Haile Selassie
"Mkutano huu hakuwezi kumalizika bila kupitishwa kwa Itifaki moja ya Afrika ...na hatuwezi kuondoka bila kuanzisha Shirika moja la kiafrika... tukishindwa, tutakuwa tumeacha wajibu wetu Kuelekea Afrika na Watu wake...lakini tukishinda hapa, tu, tutakuwa tumehalalisha uwepo wetu".
(Hotuba ya mtawala Haile Selassie, kwenye mkutano wa Addis Ababa, Mei 1962).
"Ras Tafari Makonnen" anayejulikana kama "Haile Selassie", inamaanisha nguvu ya pande tatu : Baba, Mwana, na Roho takatifu, yeye ndiye mfalme wa mwisho wa Ethiopia, alizaliwa mnamo Julai 23 1892, mjini mwa "Argentina Guru"-Ufalme wa Ethiopia- mkoa wa Harar, amefariki Dunia mnamo Julai 27 1975, kutoka kwa familia safi ya Orthdox na nasaba ya kifalme ya kale_ ambapo baba yake alikuwa mshauri mkuu wa mfalme "Menelik ll", mbali na uhusiano wake wa kindani na familia inayotawala kupitia babu yake mzaa mama, na huyu ndiye baba wa wasichana wanne na wavulana wawili, alisifiwa kama mwenye akili, kidiplomasia na mtukufu, ana Lakabu nyingine nyingi kama {Yuda Mteule wa Mungu, Mfalme wa Ethiopia} {Simba Muweza wa Kabila} {Mfalme mkuu wa Ethiopia}.
Alishikilia vyeo kadhaa, alifanya kama Kiongozi wa Jimbo la (Sidamo, Ethiopia) 1907, Kiongozi wa Jimbo(Harar) hadi 1909, alitawazwa kama mfalme wa Ethiopia 1928, kisha mtawala wake 1930.
Alichukua jukumu kubwa katika kujihusisha Ethiopia kwenye Mkusanyiko wa Mataifa 1923, kisha Umoja wa Mataifa 1948.
Haile Selassie ni mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika- Umoja wa Afrika sasa- iliyoanzishwa mwaka mmoja baada ya mapendekezo ya mkutano wa Addis Ababa Mei 1962, na aliyoizungumzia Hotuba yake maarufu, na Addis Ababa ilichaguliwa kama kituo cha Umoja wa Afrika mnamo 1963 wakati wa kusainiwa kwa hati ya Uanzilishi wake.
Ikumbukwe kwamba utawala wake ulidumu kwa karibu na nusu karne, ulishuhudia matukio mengi ikiwa ni pamoja na: Shambulio la Mussolini kwa Ethiopia mnamo Oktoba 1935, pia alishuhudia Vita vikuu vya Pili Duniani na Ukombozi wa Ethiopia1941, -inafaa kutaja hapa Hotuba yake maarufu ya kihistoria katika Mkusanyiko wa Mataifa, ambayo baadaye ikawa moja ya icons muhimu zaidi za kupinga Ufashisti- pia alishiriki katika mikutano mingi ya kiafrika ikiwa ni pamoja na: mkutano wa(Monrovia Nchini Liberia) 1961, uliokuwa ukitoa wito wa Umoja na Usharikiano kati ya nchi za Afrika, na (mkutano wa Lagos) 1962 na mikutano mingine.
Haile Selassie alijulikana kwa hamu yake kubwa ya elimu, Dalili bora ya hivyo ni mchango wake wa moja ya majumba yake matatu kugeuzwa liwe Chuo Kikuu. Pia alikuwa na ziara nyingi Duniani kote, mnamo1924 alizunguka Duniani pamoja na Magavana wa Majimbo ya Ethiopia, alitembelea Misri na ElQuds(Yerusalemu), na nchi kadhaa za Ulaya kama Paris, Amsterdam, Geneva, Athena na Brussels.
Jana, Rais wa Misri"Abd El-Fatah El-Sisi" alishiriki pamoja na Viongozi wa Afrika kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia katika kuonyesha Marehemu mfalme wa Ethiopia" Haile Selassie", na mnamo 1968 Marehemu Rais"Gamal Abd El Nasser" na mfalme wa Ethiopia walishirikiana katika uzinduzi wa Kanisa Kuu la Mark, si hivyo tu, lakini Misri wakati huo iliweka jiwe la kimsingi la kanisa mnamo 1965, na ilitoa Paundi 150.000 za Misri kama mchango katika ujenzi huo.
Na mnamo 1973 katika zama ya Rais Marehemu "Anwr El Sadat" Misri ilishuhudia ziara ya mfalme wa Ethiopia na Rais mwenyewe akampokea wakati huo katika sherehe kubwa, inayothibitisha ukweli wa miaka 88 ya mizizi ya mahusiano ya Misri na Ethiopia.