Wizara ya Vijana na Michezo yajiandaa kuzindua toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Wizara ya Vijana na Michezo yajiandaa kuzindua toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Dokta Ashraf Sobhy:
Ushirikiano wa Kusini - Kusini na Vijana wa Harakati ya Kutopendelea ni Kaulimbiu ya Toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.
Kutegemea Historia kunaweza kutusaidia kupata Masuluhisho kwa Shida za kisasa.
Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, inajiandaa kuzindua toleo la tatu la Udhamini wa Kiongozi Gamal Abd El Nasser, unaopangwa kufanyika mnamo Juni ijayo, ukiwa na kichwa cha "Ushirikiano wa Kusini - Kusini na Vijana wa Harakati ya Kutopendelea"
Toleo hilo linategemea kikubwa majadiliano kati ya washiriki, kujua Zaidi kuhusu Maadili ya Harakati ya Kutopendelea, athari zake Duniani kote, pia kuainisha misingi ya jukumu la vijana wa Harakati ya Kutopendelea , na kuunda dhana mpya inayoendana sawa saw ana vyanzo vya zama yetu, linaloiwezesha kuwakilisha kiwango cha chini cha masilahi za kisiasa na kiuchumi nchini mwake, pamoja na kufikia jukumu lake lililokabidhiwa kwa Ushiriki kuelekea Ushirikiano wa Kusini-Kusini, kulingana na Uadilifu, Amani na Usalama Duniani, na kuzima athari za Uovu, Ghasia na Vita Duniani.
kutoka upande wake, Waziri huyo Dkt. Ashraf Sobhy, alisisitizia mnamo kipindi cha kisasa umuhimu wa jukumu la vijana wa Dunia la kufufua tena maadili ya Kutopendelea kama nguvu laini na ya kidiplomasia yenye uwezo wa kupambana na vita baridi na kuimarisha Nguzo za Amani na Usalama Duniani, akiashiria kuwa kutegemea Historia kunaweza kutusaidia kupata Masuluhisho ya Shida za kisasa.Na ni muhimu sana kufanya upya kwa Harakati ya Kutopendelea ya kisasa na ianze tena kutoka Misri.
Timu ya kazi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa iliona kuwa wakati wa kihistoria unatulazimisha kutoa nafasi kwa ajili ya kile kinachoweza kutolewa kutoka kwa "Harakati ya Kutopendelea" na Mpango wake wa kihistoria uliozinduliwa na viongozi wa Dunia hapo awali, ambapo ulianzishwa 1955, baada ya Mkutano wa Bandung, na kiini chake kilikuwa nchi 29 zilizohudhuria mkutano huo, pia Harakati hiyo iliundwa kutokana na vita baridi iliyozuka kati ya Nchi mbili kubwa wakati huo nazo ni : NATO ikiongozwa na Marekani, na Warso ikiongozwa na Umoja wa Kisovieti, na hivyo kwa ajili ya kuzuia sera zilizosababisha vita hivyo. Na kweli Harakati hiyo ilikuwa na nafasi kubwa katika kudumisha Amani na Usalama na kushinda Ukoloni, na si hivyo tu bali kuibuka mataifa mapya yanajitegemea. na mnamo kipindi zaidi ya miaka 50, idadi ya nchi wanachama wa Harakati ya Kutopendelea ifikapo zaidi ya nchi 116.