" Udhamini wa Nasser wa Uongozi " katika ziara yake kwa Ngome ya Salah al-Din
Vijana waafrika wanaoshiriki katika " Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kiafrika " walitembelea Piramidi na Sphinx, wakati ambapo walitazama eneo la Panorama ili kutambua zaidi kuhusu Ustaarabu wa kale wa Mafarao.
Hayo yalitokea wakati wa shughuli za siku ya kumi na mbili ya Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kiafrika ", uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo, "Ofisi ya Vijana wa Afrika na idara kuu ya Bunge na Elimu ya Uraia" kwa Ufadhili wa Dk. Mustafa Madbouly. , Waziri Mkuu, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni, kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana wa Afrika.
Bw. Naji Hanafi, Mkurugenzi Mkuu wa Ngome hiyo aliwasindikiza katika ziara hiyo , na walitembelea Misikiti ya Muhammad Ali, na Al-Nasir Muhammad, Panorama ya Ngome hiyo, na Makumbusho ya Polisi,pia waliangalia Onesho maalum la Cultrama ya Ngome,ambapo linatoa historia ya Ustaarabu wa Misri tangu zama za kale hadi nyakati za kisasa.
Mkuu wa Sekta ya Mambo ya Kale ya Kiislamu, Kikoptiki na Kiyahudi Dkt.Gamal Mustafa alisema wageni hao walielezea kushangazwa kwao kwa maonyesho hayo, wakisisitiza Ukale,Utofauti na Upekee wa ustaarabu wa Misri, pia eneo la kipekee la Misri linaifanya kuwa mkusanyiko kwa Waafrika wote .
Wageni walitilia maanani ili kuchukua picha nyingi za kumbukumbu ili kusajili ziara yao kwenye ngome hiyo, na pia walitoa Shukrani zao kwa Serikali ya Misri kwa ukarimu na ushirikiano wake.