Dkt. Amr Ramadan, Mhitimu wa kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Dkt. Amr Ramadan, Mhitimu wa kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa  Kimataifa

Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud


Mmisri mwaandajii wa programu, mjasiriamali, na mwanaharakati wa hali ya hewa, tena ni Mhitimu wa kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na mwenza wa Shirika la Fedha la Kimataifa katika Ushirikiano wa Vijana wa mwaka 2022.

Kwanza: uzoefu wa kisayansi

Alihitimu kutoka Kitivo cha Famasia, Chuo Kikuu cha Alexandria mnamo mwaka 2018.

Pili: Uzoefu wa kazi

- Wakati wa masomo yake, alishikilia cheo cha  Katibu wa Kamati ya Juu ya Vyombo vya Habari na Utamaduni katika Muungano wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Alexandria.

 - Ameteuliwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani  ili kushiriki katika Mpango wa Uongozi wa Wanafunzi kwa ajili ya kusoma  muhula  mnamo kipindi cha likizo  ya kiangazi wa 2016 katika Chuo Kikuu cha Bard huko New York.

- Alishiriki katika programu kadhaa za kubadilishana  uzoefu wa vijana zinazohusiana na Ajenda ya 2030 pamoja na Umoja wa Ulaya huko Ujerumani, Italia, Ufaransa, Uholanzi, Uhispania, Denmark, Jordan na Morocco.

- Aliwakilisha Misri katika ziara ya kimataifa inayohusiana kwa  Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza na Baraza la Uingereza pamoja na wawakilishi kutoka nchi 8  mnamo mwezi wa Februari 2017 ndani ya mpango wa "Raia  mwenye bidii".

 - Vilevile , alitoa hotuba nyingi kupitia jukwaa la TED, na yeye ni mhadhiri ambaye alitoa mihadhara kadhaa kuhusu ufadhili wa masomo, programu za kubadilishana utamaduni, programu za kubadilishana  uzoefu wa vijana, na programu za maendeleo endelevu katika vyuo vikuu vingi vya Misri.

Tatu: Kutunukiwa na Tuzo

- Hivi  karibuni , alitunukiwa katika kongamano la Amani wa Dunia huko Dubai, Falme za Kiarabu, kama kijana bora zaidi wa  kueneza Amani Duniani.

- Alitunukiwa  kwa jina la mwanafunzi bora zaidi katika kiwango cha Chuo Kikuu cha Alexandria  kwa mara mbili mnamo 2016 na 2018.
 

 Sasa hivi , Dkt. Amr ameanzisha kampuni  la   kutoa mafunzo na maendeleo ambalo husaidia vijana kujifunza kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu kupitia miradi kadhaa ya elimu kwa ushirikiano na mashirika ya ndani na ya kimataifa vilevile , hutoa programu za elimu zinazowawezesha vijana kujiandaa. kwa mitihani ya kimataifa, kukubaliwa katika udhamini wa masomo, programu za kubadilishana Utamaduni, na mipango ya Maendeleo Endelevu.