Misri na Nyumba ya kiafrika kupitia miaka 60 baina ya mwendelezo na mabadiliko (1)

Misri na Nyumba ya kiafrika kupitia miaka 60 baina ya mwendelezo na mabadiliko (1)

Imefasiriwa na / Aya Nabil

(1) Nasser na Urais wa Umoja wa Kiafrika

Kihistoria, huu ni Urais wa nne wa Misri wa Umoja wa kiafrika - Jumuiya ya Umoja wa Afrika hapo awali - muda wote wa historia  Serikali za Misri zilikuwa na nia ya kuwa na jukumu zuri na la kipekee, lenye majukumu yanayolingana na sifa za Misri na kuendana na mahusiano yake ya asili na bara letu la Afrika, ambalo liliifanya kuwa mhusika wa kikanda mwenye ushawishi katika usawa wa nguvu.


Urais wa kwanza wa Misri wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika ulikuja mwaka 1964, yaani, baada ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo na kutokana na juhudi za Misri zinazoendelea kwa Afrika mnamo kipindi hicho. Wakati huo Rais Gamal Abdel Nasser alikuwa mpangaji, mwandaaji, na msimamizi mkuu wa sera ya kigeni ya Misri kwa Afrika , ambapo alipata msaada kupitia na vyombo vya urais vilivyowakilishwa na Ofisi ya Masuala ya kiafrika ya Uraisi wa Jamhuri, wakiwemo makada wa viongozi wa serikali. kama vile "Helmi Shaarawi" na "Mohamed Fayek", pamoja na Kamati Kuu ya Masuala ya kiafrika, na baadhi ya vyombo vingine vya utendaji kama vile Idara ya kiafrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, vituo vya redio na mashirika maarufu kama vile Kamati ya Misri ya Ushirikiano wa Afro-Asia.

Mnamo kipindi hicho, Misri ilikuwa na jukumu  muhimu katika mafaili yote ya bara hili, na ilikuwa na uongozi  katika kukabiliana na ukoloni wa jadi, ambao baadaye ulikuja juu ya ajenda ya Shirika la Umoja, ambayo  ilianzisha "Kamati ya Uratibu wa Ukombozi wa Afrika.” Misri ilianza tena jukumu lake la kuunga mkono harakati za ukombozi kupitia mfumo huo mpya wa udhibiti wa kiafrika, Bajeti ya Misri ndiyo ilikuwa kubwa zaidi katika Shirika hilo,  iliyokadiriwa wakati huo, kulingana na Kifungu cha 23 cha Hati ya mwanzilishi , kwa takriban Paundi Sterling 100,000.

Kabla ya hapo, Misri ilikuwa na nafasi ya kwanza katika kuunga mkono harakati za ukombozi Barani Afrika kabla ya kuanzishwa kwa shirika hilo,  hii ni kwa sababu "Nasser" aliona wakati huo usalama wa taifa wa Misri unahusishwa na usalama na uhuru wa nchi nyingine za bara hilo, na hivyo basi  ukombozi wa Misri kutoka ukoloni unahusishwa na ukombozi wa nchi zingine za bara. Jambo ambalo lilimwezesha kupokea viongozi kadhaa wa Afrika mjini Kairo, ambapo aliwapatia ulinzi na kufungua ofisi kwa wawakilishi wa vyama vya ukombozi, iwe  kutoka Kenya, Nigeria, Uganda au Somalia, na halafu kutoa misaada ya kijeshi  kwa harakati za  ukombozi wa kitaifa.  Kwa mfano Harakati za ukombozi wa kitaifa nchini Algeria - akivumilia  matokeo ya hayo kutokana na ushiriki wa Ufaransa katika uvamizi wa pande tatu dhidi ya Misri, na si hivyo tu, bali alianzisha pia Umoja wa Afrika mjini Cairo kwa madhumuni ya kuratibu kati ya ofisi za Harakati za ukombozi. na shughuli zao ndani ya mfumo wa siasa ya Misri.idadi ya ofisi ilifikia ofisi 22 na tume mwanzoni mwa miaka ya sitini, na Umoja ulitoa idadi ya majarida muhimu kama vile " Mwamko wa Afrika" ​​na "Ujumbe wa  Afrika."

Pia alitoa mazoezi kwa makada wa Harakati  katika vyuo vya Misri, Shule ya Al-Sa'kaa  na Chuo cha Kijeshi, hayo yote yalichangia kwamba "Kamati ya Uratibu wa Ukombozi wa Afrika" inayofuata Shirika la Umoja wa kiafrika kukamilisha lengo lake na bara zima lilikombolewa kutoka kwa ukoloni,kwa hivyo kamati ilifuta akaunti yake ya benki baada ya kukamilisha kazi yake kikamilifu.

Misri pia iliongoza na  kukabiliana na masuala  ya ubaguzi wa rangi,  na kukataa "Bantustans", na ilikuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara na watu wa Afrika na Harakati za  ukombozi, haswa Afrika Kusini, kupitia makada wake huko Kairo kupitia vipindi vya redio vilivyoelekea kwa Kiingereza, Kizulu na Kiswahili. , na uungaji mkono wake kwa Chama cha kitaifa cha kiafrika (ANC),na Pia ilitoa misaada kwa Harakati za ZANU zilizokuwa zikipigana na wazungu wachache huko Rhodesia - Zimbabwe - sasa.

Huo ulikuwa ni uwasilishaji wa mazingira yaliyoifanya Misri ikawa Rais wa Umoja wa Afrika (zamani,Shirika la Umoja wa Afrika ) Katika enzi ya Abdel Nasser, Sera zilibadilika na mabadiliko ya marais, lakini wote walikubali katika utumishi wa Bara letu la Afrika. Je, ni mazingira gani yaliyoambatana na kurudi kwa Misri katika Urais wa Umoja wakati wa enzi ya Rais El-Sisi?