Machu Picchu, Ngano Iliyopotea Juu ya Mawingu, na Njia ya Furaha, Sant Catherine

Machu Picchu, Ngano Iliyopotea Juu ya Mawingu, na Njia ya Furaha, Sant Catherine

Imetafsiriwa na/ Ahmed Salama
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
                           
Machu Picchu ni ngano iliyopotea  juu ya mawingu na baadhi ya watu wanaiita Jiji la Machu Picchu au Kasri  lililopotea. Neno Machu Picchu katika lugha ya Inca linamaanisha kilele cha milima ya kale. Kasri hilo liko katika mji wa Cusco, huko nchini Peru, kati ya milima miwili ya Andes na chini yake kuna mto wenye maji yenye haraka na inafunikwa na misitu mizito. Liliorodheshwa kwenye orodha ya Maajabu Saba ya Dunia mpya na UNESCO mnamo 1983, yaani miaka takriban 50 baada ya ugunduzi wake.

Machu Picchu ulijengwa katika enzi ya utamaduni wa Inca mwishoni mwa karne ya 15, na una mitaa iliyopangwa vizuri, majumba, na bustani, na hata Mawe yalijengwa juu ya mengine bila matumizi yeyote ya ujenzi.

Saint Catherine ni barabara ya furaha, kwa sababu hiyo inakuwa eneo linalostahili kuchunguza ndani ya milima, mabonde yake, vyanzo vya maji, na maeneo ya kihistoria ambayo hufufua kutamba historia, utamaduni, na utukufu wa Wamisri wa zamani.

Mji wa Saint Catherine ni miongoni mwa miji maalumu na ya kipekee zaidi huko mjini Sinai. Unakaa kwenye uwanja wa juu, ukiwa unakaribia mita 1,600 juu ya usawa wa bahari.  Inazungukwa na safu za milima ambazo ni kubwa zaidi katika Sinai, bali hata katika Misri kwa ujumla.


Mlima huu ni miongoni mwa milima ya juu kabisa huko nchini Misri, ambapo  urefu wake umekuwa 8,563 futi juu ya usawa wa bahari. Unaitwa  kwa jina hilo kwani imetajwa kwenye mila za wamonaki  kwamba wakati wa nyuma,  malaika walibeba mwili wa Mtakatifu Catherine kutoka mahali alipopewa kifo chake huko mjini Alexandria mwaka 307, na kuupeleka mlimani hapa, ilihali wakati wa kisasa, tunaweza kuona fuvu lake na mfupa wa mkono mmoja uliohifadhiwa ndani ya sanduku ndani ya kanisa, hadi leo, na kutoka kilele chake, mtu anaweza kuona Ghuba ya Aqaba na Ghuba ya Suez, hususan wakati jua linang'aa.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy