Afrika ndiyo ya kujiandikisha zaidi katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi na walemavu kwa 2.2% 

Afrika ndiyo ya kujiandikisha zaidi katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi na walemavu kwa 2.2% 

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi unaendelea kupokea waombaji wa udhamini huo kutoka Duniani kote hadi sasa, ambapo idadi ya waombaji mnamo wiki ya kwanza ilifikia watu 670.

Idadi ya wanaume walioomba Udhamini ilifikia 68.3%, huku idadi ya wanawake ikifikia 31.8%.

Bara la Afrika linawakilisha 88.8% ya waombaji, wakati Asia inawakilisha 1.6%, na Ulaya idadi sawa sawa, wakati Amerika ya Kusini inakuja na 1% ya jumla ya waombaji, pia kiasi cha watu Walemavu Kinawakilisha karibu 2.2% ya jumla ya waombaji wa Udhamini.

Hadi sasa Idadi ya waombaji wa Udhamini  wenye umri kati ya miaka 35 na 40 imefikia 11.6%, wakati wenye umri kati ya 25 na 30 imefikia 35%, waombaji wa Udhamini wenye umri kati ya miaka 16 na 25 imefikia 26.3%. Na wenye umri kati ya 30 na 35, imefikia 22.7%, wakati idadi ya waombaji wenye umri 40 hadi 45 ilifikia 2.6%, na inatarajiwa kuongeza idadi ya waombaji mnamo siku zijazo.

Ama kuhusu waombaji walio na Mafunzo ya Juu ilifikia 19.3%, wenye Shahada ya Uzamili walifikia 17.6%, na wenye Shahada ya Uzamivu  walifikia 8.2% ya jumla ya waombaji.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa; ni hatua ya kukamilisha juhudi za Misri kutekeleza jukumu lake lililokabidhiwa kuimarisha nafasi ya Vijana ndani, kikanda, bara na kimataifa, kupitia kutoa aina zote za misaada, Ukarabati na kutoa mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kufaidika kutoka kwa uwezo na mawazo yao.

Imepangwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa utaanza mnamo Mei 28 ijayo, na utaendelea kwa siku 15.