Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye Karamu ya Chakula cha Mchana Iliyoandaliwa na Waziri Mkuu wa Umoja wa Kisovieti kwa Heshima yake mnamo Mwaka 1958
Imetafsiriwa na/ Neema Ibrahim
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kupitia karamu ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Waziri Mkuu wa Umoja wa Kisovieti kwa Heshima yake mwaka 1958.
Ziara hiyo iiliyo muhimu sana katika mahusiano kati ya Umoja wa Kisovieti na Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu (Siria na misri). Kwa mara ya kwanza, tunakutana na viongozi wa Umoja wa Kisovyeti, na tunazungumza kwa mambo yote kwa wazi.
Ushirikiano uliofanyika katika miaka michache iliyopita kati ya Umoja wa Kisovieti na Jamhuri yetu ya Kiarabu umethibitisha kwamba inaweza kufuata sera inajenga kwa ushirikiano na urafiki.
Usaidizi wako kwetu haukutegemea sharti au jukumu lolote. Umeheshimu sera yetu ya kujitegemea kila wakati. Hakutokia uingiliaji kwa njia yoyote, na uliheshimu Sera chanya ya kutopendelea upande wowote ambayo tulitangaza. Mazungumzo yaliyofanyika baina yetu yamedhihirisha kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umetegemea katika urafiki na uongofu, kama ilivyoelezwa pia katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, ambayo itapokelewa kwa shukurani kamili na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu.
Matangazo ya uadui na propaganda za kikoloni zilijaribu kuibua mashaka baina ya watu wa taifa la Kiarabu kuhusu ushirikiano wao na Umoja wa Kisovieti, na nilisema katika taarifa zangu nyingi kwa magazeti ya Uingereza na Marekani kuhusu uzoefu wetu katika ushirikiano na Umoja wa Kisovieti: Ushirikiano huu ni ushirikiano wa uongofu kwa kutusaidia kukomboa na kuondokana na ushawishi wa kimagharibi , ili kutusaidia katika maendeleo ya kiuchumi na ili nchi yetu iwe ya viwanda, na kwamba anayetaka kuitawala nchi yetu hawezi kuisaidia kufikia vituo vya nguvu, iwe kwa upande ya nguvu za kijeshi au kutoka upande wa ujenzi wa viwanda.
Tulipigania ili hawajumushii ushawishi wa nchi za kikoloni, na tuliamua kwamba sera yetu itakuwa huru na inatokana na dhamiri ya nchi yetu, hawakuwi katika ushirikiano wetu katika miaka minne iliyopita, tulikuwa wafuasi wa sera ya ukombozi tuliipanga, na miaka hii imeongeza uthabiti wetu katika kuifuata.
Ushirikiano huu ulikuwa mafanikio ya vimaadili vilivyotangazwa na Mkutano wa Bandung, ambazo ni kanuni za kuishi kwa Amani na ushirikiano kati ya mataifa, bila kujali mifumo yao tofauti ya kijamii.
Tulishiriki katika mkutano huu, na tulikuwa kuzieleza hisia za watu wa Kiarabu walioteseka kutokana na udhibiti wa ukoloni, na wanaotaka ukombozi wa kisiasa na kiuchumi, na pia wanataka kujenga uchumi wao katika muundo imara na mzuri.
Hii ndiyo sera ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu; Uhuru kwa watu wote wa Kiarabu, na ushirikiano na nchi bila jukumu au sharti. Ninafurahi kwamba mazungumzo yetu yamethibitisha uelewa wetu kamili katika suala hili, na kwamba - Mungu akipenda- tutaendelezia ushirikiano huo unaozingatia urafiki na uaminifu.
Tuliomba kwenye Mkutano wa Bandung ili kuzuia majaribio ya atomiki, kuzuia matumizi ya silaha za nyuklia, na kutumia atomi kwa malengo ya amani ili kusaidia nchi za nyuma ya kiuchumi. katika utumishi wa binadamu. Ulipotangaza - Mheshimiwa Rais - uamuzi wako wa kupiga marufuku majaribio ya atomiki katika Umoja wa Kisovieti, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ilitangaza kwamba inaunga mkono uamuzi huu, na kutoa wito kwa nchi zote kukuunga mkono, na kuomba makubaliano ya kuzuia matumizi. ya silaha za nyuklia.
Majaribio ya atomiki yanaathiri ubinadamu, na tuna haki ya kutetea utu na binadamu, na pia tuna haki ya kuomba kuzuia majaribio ya atomiki katika sehemu tofauti za ulimwengu, haswa baada ya kutangazwa kuwa Ufaransa itafanya majaribio ya atomiki katika Afrika; Jambo ambalo linaziweka nchi za Kiarabu kwenye hatari.
Hii ilitangazwa katika Mkutano wa Bandung mwaka 1955; Ilitangaza kanuni za kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano kwa ajili ya amani ya dunia, na tuliunga mkono hili mwishoni mwa 1957 katika Mkutano wa Watu wa Afrika-Asia uliofanyika Cairo.
Mwezi huu, Mkutano wa Nchi Huru za Kiafrika ulifanyika mjini Accra, na maoni yote katika mkutano huu yanathibitisha vimaadili vya Bandung na kuziathiriwa nayo.
Nimefurahishwa - Mheshimiwa Rais - maelezo yako ya uelewa wako kwa mapambano ya nchi za Kiarabu kwa uhuru , na kuelewa kwako hatari ya Israeli ambayo inatishia nchi za Kiarabu. Kwa Kuzingatia Israeli kama njia ya ukoloni.
Watu wa Jamhuri ya Muungano na watu wa Kiarabu wanakutazama kama rafiki ambaye huwasaidia bila sababu au maslahi. Lakini ili kuthibitisha uhuru wake na uhuru, kama ulivyoelezea katika hotuba yako hivi sasa. Tunathamini urafiki huu na tunajitahidi kuuanzisha, kuuimarisha na kuudumisha.
Katika hotuba yangu, natumai kuwasalimu urafiki wa Soviet-Waarabu, Rais Khrushchev na viongozi wa kirafiki wa Soviet, na ninakutakia pia likizo njema.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy