Siku moja … Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais wa Ghana Nkrumah na mke wake wa Misri Fathia Rizk Halem na watoto wake watatu waondoka Accra kuelekea Kairo

Siku moja … Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais wa Ghana Nkrumah na mke wake wa Misri Fathia Rizk Halem na watoto wake watatu waondoka Accra kuelekea Kairo

Na/ Said El Shahat

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri iliongea pamoja na ubalozi wake huko Ghana : Mwambie Bi.Fathia aelekea kwa Ubalozi huko na watoto wake watatu na kupeleka barua rasmi kwa Jina la serikali ya Misri kwa mamlaka ya mapinduzi kwa kuacha Bibi huyo Mmisri na watoto wake kuondoka Accra kisha waelekee Kairo. 

Mambo ya Nje ya Misri ilitoa barua hii baada ya mapinduzi ya kijeshi mara moja dhidi ya Rais wa Ghana Nkrumah mnamo Februari 24,1966 na Bibi huyo aliyekusudiwa ni Fathia Rizk Halim , bibi wa Misri aliyeolewa na Nkrumah mnamo Desemba 30, 1957 na alikuwa na umri wa miaka 26 na jina lake likawa kulingana Dkt. Osama Abdeltawab Mohamad katika kitabu yake < Mahusiano kati ya Misri na Ghana 1957-1966>, alithibitisha kwamba hali ya Bi. Fathia ilikuwa kesi ya pili iliyoshughulika Uongozi wa kimisri mara baada ya mapinduzi ; kwani alitoa huduma kubwa kwa uongozi wa kisiasa ya kimisri na serikali ya kimisri iliona kwamba ni wajibu wake  kumlinda, tena yeye hakufuatana na mumewe katika safari yake huko Asia ambayo alianza kabla ya mapinduzi yalipotokea, Misri ilishughulikia umuhimu wa kuwarejesha yeye na watoto wake; wawe na Usalama  kutoka mapya ya matukio huko Ghana, ama suala la  kwanza ambalo Uongozi wa kimisri uliloshughulikia  ni Kuwaangalia kwa ukaribu wamisri wanaopo huko  Ghana, ambapo kulikuwa na Jumuiya kubwa ya wamisri iliyojumuisha walimu wengi, maprofesa wa vyuo vikuu na wataalam wa fani zote, na mnamo  mchana wa Februari 24, ubalozi wa Misri huko Accra kwa Wizara ya Mambo ya Nje huko Kairo ulipeleka barua ya kuthibitisha kwamba Wamisri wote nchini Ghana wako salama kabisa.

“Nkrumah” alikuwa kiongozi wa Ghana aliyeongoza Harakati ya Ukombozi wa kitaifa kwa nchi yake ili kupata uhuru kutoka kwa ukoloni wa Uingereza baada ya kukaliwa kwa zaidi ya karne moja, na tayari aliupata mnamo Machi 1957, na kwa mujibu wa kile kilichotajwa na "Abdel Tawab": " Vita vya Suez vya 1956 vilivuta hisia za Nkrumah kwa Misri na Gamal Abdel Nasser, na alisema kwa zaidi ya tukio moja, akisema: "Baada ya Suez, sote tuligundua kwamba tunaweza kusonga mbele tena tunaweza kufikia. 

Kama kwamba Uongozi wa Kimisri ulimratibu ndoa ili kufanya uhusiano wake na Abdel Nasser kuwa wa kirafiki na mshikamano, na hii inathibitisha kwamba Nkrumah kila anapokuja Kairo, Rais Abdel Nasser alikuwa akifika uwanja wa ndege wa Kairo na familia ya Bi. Fathia, ili iweze kuonekana kuwa Rais Abdel Nasser ni shemeji wa Nkrumah.

Abdel Tawab anathibitisha kwamba Bi. Fathia alitoa huduma kubwa za kitaifa kwa Misri, kwani alikuwa akikutana na Rais Abdel Nasser na familia yake alipokuja Misri na akimjulisha kuhusu shughuli yoyote ya Israeli ambayo ingezuia jukumu la Misri nchini Ghana.

Abdel Tawab anaongeza: “Nkrumah aliathirika sana na Abdel Nasser kiasi cha kumpa mwanawe wa kwanza jina la Gamal, na miezi michache kabla ya kuzaliwa kwake alisema kwamba akiwa mtoto wa kiume ataitwa jina la mtu mpendwa ambaye anamheshimu na kukadiria na akalificha jina hili hadi alipolitoa Aprili 3, 1959.

Nkrumah alikuja Misri mnamo Februari 21, 1966, yaani, siku tatu kabla ya mapinduzi, na kulingana na Al-Ahram Februari 22, alikaa Kairo kwa saa 16 tu, Kisha akaondoka, na Rais Gamal Abdel Nasser alikuwa wa kwanza kumuaga, na akaenda Burma na kisha katika mji mkuu wa China, Beijing, na alipangiwa kwenda "Hanoi" huko Vietnam, kisha Moscow, na Ratiba ya ziara hizi ilikuja katika utekelezaji wa pendekezo la Nchi Zisizofungamana kwa Upande Wowote, ziwe  na nafasi katika kutatua tatizo la vita vya Marekani dhidi ya Vietnam, na matarajio ya kuingilia kijeshi kikamilifu katika maeneo ya Vietnam. Naye Nkrumah amechaguliwa kutoka kwa Mkusanyiko wa Kutofungamana kwa upande wowote ili kujaribu kutatua kesi hiyo, na alitaka kuzuru Kairo ili kufahamu maoni ya Rais Abdel Nasser tena kuyachukua naye huko kwa viongozi wa nchi atakazotembelea, na viongozi wa mapinduzi kutoka jeshi la Ghana walichukua fursa ya safari yake kwa ushirikiano na vikosi vya polisi na kutekeleza utashi wao wa kufanyika mapinduzi dhidi yake.

Bi.Fathia na watoto wake watatu walifikia  uwanja wa ndege wa Kairo baada ya saa sita usiku mnamo Februari 25, na Al-Ahram iliripoti katika toleo lake la Februari 26, 1966, maneno yake kuhusu saa ngumu alizokaa na watoto wake katika makazi yake katika Ikulu ya Jamhuri, na juhudi za balozi wa Misri nchini Ghana, Farid Abdel Qader, kuhakikisha anatoka nje, alikuwa akimsubiri kwenye milango yake, na akamchukua yeye na watoto wake kwenye gari la ubalozi hadi uwanja wa ndege.

Al-Ahram inaongeza kwamba mara tu Bi.Fathia alipotoa kwenye ndege, aliuliza kwa woga: “Mama, yuko wapi? Akamkuta mama yake anamsubiri, wakapeana mabusu, na gari likaondoka nao hadi Ikulu ya Uhuru, na kutoka hapo akampelekea mumewe Nkrumah barua ya kumjuza habari ya kufikia kwake Kairo akiwa na watoto wake watatu, na pia alipeleka barua kwa Balozi wa Misri nchini Ghana, Farid Abdel Qader, akimshukuru kwa jitihada zake pamoja naye, na aliongeza kwa Al-Ahram kuwa Nkrumah alitangaza kutoka Beijing kwamba hivi karibuni atarudi Ghana.

Vyanzo:

Youm7.