Maadhimisho ya Uhuru wa Libya

Imetafsiriwa na/ Malak Hazem
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Leo, Desemba 24, inaadhimisha Siku ya Uhuru wa Libya, baada ya mfululizo wa vita vya kishujaa vilivyofanywa na watu wa Libya ili kukomboa ardhi kutoka kwa mkoloni wa Italia, na kufuatia tangazo la uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa Libya, Katiba ya Libya ilitangazwa mnamo tarehe Desemba 24, 1951, na Muhammad Idris Al-Senussi alichaguliwa kuwa Mfalme wa Ufalme wa Libya na mfumo wa shirikisho unaojumuisha majimbo matatu (Tripolitania, Cyrenaica, Fezzan).
Katika siku hii, Mfalme Senussi alitangaza kutoka kwenye ukumbi wa Al-Manar Palace katika mji wa Benghazi, kwa watu wa Libya na ulimwengu wote kwamba Libya imekuwa nchi huru na yenye kujitegemea.
Mahusiano ya Misri na Libya yana sifa ya kipekee, kwani usalama wa taifa wa nchi hizo mbili ni sehemu muhimu, pamoja na mipaka ya kawaida, mahusiano ya karibu ya kihistoria na maslahi ya juu ya kitaifa kati ya nchi hizo mbili.
Misri ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza zilizoshughulikia Libya rasmi baada ya uhuru wake katika miaka ya hamsini ya karne ya ishirini, na mapinduzi ya Libya yaliathiriwa mwanzoni mwa mwaka 1969 na Mapinduzi ya Julai, na Libya ilitafuta umoja na serikali ya Misri kwa kusaini Mkataba wa Tripoli mnamo tarehe Desemba 1969 na wakati Rais Abdel Nasser alipowasili Tripoli mnamo tarehe Desemba 25, 1969 katika ziara yake ya kwanza baada ya mapinduzi ya Libya, alipokelewa kwa furaha na umati mkubwa wa watu wa Libya wanaopenda.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy