Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kimageuzi" unaangaliwa na nchi

Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kimageuzi" unaangaliwa na nchi
Wizara ya vijana na michezo kwa Uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy inasisitiza juu ya umuhimu na usaidizi wa nchi kwa suala la kiafrika, kulingana na yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri mnamo matukio ya mkutano wa vijana wa dunia, ulioshuhudia shughuli adhimu kwa vijana wa nchi za kiafrika, ambapo udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kimageuzi " unaotolewa kwa ( idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia - ofisi ya vijana waafrika) mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi tarehe ya 22 toka Juni ijayo, ulikuja ili kuonyesha umuhimu wa taifa kwake, pia ukifanyika kulingana na imani yake kwa mchango wa vijana waafrika, na dharura ya kutoa njia zote za usaidizi, uwezeshaji, na mafunzo pamoja na kuwawezesha kwenye vyeo vya Uongozi na kunufaisha toka uwezo na mawazo yao.
Na katika jambo hilo, Taasisi kuu kwa Maarifa kupitia lango la kielektroniki lililotolewa kwa mnasaba wa urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika pia linalojumuisha tovuti saba kwenye mtandao wa intaneti kwa lugha za "Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kiamhari,na Kirano, inaangalia udhamini wa "Nasser kwa Uongozi " uliotolewa kwa Wizara ya vijana na michezo kwa Uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy, ukitekleza kwa mpango wa ( milioni moja kwa 2021) ili kuwawezesha vijana waafrika milioni milioni moja kwa kufikia mwaka wa 2021, uliotolewa kwa Kameshina ya elimu, teknolojia, na vyanzo vya binadamu katika umoja wa kiafrika hivi karibuni mjini mkuu wa Ethiopia "Adis Ababa".
Pia Taasisi imesambaza Udhamini kwenye tovuti yake rasmi kwa lugha tatu Kiarabu, Kiingereza, na Kifaransa kupitia mtandao maalumu wa kielektroniki kwa udhamini, na unajumuisha masharti ya kujiunga na fomu ya kusajili.
Inatajwa kwamba Wizara ya vijana na michezo imetangaza kwamba udhamini unawalenga vijana watendaji 120 kutokana na nchi wanachama wa umoja wa kiafrika, wenye maamuzi katika sekta ya kiserikali, watendaji katika sekta binafsi, vijana wa jamii ya kiraia, marais wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, waatalamu katika vyuo vikuu, watafiti wa vituo vya tafiti za kimikakati na kimawazo, wanachama wa vyama vya kiufundi, waandishi, na waandishi wa vyombo vya habari.
Na udhamini unalenga kuhamisha jaribio kale la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana waafrika wenye mitazamo inayoelekea sawa sawa na mielekeo ya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, yenye imani ya kuhudumia malengo ya umoja wa kiafrika kupitia ukamilifu, pamoja na kuunda mkusanyiko kwa viongozi vijana waafrika wenye athari kubwa zaidi barani kwa mafunzo, ujuzi unaohitajika, na mitazamo ya kimikakati.
Pia "Udhamini wa Nasser" unazingatiwa udhamini wa kwanza wa ( kiafrika -kiafrika) unaolenga viongozi vijana watendaji waafrika wenye vitengo tofauti vya uteklezaji ndani ya jamii zao, nao ni mmoja wa vyombo vikali vya kuwezesha kwa mageuzi ya kiafrika vilivyotolewa kikamilifu kwa Ajenda ya Afrika 2063.