwazi mdogo wa mstatili,  na hutumika kama vyumba vya kutazama, na vingine hutazama ua wa msikiti kupitia upenyo wa mstatili ambayo una  dirisha la mbao lenye grili za mbao, vyumba hivi vilitumika kama kambi za askari na maduka ya silaha. Katikati ya upande wa kusini, ambayo Ibn Iyas akisema Kiti cha Sultani, Ukumbi huu mkubwa ni chumba cha mstatili kina urefu wa mita tano na upana wa takriban mita nne. Ina paa la matofali kwa namna ya kuba yenye pande zisizofanana , inayosimama juu ya   matao manne yaliyounganishwa kwenye kuta

Na Katika ukuta wa kusini wa jumba hili, kuna madirisha mawili makubwa ya mstatili yalifunguliwa, kila moja ikiwa na upinde mdogo wa mawe.Madirisha haya mawili yalitokeza kutoka usawa wa ukuta kwa takriban nusu mita, na sehemu hiyo iliegemea juu ya jozi nne za nguzo za mawe. Ibn Iyas anafafanua kiti hiki, akisema: “Kiti kinachoelekea baharini, ambacho mwendo wa siku moja unaweza kuona mashua za Wazungu zikiingia ndani ya maji,” tanuri, na mnara, kwani mnara mkuu ulikuwa umefunikwa na mnara, nao ukabaki. Hadi wakati wa kampeni ya Ufaransa. Lakini ilitoweka kwa sababu ya kufyatuliwa risasi  kwa pwani ya Alexandria wakati wa utawala wa Waingereza nchini Misri.Mnara huu una maghorofa matatu tuliyojua  kupitia michoro na picha za karne ya kumi na nane na kumi na tisa BK.Inajumuisha ghorofa la kwanza ambayo ina umbo la mraba, ikitazamana na dirisha  la kwanza ya ,mwadhimi  na juu yake ni ghorofa la  pili, ambayo ni dogo zaidi kuliko ya kwanza, na linatazama dirisha la pili la mwadhini, na ghorofa hilo la tatu lenye umbo la silinda juu yake kuna kuna mwenye pande nyingi.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy