Waziri wa Vyanzo vya Maji na Umwagiliaji akutana na Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika
Dkt. Mohamed Abdel-Aty, Waziri wa Vyanzo vya Maji na Umwagiliaji, alikutana na Vijana waafrika wanaoshiriki katika "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika "ndani ya matukio ya siku ya kumi na mbili ya Udhamini uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika na Idara kuu ya Bunge na Elimu ya Kiraia) kwa uangalizi wa Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu ,Kuanzia tarehe 8 hadi 22 Juni 2019, kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana wa kiafrika.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt. Mohamed Abdel Qader, Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo wa Masuala ya Vituo vya Vijana, Dkt Mohamed Hassan, Msaidizi mkuu wa Waziri wa Vijana na Michezo wa Vituo vya Vijana, Dina Fouad, Mkuu wa Idara Kuu ya Bunge na Elimu ya Uraia, na baadhi ya Viongozi wa Wizara.
Katika mkutano huo, Dkt. Mohamed Abdel-Aty alijadili Vyanzo vya Maji Barani Afrika, masuala na matatizo yanayolikabili Bara la Afrika, ambayo yanawakilishwa katika Ukame, Mafuriko katika baadhi ya nchi, Uhaba wa maji na nishati, Uchafuzi wa maji, Migogoro ya kisiasa na Mashambulizi ya kigaidi katika baadhi ya nchi, Imaskini, pamoja na Migogoro ya kiuchumi, inayoathiri kufikia ukuaji na maendeleo ya Bara la Afrika, akisisitiza kwamba ongezeko la wakazi ni tishio kubwa, ambayo kwa upande wake huathiri masuala na matatizo yote.
Abdel-Aty alielezea njia za kusimamia maji na nafasi za kubadilisha changamoto zinazokabili nchi za Afrika kwa nafasi za kuhakikisha maendeleo, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na muungano kati ya nchi za Bara la Afrika na kubadilishana na kuhamisha uzoefu kati yao. kukabiliana na matatizo yao kwa msaada wa watu wao, pamoja na haja ya watu kuungana ili kufikia utulivu wa kikanda na kujenga Miundombinu ya nchi za Afrika, na kuongeza ufahamu na kubadilisha maoni na mitazamo kuelekea Bara la Afrika ili kufikia mkakati wa Maendeleo Endelevu na Maoni ya Misri 2030.
Abdel-Aty alisisitiza kuwa kituo cha tahadhari ya mapema cha Wizara hiyo kinahudumia zaidi ya nchi 8 za Afrika na ni maalumu katika kutabiri mafuriko, mvua na mambo mengine, na pia kuna utawala mkuu wa ufuatiliaji na mawasiliano na kuzindua mfumo wa kupima kwa mbali kufuatilia vyanzo vya maji nchini Misri kwa wakati halisi ili kudhibiti kikamilifu kila tone la maji na kuboresha usambazaji wake na kuongeza faida.
Abdel-Aty alieleza kuwa Wizara inalenga kufikia misingi ya mkakati wa 2020 unaojumuisha misingi mikuu minne nayo ni uhaba wa maji, matumizi bora ya maji kwa kuendelea mbinu za Umwagiliaji na kupunguza matumizi, kutafuta vyanzo vya maji kwa kuondoa chumvi kwenye bahari nyekundu na ya kati, kusafisha maji , pamoja na kuwezesha na kupatikana hali ya hewa inayofaa kwa ajili ya kuanzisha njia za mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi kwa kupitia kuandaa kampeni za vyombo vya habari, pamoja na kampeni za uhamasishaji na mikutano ya kubadilishana habari na maono, akisisitiza utayari wa Wizara ya vyanzo vya Maji na Umwagiliaji kutoa aina zote za msaada, mafunzo, kubadilishana na kuhamisha uzoefu wa Misri kwa watu wa bara la Afrika katika nyanja zote ili kukabiliana na changamoto na kufikia maendeleo Barani.
Abdel-Aty aliashiria umuhimu wa kuwepo kwa ushindani kati ya nchi za Afrika kwa ajili ya kuendeleza bara hilo na kufikia ukuaji, haswa kwamba maendeleo na utulivu wa Afrika ni maendeleo ya kweli kwa Misri.