Sébastien Haller Afufuliwa upya

Sébastien Haller Afufuliwa upya

Imeandikwa na/ Ahmed Magdy

_Mshambuliaji wa timu ya Borussia Dortmund ya kiujerumani, na timu ya kitaifa ya Cote dìvoire, alipatwa na saratani ya korodani mnamo mwaka 2022, kwa hivyo ameacha kufanya mazoezi na kucheza soka kwa ujumla, pamoja na kufanya upasuaji kadhaa na kupata tibakemikali, mwanzoni mwa mwaka wa 2023, mchezaji huyo aliweza kuishinda saratani ambapo ugonjwa huo haumzuii kukamilisha safari yake na Dortmund na kuwa nyota wa timu. 
_ Halafu Shirika la Reuters liliangazia kauli za mchezaji wa timu ya kitaifa ya Ndovu kama inavyojulikana ambapo alisema: “ mwaka wa 2022 haujawa rahisi lakini uliniwezesha kuzikabili changamoto mpya za mwaka wa 2023 “
_  sasa wasomaji wangu wapendwa tulifikia hatua muhimu sana katika historia ya mchezaji huyo ambapo aliongoza timu yake ya kitaifa kuelekea ushindi katika finali ya Kombe la Mataifa ya Afrika la Afcon, ambapo alifunga bao la ushindi ili wapate mtaji wa nne wa michuano hiyo. 

_  kwa hiyo hebu tuangalie kwa ukaribu zaidi baadhi ya maelezo kuhusu  mshambuliaji huyo: 
_ kwa jina anaitwa Sébastien Romain Teddy Haller, amezaliwa tarehe 22 mwezi wa Juni mwaka 1994, huko Ris-Orangis Ufaransa, Mamake alitoka Core dìvoire, na baba yake alikuwa Mfaransa, na pia hakukua peke yake na wazazi wake tu ambapo alikuwa na kaka yake anayeitwa Sery Tessia, na dada yake Armelle, na alipokuwa na umri wa miaka 3 wazazi wake waliona upendo wake kwa michezo, ambapo alipokuwa na miaka 10 alianza safari yake ya kucheza mpira wa miguu na timu ya F.C.O Vigneux, iliyoshinda taji lake la kwanza baada ya kujiunga kwa Haller, Baada ya miaka miwili ya kucheza na FCO Vigneux, Haller  alihamia kwenye akademia kubwa inayoitwa Bretigny Foot, Bretigny Foot ilimfanya kuwa maarufu, na ilikuwa wakati huu alianza kujiona kama nyota wa baadaye, na mnamo mwaka wa 2007 akajiunga na taasisi ya vijana wa Auxerre, Baada ya miaka mitatu ya kucheza soka la kulipwa, Haller aliamua kuhama Ufaransa, wakati huu na kwenda Uholanzi, Kutafuta mafanikio kulimfanya ajiunge na FC Utrecht ya Uholanzi kwa mkopo kabla ya kufunga mkataba wa kudumu.
_ Akiwa na umri wa miaka 22, Haller alijiunga na Eintracht Frankfurt, na Mnamo 2020  AFC Ajax ilinunua talanta ya Haller, na sasa anachezea huko Ujerumani na Borussia Dortmund.

_  jamani nadhani tunaweza kupata mafunzo mazuri kutoka kwa hadithi hiyo ya Haller, aliyepambana na saratani hadi kuishinda na kusaidia timu yake ya taifa katika kushinda kombe la Afcon, kwa hivyo mkiwa na mambo magumu maishani mwenu msikate tamaa na endeleeni kupiga hatua na kusonga mbele ambapo hiyo ndio ni sifa ya mabingwa.