Mohammed Al-Saidi, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ni Mgombea wa uanachama wa Idara ya Kiraia Chini ya Umri kwenye Chama cha Wahandisi

Mohammed Al-Saidi, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ni Mgombea wa uanachama wa Idara ya Kiraia Chini ya Umri kwenye Chama cha Wahandisi

Imefasiriwa na/ Husna Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Mhandisi Mohamed Mohsen Mohamed El-Saidi na umaarufu wake ni Mohamed El-Saidi, mhitimu wa kundi la pili la Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alitangaza kugombea kwake uanachama katika Baraza la Chama kidogo cha Wahandisi huko Kairo Na.(1), ambapo wahandisi wote wa Mkoa wa Kairo watapiga kura katika idara yake yote, na pia aliwasilisha mgombea wa uanachama wa Baraza la Idara ya Kiraia chini ya umri, ambapo wahandisi wote wa kiraia watapiga kura kwenye ngazi ya Jamhuri, na uchaguzi umepangwa kufanyika kesho, Ijumaa, Februari 23, kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo na katika makao yote ya madogo ya Chama katika ngazi ya Jamhuri.

Katika muktadha huo huo, Mhandisi Mohamed Al-Saidi alikuwa na juhudi na ushawishi bora kwenye duru za kiraia, ikiwa ni pamoja na mchango wake katika uanzishwaji wa Kamati ya Msaada wa Kisheria kwenye Chama cha Wahandisi mnamo 2016, pamoja na kazi yake ya kazi wakati wa uanachama wake wa Kamati ya Vijana na Mawasiliano ya Chama mnamo 2018, pamoja na kuwa mmoja wa waanzilishi wa kuwasilisha tatizo la elimu ya uhandisi mnamo 2020, iliyosababisha utoaji wa maamuzi rasmi chini ya Ufadhili ya Kapteni Mhandisi Hany Dahy, pamoja na kuwa mwanachama wa Kamati ya Mafunzo katika Chama kidogo cha Wahandisi huko Kairo tangu 2020 hadi sasa.

Ikumbukwe kuwa shughuli za Udhamini wa Nasser  katika toleo lake la pili zilifanyika mnamo Juni 2021 chini ya kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", iliyolenga kuongeza ushirikiano na mawasiliano kati ya vijana wa nchi zinazoendelea kutoka Ulimwenguni Kusini, na ilikuja na ushiriki wa viongozi wa vijana wa 150 kutoka nchi za 45 kwenye mabara matatu (Asia, Afrika na Amerika ya Kusini) chini ya ufadhili wa Rais wa Jamhuri.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy