Kipindi cha tatu "Vyombo vya Habari vya Afrika-Asia vyakabiliana na Taarifa potovu: Changamoto na Masuluhisho"

Kipindi cha tatu cha programu ya Raia wa Ulimwengu mzima kinaangazia habari zisizo sahihi na changamoto kuu,  pamoja na  kutilia mkazo  zaidi njia za kukabiliana na Janga hili wakati wa COVID-19. 

Mkutano huo utawakaribisha watangazaji maarufu wa televisheni kutoka Afrika na Asia ili kubadilishana uzoefu, mambo wanayoyajali na mapendekezo yao .

 Mtangazaji maarufu wa Televisheni nchini Kenya Bi Shawn Osimbo anazungumzia changamoto zinazokabili vyombo vya habari Barani Afrika haswa  mnamo nyakati za majanga na mabadiliko. Na kutoka Asia, Bw. Jules Goyang ni Mtangazaji wa Mtandao wa Televisheni ya Watu wa Ufilipino (PTV) - kituo kikuu cha utangazaji kinachomilikiwa na Serikali ya Ufilipino - na mwanachama  wa Baraza la Ushauri la Vijana la Umoja wa Mataifa.  vilevile ,Bw. Jules,kiongozi  kijana na mjasiriamali,  atajadili nafasi ya vyombo vya habari katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Shawn alisema kwa kuwa ni   mwanamke , changamoto kubwa katika safari yake ya kazi ni  shaka za wanaume juu   ya uwezo wake kama mtangazaji wa televisheni ya michezo, basi  alijiwekeza  mwenyewe na alipata ujuzi ili kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa michezo. Pia alisisitiza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuzingatia ambacho wanakichapisha na kupata na kutafuta taarifa sahihi na kuzihakikishia kabla ya kuzitangaza kwa umma.

alihitimisha hotuba yake mwishoni mwa mkutano kuhusu ziara yake nchini Misri mwaka jana na alisifu upangaji wa Misri kwa  Kombe la Mataifa ya Afrika, akielezea furaha yake kubwa kwa ziara yake nchini Misri na kuhudhuria kwake Kombe la Mataifa ya Afrika.

 wakati ambapo huko Ufilipino na mataifa mengine Barani Asia, Jules alieleza kuwa kuwepo kwa uwakilishi sawasawa  kwa wanawake na wanaume katika kutoa  habari katika miaka michache iliyopita. Jules alielekea ujumbe kwa watazamaji wa kipindi hicho, akisema kwamba  tunapaswa kuwa na busara tunaposhughulikia habari kwenye mitandao ya kijamii, na tuhakikishe  ukweli wake   kabla ya kuzishiriki, kuzipenda au kuzitolea maoni kupitia kuchanguza  chanzo cha habari hizo.

Vipindi vya programu hiyo vinasimamiwa na Amira Sayed, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Misri, ambalo ni gazeti la kwanza la lugha ya Kiingereza katika Mashariki ya Kati, pamoja na kuwa mwakilishi wa Misri katika Bunge la Vijana la Kimataifa la Maji, na alishiriki katika kugusia matukio mengi ya kimataifa. ndani na nje ya Misri. 

inatajwa kwamba orodha ya wageni wa programu ya Raia wa Ulimwengu mzima   inajumuisha watungaji maamuzi na viongozi  vijana  kadha kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni na katika nyanja mbalimbali,  na hivyo kwa lengo la kufikisha ujumbe chanya kwa vijana Duniani ili kuunda kiunganishi kati ya vijana na watoa maamuzi.