Wizara ya Vijana na Michezo yahitimisha shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika 

Wizara ya Vijana na Michezo yahitimisha shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika 
Wizara ya Vijana na Michezo yahitimisha shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika 

Wizara ya Vijana na Michezo, inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy,  ilihitimisha shughuli za Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo  (Ofisi ya vijana ya Afrika na Idara kuu kwa Ubunge na Elimu ya kiraia) ukiwa na Ufadhili wa Dokta. Mustafa Madbuli "Waziri Mkuu", mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi 22 Juni, 2019,kwa Ushirikiano wa Umoja wa Vijana waafrika, katika Kituo cha Elimu ya Uraia huko Algazira.

Baadhi ya Mabalozi wa nchi za Afrika kama Rwanda ,Congo, Zambia na Ethiopia pamoja na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika nchini Misri Balozi Abdelhamid Bozhair , Mwakilishi wa Umoja wa Vijana waafrika Bw.Munzer Al Maseref, Bi. Dina Fouad Mkuu wa Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia na Bw.Hassan Ghazaly Naibu wa Mkuu wa Umoja wa Afrika na Mwanzilishi wa  ofisi ya Vijana ya Afrika katika Wizara ya Vijana na Michezo na Maafisa kadhaa wa Wizara wote wamehudhuria  sherehe ya Kuhitimisha kwa Vijana wa Kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika.

Katika hotuba yake, Munzer Al Maseref  , Mwakilishi wa Umoja wa Vijana wa Afrika, alisisitizia umuhimu wa Udhamini wa Nasser kwa Vijana waafrika, unaochangia katika kurekebisha na kuendeleza vijana wa  nchi za Afrika ili kufikia malengo ya Umoja wa Afrika na kuunda na kuendelea  bara la Afrika, na akisifu mchango na juhudi za Uongozi wa Misri inayoongozwa na Abd El Fatah El-Sisi kwa kuimarisha vijana wa Afrika na kuchangia katika maendeleo ya watu wa nchi za Afrika kwa kuhamisha jaribio la Baba Waanzilishi wa Umoja wa Afrika haswa Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser.

Al Maseref   akaelezea mchango wa Misri na Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser katika kuimarisha bara la Afrika kwa kusaidia harakati za Ukombozi, kitu ambacho kimesaidia kuunganisha kwa nchi za Afrika katika enzi zote zilizopita, akisisitiza kubwa Vijana Waafrika wana jukumu la kuboresha na kuunda Bara la Afrika,pia kutekeleza Ajenda ya 2063 kwa ajili ya Maendeleo,Kufikia Utulivu, Uhuru,na Ustawi wa Bara la Afrika.

Al Maseref ameahidi kuwa Mawasiliano ya Vijana waafrika yataendelea pamoja na kukuza Ushirikiano kati ya Umoja na Vijana waafrika ili kuendeleza uwezo wao; wawe na uwezo wa kushikilia Uongozi wa Bara la Afrika.

Na kwa upande wake Balozi Abdelhamid Bozhair, Mkuu wa Ofisi ya  Umoja wa  Afrika nchini Misri akielezea furaha yake kubwa kwa kuhitimisha kikundi cha kwanza cha Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo  (Ofisi ya Vijana ya Afrika na Idara kuu kwa Ubunge na Elimu ya kiraia) kwa Ufadhili wa Dkt.  Mostafa Madbouly Waziri Mkuu vilevile akiashiria kwamba Udhamini huo  unasaidia kuhifadhi makumbusho ya kisiasa na yenye Ustaarabu kwa waafrika wote ambayo ni makumbusho ya Kiongozi Marehemu Gamal Abd El  Nasser aliyeanzisha Umoja wa Afrika.

