Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wafikia kwenye Mfereji wa Suez

Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wafikia kwenye Mfereji wa Suez

Luteni Jenerali Osama Rabie, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, alipokea, asubuhi ya siku ya 13 ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Dkt. Ashraf Sobhi, Waziri wa Vijana na Michezo, Nagwa Salah, Mkuu wa Idara kuu ya Maendeleo ya Vijana kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, Mamlaka ya Mfereji wa Suez, wanahabari na waandishi wa habari, wakifuatana na wajumbe wa vijana walioshiriki katika toleo la nne la Udhamini, baada ya kuwasili katika Kituo cha Uigaji na mafunzo ya baharini ya Mamlaka ya Mfereji wa Suez katika Mkoa wa Ismailia, katika mfumo wa ziara yao kwa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, inayolenga kujifunza kuhusu habari za hivi karibuni za miradi ya maendeleo katika eneo la Mfereji.

Kwa upande wake, Luteni Jenerali Osama Rabie, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, alimkaribisha Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhi na wajumbe wa vijana walioshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, akielezea furaha yake kwa uwepo huu wa kundi hili la nyota la makada wa vijana  viongozi wa mustakabali katika Mfereji wa Suez ndani ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na alisisitiza umuhimu wa kimkakati ambao mfereji unawakilisha kwa harakati za biashara ya kimataifa, ambalo liliufanya kuwa lengo kuu la Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na marudio ya miradi mikubwa ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez alitoa mada kuhusu Mfereji wa Suez iliyojumuisha simulizi ya historia yake, hatua mbalimbali za maendeleo yake, umuhimu wake kwa harakati za biashara ya kimataifa, mfumo wa urambazaji kwake, na kutoa mwanga juu ya faida za urambazaji zilizofikiwa na mradi mpya wa Mfereji wa Suez, hasa ongezeko la kipengele cha usalama wa urambazaji na uwezo wa mfereji kukabiliana na hali za Dharura zinazowezekana, pamoja na kuinua uainishaji wa mfereji kwa kuongeza uwezo wake wa nambari na wa kunyonya na kuongeza uwezo wake wa kupokea meli kubwa zenye rasimu kubwa, akionesha kwamba historia ya Mfereji wa Suez yaelezea mapambano ya watu wa Misri kwa miaka kumi katika kuuchimba hadi ufunguzi wake, akisisitiza kwamba mkondo wowote wa baharini hujenga maisha kwenye kingo zake, Wakati wa hotuba yake, Rabie alizungumzia kuchimba kwa Mfereji mpya wa Suez na mfumo wa urambazaji kwake, akielezea kuwa una urefu wa kilomita 72, kina cha mita 24, upana wa mita 400, na unaweza kubeba meli zenye rasimu ya futi 66, na kwamba dredgers 45 zilishiriki kama mradi mkubwa zaidi wa uchimbaji ulimwenguni kulingana na Elezo la Guinness kwa Rekodi.

Rabie alieleza kuwa wafanyakazi na maafisa 50,000 walishiriki katika mradi wa kuchimba Mfereji mpya wa Suez, na mradi huo ulitekelezwa kikamilifu kwa siku 354, kwa siku 11 kamili kabla ya muda uliopangwa, baada ya kukusanywa na kufadhiliwa kwa paundi bilioni 64 za Misri kwa siku nane tu akisifu watu wa Misri na jukumu lao katika kufadhili mradi huu mkubwa, kisha ikaoneshwa filamu iliyojumuisha sehemu za moja kwa moja za ununuzi wa raia wa vyeti vya Mfereji wa Suez na ushiriki wao katika kazi hii ya kitaifa kwa ajili ya nchi yao pendwa, Misri, na imani kwa kiongozi wao, Rais Abdel Fattah El-Sisi, pia Rabie alishughulikia taarifa kwa shughuli ya urambazaji katika Mfereji wa Suez mnamo miaka ya 2020 – 2021 – 2022 ambapo idadi ya meli ilipanda kutoka meli 18830 mnamo mwaka wa 2020 hadi meli 20694 mnamo mwaka wa 2021 kisha meli 23853 mnamo mwaka wa 2022 mizigo iliongezeka na marudio kwa dola mnamo miaka ile, pia ilipanda katika robo ya kwanza ya miezi kuanzia Januari hadi Machi ya mwaka huu wa 2023, Luteni Jenerali Rabie alisisitiza umakini wa Mfereji wa Suez kuboresha kiwango cha huduma za baharini na vifaa zinazotolewa kwa meli zinazovuka kwa kupitisha mkakati kamili wa maendeleo unaozingatia mambo manne makuu, yanajumuisha ukuzaji wa njia ya urambazaji ya mfereji na uboreshaji wa meli za baharini pamoja na kuongeza matumizi ya mali za mamlaka na vyanzo anuwai vya mapato.

