"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " watembelea Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo 

"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " watembelea Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo 

Leo Jumanne, wajumbe wa Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  katika toleo lake  la pili, wametembelea Chuo cha kitaifa cha Mafunzo, kwa mahudhurio ya  Mratibu Mkuu wa Udhamini huo , Hassan Ghazali, ikiwa ni pamoja na  shughuli za siku ya kumi na tano na ya mwisho kutoka Udhamini wa Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser wa Uongozi wa Kimataifa, ukifanyika kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Misri, ukiwa na kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini ".

Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo hicho Dkt.Rasha Raghe alikuwa wa kwanza aliyewakaribisha  wajumbe wa Vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo kwa toleo lake la pili, ambapo mwanzoni mwa hotuba yake aliwakaribisha,akisisitiza kuwa Udhamini huo , uliofanyika kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri na unaotekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo kwa ushirikiano na Chuo cha kitaifa cha Mafunzo, unatokea ndani ya mfumo wa jukumu  la Misri la  Uongozi kwa kukuza mahusiano ya ushirikiano na mahusiano ya pamoja na jamii, haswa   upande wa Vijana katika nchi mbalimbali Duniani, haswa wawakilishi wa mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya Kusini wanaoshiriki katika shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili.

Wakati wa ziara yao kwa Chuo cha kitaifa cha Mafunzo, Wajumbe wa Vijana wanaoshiriki  katika Udhamini huo walitazama majengo ya chuo hicho na kusikiliza maelezo ya kina kwa falsafa ya ufundi wa majengo na hatua zinazofuata kwa kukamilisha mipango ya Chuo hicho kwa kuwawezesha watalaamu vijana  , pamoja na jukumu la  uongozi  la Chuo hicho katika kuwakuza vijana katika nyanja zote.

Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  , aliashiria   kuwa shughuli za Udhamini huo ulijumuisha   kuandaa ziara kadha za washiriki wa Udhamini  kwa maeneo mbalimbali , ikiwa ni pamoja na Chuo cha kitaifa Mafunzo , Mamlaka ya Mfereji wa Suez Panorama ya Vita vya Oktoba, Piramidi za Giza na Saqqara, na Makumbusho ya Jeshi la Wanahewa, Shirika la  kiarabu la utengenezaji, Chuo cha Polisi, Bunge, Kituo cha Tafiti za Kilimo, na maktaba wa Alexandrina, kwa lengo la kutambulisha wajumbe wa vijana kutoka mabara matatu ( Afrika, Asia na Amerika Kusini) wanaoshiriki katika Udhamini kwa vivutio vya ustaarabu wa Misri na kiwango cha maendeleo ambacho Misri inakishuhudia sasa  hivi na kuangalia uzoefu wa Misri katika nyanja mbalimbali na maendeleo ya sasa iliyofikia katika nyanja mbalimbali.

Ghazali ameshaongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkubwa wa Misri katika kuthibitisha na kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana wa mabadiliko wenye maoni yanayoendana na Maelekezo ya Urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia Ukamilifu, pamoja na kuunganisha viongozi vijana wenye uwezo wa  Kuathirika zaidi Duniani kwa mafunzo, ujuzi muhimu na maoni ya kimkakati.

Ikumbukwe kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa lilitolewa mnamo Juni 2019, kwa uangalizi wa Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mustafa Madbuli, lililolenga viongozi vijana wenye ujuzi wa utendaji  tofauti na ufanisi ndani ya jamii zao kwa ajili kuhamisha uzoefu wa kimisri wa kimaendeleo katika kuthibitisha Taasisi na kuunda Taswira ya kitaifa.