Muungano wa Wanafunzi wa Afrika

Muungano wa Wanafunzi wa Afrika

Imefasiriwa na / Aya Nabil

Muungano huu ni  Shirika linalojumuisha wanafunzi wote wa Afrika tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972, na hadi wakati huu una uwepo katika nchi 54 Barani Afrika, kama mkusanyiko mkubwa zaidi wa wanafunzi Barani humo, na Muungano huo ulikuwa na jukumu muhimu sana na wa ushawishi katika mapambano dhidi ya ukoloni na kukomesha ubaguzi wa rangi wakati wa harakati za uhuru wa kitaifa wa Afrika, na mnamo mwaka wa 2000, Muungano huo ulipewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa, kwa kutambua juhudi na mchango wake katika kuendeleza haki za wanafunzi na kutetea haki zao, na kazi yake ya kuleta demokrasia kwa elimu katika bara la Afrika.

Muundo wa kiutendaji wa Umoja huo unawakilisha  maeneo yote madogo katika nchi mbalimbali za Afrika, hufanya kazi kwa njia huru, uwakilishi, kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kufanya kazi kulingana na misingi ya kidemokrasia, pamoja na  kuanzisha ofisi zisizo za kikanda ili kuhakikisha Nguzo za Usimamizi na kukamilisha juhudi za makao makuu huko Accra-Ghana.

Ambapo nguvu kuu ya Muungano huo iko katika utofauti wake na nguvu yake ya kiidadi ambayo hutumiwa kama chombo cha kujadili na kuzungumza kuhusu maslahi ya juu ya wanafunzi wakati wote, pamoja na kwamba Muungano huo huzingatia  pia utamaduni mbalimbali  na utofauti wa kiutamaduni wa wanafunzi bila kujali dini yao, jinsia yao, asili yao ya kiutamaduni, imani zao za kisiasa, asili yao ya kikabila au hali yao ya kijamii.

Sasa Muungano huo unafanya kazi ya kuhakikisha lengo lake la kimsingi kupitia kujenga uwezo, kuunganisha, na ushirikiano, pamoja na kufanya kazi ili kuhakikisha usawa katika kupata elimu bora, uhakikisho wa ubora wa elimu ya juu, kuunganisha  na mifumo yake, na kuifanya ipatikane kwa wote kwa kuzingatia kimsingi uhuru wa kubadilishana wasomi, pamoja na Kukuza dhana ya utawala wa kidemokrasia, kutetea haki za wanafunzi, kuimarisha jinsia na utamaduni wa kiafrika, maendeleo endelevu, ujasiriamali, na kuunganisha maadili ya amani, haki na demokrasia.