Mji wa Ras Sidr
Mji wa Ras Sidr uko katika upande wa mashariki kwa ghuba ya Suez . katika kaskazini na kusini mwa eneo la Oyoun Musa, na eneo hilo ni mahali mbalimbali pa kiutalii kwa utalii wa mazingira(Alcotorizm)na huko unaweza kufanya mazoezi ya Tanga, kuogelea, kupiga mbizi na safari au mapumziko ya afya na kujua mahali pa kihistoria na kiutamaduni.
Mji huo ni wa kwanza katika Sinai kusini kutoka upande wa mashariki, na uko mbali na mfereji wa Suez karibu na kilomita 60 .mji wa Ras Sidr uko katika ghuba ya Suez, na una ukubwa wa kilomita 6750 za mraba, na kuna katika mji ule mabonde mengi yenye rutuba kama bonde la Sidr.
Inawezekana kufikia eneo la Ras Sidr kwa bahari,ardhi na hewa,ambapo kwamba mji huo uko mbali na mji wa Kairo kilomita 200 kwa ardhi kupitia handaki ya shahidi Ahmed Hamdy na kwa bahari kupitia bandari za Suez kama Al-Adabiya, Al-Arish na Al-Tor. Uwanja wa ndege wa kimataifa tayari umeanzishwa katika eneo hili, na hapo kuna viwanja vitatu vya ndege vya kimataifa vinasaidia eneo la Ras Sidr,navyo ni Kairo, Al-Arish na Sharm El-Sheikh.
Mji wa Ras Sidr una maeneo mbalimbali ya kiutalii kama fukwe zake nzuri kwa urefu wa kilomita 95 na hewa yake nzuri hadi milima ya Serpal au mlima wa farao unaotoa nafasi kwa wapenzi wa kutazama ndege, na pale kuna mbuzi wa mlima na ngamia wanaoweza kutembea katika milima na mabonde.
Na kutoka mambo muhimu zaidi ya eneo la kiutalii ni mapumziko yake ya afya ya kikibriti yaliyogunduliwa na Mafarao tangu miaka 5000 na mapumziko yale ni vyoo na macho ya kawaida ya kibiriti yalifika joto lake hadi 75. Kuna pia mabonde yanayovutia wapenzi wa safari za jangwa na kuwinda kama bonde la Al-Gherendel, la Tiba na bonde la Taraki,na mabonde yale yalijazwa, na mimea, miti ya ajabu na ndege za kware. Mji wa Ras Sidr una vikundi vitatu vya wabedui ni Oyoun Musa ,bonde la Gherendel na Abu Essaouira, na huko kuweza kujua mahusika ya kikabila na sanaa za kibedui kama kazi za mikono zilizopambwa na turquoise ya Sinai, nguo zilizoshonwa na sanaa za muziki za bedui.
Mji wa Sinai ukizingatiwa mkutano wa tamaduni, ustaarabu wa kale na ujumbe wa mbinguni tangu enzi ya Mafarao, nabii Musa, Mkiristo, wagiriki na warumi, na kutoka mahali mazuri hapo ni Oyoun Musa, choo cha farao na bonde la maktab.
Vijiji vya kiutalii vilizidi katika mji wa Sinai katika miaka ya mwisho ili kufurahia fukwe zake nzuri katika maji ya ghuba ya Suez,na hewa yake nzuri mnamo mwaka mzima,pamoja na utalii wa burudani katika fukwe za Ras Sidr ,ambapo kuna baadhi ya mahali pa kihistoria ndani yake kama:
Maandishi ya pango:
Maandishi ya pango yalikuwa makale zaidi kuliko maeneo ya utalii wa kitamaduni yote katika Sinai, na maandishi haya yanazingatia kujali kwa wamisri kwa madini na kutuma safari hadi maeneo haya katika bonde la Sidr katika mashariki ya ghuba ya Suez, lakini baadhi ya maandishi ya pango yaliharibika. Jina la pango linaitwa sehemu ya bonde la Qunia,ambapo kuna hapo mlima ambao una turquoise ambayo zilitokwa na wamisri wakale, na bado kuna katika eneo hili mabaki ya mapango ya wafanyakazi kwenye moja ya majengo yenye urefu, inawezekana kufuatilia kuta zake lakini maandishi muhimu yaliyokuwepo hapo, hayakuwepo tena, ambapo kutuma baadhi ya maandishi haya hadi makumbusho ya Misri mjini Kairo au yaliharibika katika majaribu ya kutafutia turquoise katika mwanzo wa Karne ya kisasa.
Ngome wa Al-Gondi:
Ngome hii iko katika mlima wa kichwa cha Al-Gondi iliofika hadi urefu wa futi 2150 juu ya bahari, na uliongezeka futi 500 juu ya mto mpana juu ya pande zote, na mlima huu una sura ajabu na mahali pazuri pa sura ya kawaida unaweza kuuona kwa macho yake kutoka kilomita mbali, na anayesimama juu yake anagundua mbali zaidi kutoka umbali huu. Kujenga ngome hii kunahusisha na matokeo ya kihistoria ambapo Salah El-Din na ndugu yake mfalme Al-Adel wameanza kujenga ngome hii katika mwaka 1183, na wamemaliza katika 1187.
Utaratibu wa Ngome :
Ngome ya Salah Al-Din iko juu ya mlima wa El-Gondi, na ngome hii ina sura ya mstatili ilielekea katika pande mbili kaskazini kwa mashariki na kusini kwa magharibi, na upande wa kusini ulimaliza kwa sura ya bunduki, mkono wa mgome ni Kati ya mita 150 hadi 200 kama urefu na upana wake ni mia mita na ukuta nje wa ngome ni mita mbili, lakini pande zake zilijengwa na nguzo ngumu. Ngome hii inajumisha ndani yake vyumba vidogo kwa wanajeshi, na kujenga majengo mengi kwa vitu mbalimbali kama shimo la upana( mita 50-60 ) kina chake ni mita tano chini ya ardhi na lilikuwa kama duka la vyakula, na pia msikiti bila paa, na ukuta wake wa mashariki una kibla kina uaandishi maridadi wa Basmala na paa ya msikiti ni mita 6-12, kuna pia bomba la maji lilichorwa katika mlima ambapo kuna ndani yake tanki ya vipimo vya mita 5,5-6-10, na bado kuta zake ni nzuri na ina mashimo mawili kwa kuingia na kutoka maji.