" Ujumbe wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watembelea Kituo cha Tafiti za Kilimo "
Leo Alhamisi, Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na kuboresha Ardhi, zimeandaa ziara ya kutembelea Kituo cha kijimbo cha chakula na Malisho kinachohusiana na Kituo cha Tafiti kilichopo Wizara ya Kilimo, kwa Ushirikiano wa idadi ya wajumbe walioshiriki katika Udhamini wa Gamal Abd El Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa toleo lake la pili, chini ya kauli mbiu " Ushirikiano wa Kusini-Kusini " kwa ushirikiano na Chuo cha kitaifa cha Mafunzo, Wizara ya Mambo ya Nje na taasisi kadha za kitaifa,pamoja na Ufadhili wa Rais. Abd El Fatah El-Sisi, kwa ushirikiano wa viongozi wa vijana 100 kutoka nchi 50 kwenye mabara matatu (Afrika - Asia - Amerika ya Kusini ), mnamo kipindi cha 1 hadi 16 Juni.
Wajumbe hao wakati wa kufika kwao walikaribishwa na Prof. Dkt. Saad Moussa - Msimamizi Mkuu wa Mahusiano ya Kilimo cha Nje, Prof. Dk. Adel Abd El Azim, wakili wa Kituo cha Tafiti za Kilimo kwa Masuala ya miongozo, na Prof. Maher Al-Maghraby, Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mashamba ya Pamoja na Nchi za Afrika.
wakati wa ziara hiyo, ujumbe uliangalia shughuli muhimu zaidi za kituo , programu za kiutafiti na kimawasiliano pamoja na watafiti wa mabara matatu " Afrika , Asia na America ya Kusini. vilevile , ujumbe ulipata maelezo juu ya kituo cha tafiti na jukumu lake katika kuimarisha na kuendeleza kilimo nchini Misri ambapo wakati wa mkutano imeshatoa onesho la kufafanua shughuli za mradi wa mashamba ya pamoja ya kimisri, yaliyofanyika katika nchi za Afrika .
Kwa upande wake , Msimamizi wa Mahusiano ya Kilimo cha Nje Dkt.Saad Moussa alisema kwamba kilimo cha Misri kilishuhudia maendeleo yasiyo na kifani katika Kiwango cha kitaifa ndani ya Misri katika zama ya Rais Abd El Fatah El-Sisi, na Misri ilifanikiwa kuimarisha ushirikiano wa kilimo pamoja na nchi za Afrika na kurudi katika nafasi yake ya uongozi, haswa wakati wa uongozi wake kwa Umoja wa Afrika, ambapo Rais El-Sisi amebeba matatizo ya Afrika na kufanya juu chini ili kuyatatua Kwa hivyo, upanuzi wa mradi wa kuanzisha mashamba ya pamoja na nchi za Afrika ulikuwa mojawapo ya miradi ya maendeleo iliyofanikiwa kuchangia programu za Maendeleo Endelevu katika nchi za Afrika, pamoja na kuwasilisha ujuzi wa kilimo wa Misri kwa ndugu waafrika, ambapo mradi wa kuanzisha mashamba ya pamoja na nchi za Afrika umeendelea kwa njia inayoonekana katika hali halisi tangu miaka iliyopita pamoja na kutekeleza malengo muhimu ya mikakati yanayohusiana na kuongeza uzalishaji , kuwasilisha Teknolojia na kutumia tafiti za kisasa kupitia kujenga uwezo na kuendeleza maeneo ya logistiki ili kuimarisha uwekezaji.
wakili wa Kituo cha Tafiti za Kilimo Dkt.Adel Abd El Azim aligusia shughuli za kituo kupitia kufuatilia malisho yanayozalishwa ndani na kuagizwa kutoka nje , kuboresha na kufanya upya njia ya uchambuzi ili kuzuia udanganyifu, kudhibitisha kitaifa na kimataifa na kusaidia watafiti wa vyuo vikuu na vituo vya Tafiti katika shughuli zao za utafiti, kutekeleza programu za mafunzo kwa watafiti na mafundi katika nyanja za uchambuzi mbalimbali .
Mwishoni mwa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mashamba ya Pamoja na Nchi za Afrika Dkt. " Maher Al-Maghraby " alitoa onesho la kina lililosajiliwa kwa vituo na shughuli za Mradi wa Mashamba ya Pamoja ya kimisri, haswa yale yatakayoendelea kuanzishwa mnamo kipindi kijacho. pamoja na kujibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe, ambayo miongoni mwao ni athari za Covid 19 katika maendeleo ya kilimo, jinsi ya kugundua mbinu za kisasa kwa lengo la kuendeleza programu na shughuli za kilimo kwa ujumla.
Inatakiwa kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za nchi ya Misri baada ya uongozi wake wa Umoja wa Afrika wakati wa 2019 kutekeleza jukumu lake katika kuimarisha mchango wa vijana waafrika kwa kutoa aina zote za misaada, kujiwezesha na mafunzo pia.
pamoja na kuwawezesha katika vyeo vya uongozi na kufaidika kwa uwezo na mawazo yao. vilevile , huzingatiwa mojawapo ya njia ya kutekeleza Mtazamo wa Misri 2030 na Misingi kumi ya Shirika la Mshikamano Afro-Asia na Ajenda ya Afrika 2063, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ushirikiano wa Kusini- Kusini , Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu uwekezaji kwa vijana na Hati ya Vijana wa Afrika.