Ahmed Mokhtar.. Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Imefasiriwa na / Mervat Sakr
Elimu na uzoefu wa kazi
Shahada ya kwanza ya Sheria, Chuo Kikuu cha Ain Shams, kisha Uzamili wa Ujasiriamali.
Anafanya kazi katika Sekta ya Mahusiano ya Umma na Itifaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kairo, mhitimu wa Chama cha Kizazi cha Baadaye mnamo 2006 na mhusika wa kamati yake ya mawasiliano hadi 2010.
Mjumbe wa Kamati ya Kazi ya Asasi za Kiraia na Kujitolea ya Baraza la Taifa la Vijana mwaka 2010.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Maammaroun cha Maendeleo ya Jamii kutoka 2015 hadi kuhitimu, mpango wa Urais kwa watendaji wanaohitimu kwa uongozi, kundi la Al-Assar 2020, na mkuu wa klabu ya kijamii katika programu hiyo.
Mhitimu wa Chuo cha Kijeshi cha Nasser katika kozi zake zote 2021.
Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la pili 2021, Mkufunzi na mshauri wa mijadala, sera za umma na asasi za kiraia katika Baraza la Uingereza katika mipango ya Sauti ya Vijana wa Kiarabu, Sauti ya Vijana wa Mediterranean, wananchi wanaofanya kazi, mipango ya ujumuishaji wa kijinsia na watu wenye ulemavu wa mijadala na sera za umma katika Kituo cha Msaada wa Uamuzi na Uamuzi katika Baraza la Mawaziri.
• Mkufunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Taifa na programu nyingi katika usimamizi, uongozi, mawasiliano na maendeleo ya ujuzi, pamoja na mipango ya kijinsia kwa kushirikiana na Wanawake wa Umoja wa Mataifa.
Mkufunzi katika makampuni mengi ya ndani na ya kikanda na taasisi za kuendeleza ujuzi wa kibinafsi na kijamii katika mfumo wa kujenga amani, yasiyo ya vurugu, mawasiliano yasiyo ya vurugu, tofauti, mazungumzo, usimamizi wa migogoro na masuala ya kijinsia.