Kumbukumbu ya Kifo cha Marehemu Rais Abeid Amani Karume

Kumbukumbu ya Kifo cha Marehemu Rais Abeid Amani Karume

Imefasiriwa na / Aya Nabil

Leo ni kumbukumbu ya miaka 51 ya Kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Sheikh Abeid Amani Karume.

Sheikh Abeid Karume alizaliwa katika mji wa "Pongwe"  kisiwani mwa  "Unguja" mnamo Agosti 4, 1905, kwa familia ya watu 6, baba yake aliaga Dunia mwaka 1909 akiwa na umri wa miaka minne, Karume alipata elimu ya Qur'an na kuanza masomo yake ya kimsingi katika shule ya "Mwera", mwaka 1913 alihamia na mama yake kwa mji wa "Unguja" kuendelea na masomo yake na  huko aliishi na baba yake mdogo aliyekuwa Sajin katika jeshi la polisi la Mfalme, lakini kwa bahati mbaya, kipindi cha masomo yake kilikuwa miaka mitatu tu.

Na mnamo mwaka wa 1920 alifanya kazi kama baharia katika boti za usafirishaji wa mizigo  mbele ya kisiwa na hatimaye alipata cheo cha kamanda wa wafanyakazi, na baada ya  mwaka wa 1938 aliongoza kundi la boti za mvuke zilizobeba abiria kutoka na hadi bandari,kisha akaondoka Zanzibar katika miaka ya mwanzo ya maisha yake, akihamahama baina ya  sehemu kadhaa za dyunia hadi alipofika London, ambapo alipata uzoefu mkubwa katika jiografia ya kisiasa na masuala ya kimataifa wakati wa mikutano yake na wasomi waafrika kama vile Kamuzu Banda kutoka Malawi.

Karume alishughulikia siasa kwa mara ya kwanza mwaka 1954, na katika miaka ya kabla ya Mapinduzi ya 1964, Karume aliongoza chama cha Afro-Shirazi kupinga muungano wa utawala wa Kiarabu ulioonekana kuwa na lengo la kudumisha utawala wa kisiasa na kiuchumi wa jamii ya Kiarabu. Mnamo Januari 12, 1964, wafuasi wa chama cha Afro-shirazi walimshinda Sultan Jamshid bin Abdullah na kuanzisha utawala wa Afrika, na Karume alikuwa kiongozi wa Baraza la Mapinduzi na kisha Rais wa Jamhuri mpya ya Watu wa Zanzibar,Sheikh Abeid Karume alipewa jina la "Rais wa kwanza wa Zanzibar" baada ya mapinduzi yake ya kukomesha ufalme wa Zanzibar, tena kulingana na historia rasmi ya Zanzibar, Abeid Karume alikuwa kiongozi wa chama cha Afro-shirazi na ndiye mpangaji na kiongozi wa mapinduzi.

Karume alichukua hatua yake ya pili muhimu ya kisiasa alipokubali kuunda Muungano na Rais wa Tanganyika Julius Nyerere Aprili .Muungano huo umesababisha nchi mpya iitwayo Tanzania, hivyo akawa Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na mnamo Aprili 7, 1972 Karume ameuawa na watu wanne wenye silaha katika makao makuu ya Chama chake cha Afro-Shirazi.

Kwa hivyo siku hiyo inakuja kuadhimisha kumbukumbu yake, ni sikukuu rasmi nchini  Tanzania, na ni siku maalum kwa watanzania kukumbuka mafanikio ya mtu huyo mkuu, pia viongozi na marais  husherehekea siku hiyo kwa kwenda kaburi ya Sheikh Abeid Karume, na kuweka maua juu ya kaburi lake na kusalia kwa ajili yake.