Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji wa Vijana

Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji wa Vijana

Lengo kuu la Mwenendo huo ni kuelekeza na kurahisisha utekelezaji wa suala la kutambua gawio la idadi ya watu kwa mwaka wa 2017, ambapo Azimio la Baraza la utendaji (XXII) (EX .CL/DEC .742) la tarehe 14 Januari, 2014 lilivyotaka kutambuliwa gawio wa idadi ya watu katika juhudi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani, kwa nchi wanachama, Jumuiya za Kiuchumi na Kikanda na Washiriki kupitia mafanikio, vituo muhimu na hatua madhubuti.

Kama ilivyoelezwa katika Azimio la (ASSEMBLY/AU/DEC.601 (XXVl)) haswa, Mwenendo unabainisha nyanja muhimu kwa uwekezaji mkuu ulioelezwa kama nguzo muhimu ili kuziwezesha nchi kuongeza uwezo wao wa kutumia gawio la idadi ya watu katika miongo ijayo، na ndani ya kila nguzo, hatua na nyanja hubainishwa hatua na uwekezaji mkuu sambamba na vyombo na mifumo ya sera ya kimkakati ya Umoja wa Afrika, ili kuziwezesha nchi kutumia gawio la idadi ya watu na kuhakikisha utekelezaji kamili wa Ajenda 2063 na Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Ikumbukwe kwamba Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji wa Vijana imejikita katika nguzo kuu nne:

Ya muhimu zaidi ni "Ajira na Ujasiriamali" ambapo unalenga kufanya kazi na washiriki katika sekta binafsi ili kuongeza mafunzo na elimu ya ufundi stadi na kuongeza fursa za mafunzo kazini kwa Wanawake na Vijana.

Pamoja na kuunganisha taasisi za hiari Barani Afrika, watendaji na sekta ya kibinafsi na kuimarisha majukumu yao ya kijamii, ili kuendeleza na kusaidia mipango ya mabadiliko ya Maendeleo ya Vijana kuelekea kuandaa ujuzi na uwezo wa Vijana katika uwanja wa Ujasiriamali.

Licha ya kuendeleza programu za kujitolea za Vijana, programu za Vijana Wachipukizi wafundi, na fursa nyingine za mafunzo ili kukuza uwezo na kuwapa Vijana waafrika fursa ya kujihusisha na mashirika ya kikanda na kimataifa.

Nguzo ya pili inazingatia elimu na ukuzaji wa ujuzi, iwe na matarajio ya kuanzisha na kuimarisha taasisi za elimu za kikanda ambazo hutoa fursa za elimu na kubadilishana kwa wanafunzi katika pande zote za Afrika.

Pamoja na nguzo ya tatu inayojali Afya na Burudani, pia inajali kikubwa suala la wa kueneza uelewa wa Afya ya Uzazi, na elimu pia inazingatia athari hiyo kwa upande wa maendeleo na ustawi wa Vijana shuleni na wengine, na utekelezaji wa programu bunifu za kubadilisha tabia kwa kutumia vyombo vya habari na teknolojia mpya.

Hatimaye, nguzo ya nne, ikiwa pamoja na “Haki, Utawala na Uwezeshaji wa Vijana” ilisisitizia “kuandaa kozi za mafunzo ya uongozi na uwezeshaji wa Vijana kwa lengo la kuthibitisha maadili na matarajio ya Kiafrika ndani ya Vijana.