Rabie  wakati wa hotuba yake alizungumza na washiriki kuhusu athari za janga la Corona kwenye minyororo ya usambazaji wa kimataifa, sera rahisi za uuzaji zilizotumiwa na Mamlaka ya Mfereji wa Suez wakati wa janga hilo, na majukumu yaliyotekelezwa na Mamlaka hadi walipofanikiwa kudumisha viwango vya usafirishaji wa meli licha ya athari za janga la Corona kwa uchumi wa ulimwengu ikilinganishwa na njia mbadala, ambapo mamlaka ilishughulikia wakati wa janga hili kwa njia ya haraka na unyumbufu kamili kwa kupitisha sera rahisi za uuzaji ili kuwazuia wateja kutoka kwa njia za usafirishaji na kuvutia wateja wapya, njia ambayo ilipata sifa nyingi za kimataifa kutoka kwa taasisi za kimataifa za meli, na akaongeza kuwa kulikuwa na ushirikiano katika kusafirisha mabaharia waliokwama kupitia milango miwili ya Mfereji wa Suez ya kusini na kaskazini, kisha washiriki walisikiliza mada kuhusu Utenzi wa kuelea meli ya kontena ya Panama na juhudi zilizofanywa na mamlaka katika muktadha huu, akionesha kwamba mzozo wa kukwama kwa meli kubwa ya Panama EVER GIVEN, ambayo ilidhihirisha kwa ulimwengu wote umuhimu wa Mfereji wa Suez, na imethibitisha bila shaka yoyote uwezo wa Wamisri kusimamia kituo hicho ya urambazaji, akisifu jukumu, ushujaa na uwezo wa waongozaji wa Misri, haswa wakati wa wimbi mbaya la hali ya hewa lililotokea mnamo Machi 2020, na aliwasilisha tuzo zilizopatikana na Mamlaka ya Mfereji wa Suez.

Kwa upande wake Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhi alimshukuru Luteni Jenerali Osama Rabie, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, kwa kuwakaribisha wajumbe wa vijana walioshiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kutembelea Kituo cha urambazaji muhimu zaidi Duniani Kituo cha bahari Duniani, akiashiria nafasi ya vijana wa bara la Afrika katika maendeleo, na juhudi za Wizara katika Utekelezaji wa matukio na shughuli kwa vijana wa Afrika. Sobhi aliongeza kuwa Misri imepata nafasi yake ya asili kimataifa na kikanda kutokana na juhudi kubwa na hatua madhubuti zinazoongozwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi, katika kutayarisha upya sera ya nje ya Misri, hasa katika ngazi ya Afrika, Waziri wa Vijana na Michezo alimshukuru Luteni Jenerali Osama Rabie kuhusu juhudi zenye matokeo mnamo kipindi kilichopita, akiwaambia wajumbe wa Udhamini wa Nasser wa Kimataifa: “Tulifungua madirisha yote kwa wajumbe nchini Misri kufikia malengo yao pamoja na  Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Kuchimbwa kwa mfereji mpya kwa mwaka mmoja na makada na mikono ya Misri ni kama muujiza.

Mkutano huo ulihitimishwa na Luteni Jenerali Osama Rabie, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, na Dkt. Ashraf Sobhi, Waziri wa Vijana na Michezo, pamoja na viongozi wa vijana walioshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, kwa kumkabidhi Luteni Jenerali Osama Rabie Ngao ya Mamlaka ya Mfereji wa Suez kwa Waziri wa Vijana na Michezo, pia Dkt. Ashraf Sobhi alitoa zawadi ya ukumbusho kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez.

Ziara ya viongozi  vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la nne, kwa Mfereji wa Suez ilijumuisha ukaguzi wa mahali pa vichuguu vya Ismailia ili kuona ukubwa wa mafanikio yaliyopatikana katika uwanja huo, ikifuatiwa na safari ya baharini katika Mfereji mpya wa Suez.

Kwa upande wao, washiriki walielezea furaha yao kubwa kwa kutembelea Mfereji wa Suez, kituo muhimu zaidi cha urambazaji Duniani ndani ya shughuli za Udhamini huo, wakisifu Mfereji Mpya wa Suez,  uliochimbwa kwa muda wa rekodi mnamo mwaka mmoja na makada na mikono ya Misri na walitakia mafanikio na ufanisi kwa juhudi za kuendeleza kituo hiki muhimu cha urambazaji, wakitoa shukurani zao kwa uungaji mkono kutoka kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi kwa mpango huu wa ukarimu, ambao ulimletea uzoefu na marafiki zaidi kutoka nchi mbalimbali za dunia, huku walichukua picha nyingi za ukumbusho na video zinazoonekana wakati wa ziara hiyo.

Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya ziara muhimu ambazo huandaliwa daima mnamo shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kutokana na umuhimu wake mkubwa katika kuwatambulisha washiriki wa udhamini huo kwa Kituo muhimu zaidi cha baharini duniani, na kwa ujasiri, nguvu, nia na dhamira ya Wamisri ambayo imejumuishwa tangu kuchimbwa kwa Mfereji kwa kwanza na katika mradi wa Mfereji Mpya wa Suez, pamoja na kukabiliana na migogoro yote na changamoto zinazoikabili mamlaka na kutoka nazo kwa manufaa na mafanikio ya kuvutia.

Ikumbukwe kwamba, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuwawezesha vijana, na kutoa fursa kwa watendaji kutoka nchi mbalimbali za Dunia kujumuika na kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu katika ngazi ya bara bali Duniani kote, na kati ya nchi za Kusini-Kusini, na kuimarisha hali ya kujitegemea katika nchi zinazoendelea kupitia kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo wao wa ubunifu ili kupata suluhu za matatizo yao ya maendeleo kulingana na matarajio yao, maadili yao na mahitaji yao maalum.