Utaratibu wa Kiafrika wa kutathmini Rika (APRM)

Utaratibu wa Kiafrika wa kutathmini Rika (APRM)

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

"Kuelekea Kuimarisha Demokrasia, Utawala Bora na Udhibiti" 

Mnamo Machi 9, 2003, miaka 20 iliyopita, Utaratibu wa Kiafrika wa Kutathmini Rika (APRM) ulianzishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD huko Abuja, Nigeria, na leo, karibu miongo miwili baadaye, APRM imeenea kwa mikoa yote ya AU, inayojumuisha nchi 42 kati ya 55 wanachama wa AU katika Jumuiya ya Utaratibu huo, na Burundi ya hivi karibuni kujiunga. 

Mnamo miaka hiyo, Utaratibu ulikamilisha mapitio ya kitaifa katika nchi 24 wanachama, pamoja na mapitio ya rika ya kizazi cha pili katika nchi tano wanachama, na mapitio manne ya rika katika nchi tatu wanachama. 

Kazi ya Utaratibu wa Kiafrika wa kutathmini Rika  imesababisha utajiri wa taarifa kwa kuzingatia ushiriki mpana wa wadau na imeonesha kuwa mchango mkubwa wa Kiafrika katika uanzishwaji na uanzishwaji wa misingi inayozingatia misingi ya Afrika ya utawala bora, kwa kuzingatia uongozi shirikishi na uraia bora.

Wimbi la mapinduzi na mabadiliko yasiyo ya kikatiba ya Serikali bara letu liliyoshuhudia yameonesha zaidi kuliko hapo awali haja ya kuendelea kwa utawala bora kwa kuzingatia misingi ya Utaratibu wa kiafrika wa kutathmini Rika wa utawala bora katika ngazi za kisiasa, kiuchumi, kijamii na ushirika, demokrasia, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na utatuzi wa migogoro kwa njia ya Amani. 

Maoni ya Utaratibu wa kiafrika wa kutathmini Rika (APRM) yaliyojumuishwa katika Mpango Mkakati wa APRM (2020-2024), ni "Afrika inaongozwa vizuri kwa Afrika tunayoitaka" na Jumuiya ya APRM inakuza maoni haya pamoja na kanuni zake kupitia michakato yake ya msingi ya mapitio, inayotegemea Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala Bora, na programu za shughuli za kitaifa hutoa muhtasari wa mapendekezo yanayotokana na mapitio ya APRM yanayoendana na mifumo ya kimkakati na mipango ya kitaifa ya utekelezaji wa muda wa kati.

Pamoja na kazi ya Utaratibu wa kiafrika wa kutathmini Rika, maadili, kanuni na mapendekezo haya yanaimarisha demokrasia yetu na utaratibu wa kikatiba na yanahitaji matengenezo endelevu, msaada na juhudi kwa upande wa makundi 15 ya Umoja wa Afrika, iwe katika ngazi za chini, kitaifa au bara. 


Bila shaka, Ghasia, mapinduzi na mizozo Barani Afrika imekita mizizi na kuchochewa zaidi na uzembe katika utawala, na ni tishio la kufikia Afrika iliyo salama, iliyounganishwa, iliyoendelea, na yenye mafanikio, na ukuzaji wa demokrasia na utawala bora ndani ya mfumo wa Utaratibu wa kiafrika wa kutathmini Rika kwa kuzingatia sababu kuu za migogoro, Kulingana na kile kilichoelezwa katika ripoti za Mapitio ya Kitaifa ya Utaratibu wa Utawala wa Kidemokrasia,  unaojumuisha chanzo muhimu cha kuunga mkono Mpango wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika na kurejesha Udhibiti na utawala wa sheria.