Pia Balozi akisifu maudhui ya Udhamini  iliyochuguliwa na Wizara ya Vijana na Michezo kwa mujibu wa imani ya Uongozi wa Misri kwamba inapaswa kuhamisha Jaribio la Gamal Abd El Nasser la shughuli ya kiraia na mtazamo wa kimkakati na kisiasa kwa vijana wa Afrika ili kupata maanufa kutoka historia yake katika harakati za ukombozi  na kukaza maana halisi ya Uhuru na Utulivu pamoja na kuzingatia mchango wa  Baba Waanzilishi wa kwanza wa Umoja ya Afrika  na amesisitizia umuhimu wa kueneza maarifa ya kisiasa na dhana ya Uhuru na kutoa hamu kwa elimu na kuwezesha kwa Vijana  pamoja na kukuza juhudi na ushirikiano kati ya nchi za Afrika ili kujenga uwezo wa Vijana kama  mustakbali ya Bara la Afrika na watakaotekeleza Ajenda ya 2063 na kuongoza Afrika.

Katika muktadha huo huo Profesa El Sayed Flifl, Mkuu wa kamati ya mambo ya Afrika katika Bunge na Mkuu wa zamani sana wa Kitivo cha Mafunzo ya juu ya kiafrika amesisitiza kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika umesaidia kuhamisha jaribio la Misri kwa nchi za kiafrika ili kufikia Maendeleo na Ajenda ya 2063 na ameomba Vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo kutoa ujumbe wa upendo kwa nchi zao kutoka kwa Umoja wa Afrika,ukiwa ni Taasisi kuu inayojumuisha Waafrika, pia nyumba ambayo pande zake huundwa na Watu wa Afrika.

Kwa upande wake, Dina Fuad, Mkuu wa Idara Kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia, alisisitiza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika "uliokuwa na Viongozi Vijana 100  wakiwakilisha nchi 25 za Afrika" ni miongoni mwa mfululizo wa mipango na matukio yaliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo, inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, ili kuimarisha shughuli za vijana waafrika kupitia kutoa misaada ya kila aina, uwezeshaji na mafunzo pamoja na kuwawezesha nafasi za kuongoza na kupata manufaa kutoka uwezo wao na mawazo yao kwa mujibu wa yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri katika Shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani.

Hassan Ghazaly Naibu wa Mkuu wa Umoja wa Afrika na Mwanzilishi wa Ofisi ya Vijana ya Afrika amesisitiza kwamba Udhamini wa Nasser unazingatiwa kama njia muhimu moja ya kubadilisha kwa Afrika katika Ajenda ya 2063 na njia moja ya kutekeleza (million by 2021) ya kuwawezesha Vijana waafrika Milioni, ifikiapo 2021 ambayo imeanzishwa kwa Kamishna ya Sayansi, Teknolojia na Rasiliamali za Watu katika Umoja wa Afrika, akielezea malengo yake ambayo ni pamoja na kutoa jaribio kale ya  Misri katika kujenga taasisi za kitaifa na kuunda kizazi kipya kinaweza kuongoza bara la Afrika wenye mitazamo yanafanana na Maelekezo ya Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika yenye imani kuhudumia malengo ya Umoja wa Afrika kwa ukamilifu,pamoja na kujenga mikusanyiko kwa viongozi wa Afrika wa vijana wenye athari zaidi Barani kwa mazoezi, Ujuzi unaotakiwa pia mitazamo ya kimkakati.

Wakati wa hitimisho hilo  Aya chebii  "alishiriki kupitia Video yenye ujumbe wa upendo kwa vijana wa Afrika waliojiunga katika shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika" akiashiria mchango wa Misri na Wizara ya Vijana na Michezo katika kuelimisha na kuzoeza Vijana wa Afrika kwa kuongoza Afrika na kujenga Bara pia kuliendeleza, kisha  kipindi cha Ushairi chenye cha "Sisi" kimetolewa na mmoja wa washiriki kutoka Uganda na wakati wa kuimba unaoakisi roho ya Afrika kwa washiriki kadhaa wakiongozwa na Ahmed Omar Mwanachama wa Bendi ya wist Elbild, na  Hafla hiyo ilihitimishwa kwa kuwaheshimu washiriki na kukabidhi vyeti kwa kikundi cha kwanza cha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika.