Historia Kuu ya Afrika

Historia Kuu ya Afrika

Imefasiriwa na /  Mervat Sakr

Mwaka 1964, UNESCO ilizindua mradi wa kuunda "Historia Kuu ya Afrika" ili kubadilisha ukosefu wa maarifa uliopo wa historia ya Afrika. Changamoto iliyopo ni kuijenga upya historia ya Afrika na kuikomboa dhidi ya chuki zozote za kikabila za biashara ya watumwa na ukoloni, na hivyo kuendeleza mtazamo wa Kiafrika kuhusu historia hiyo.

Ili kufikia lengo hilo, UNESCO iliomba msaada kutoka kwa kundi la wataalamu wakuu wa Afrika na wasio Waafrika wakati huo, ambapo kazi ya wataalamu hao ni kama miaka 35 ya ushirikiano kati ya wanahistoria na wataalamu zaidi ya 230, chini ya usimamizi wa kamati ya kimataifa ya kisayansi, theluthi moja ya wanachama wake wanatoka Afrika.

Mkusanyiko wa Historia Kuu ya Afrika ni kazi ya upainia, isiyo na kifani katika jitihada zake za kufunika historia ya bara zima la Afrika, kuanzia kuibuka kwa wanadamu hadi changamoto za kisasa zinazowakabili Waafrika na Waafrika walio ughaibuni Duniani. Mpango huo wa Historia Kuu ya Afrika hauruhusu kipindi chochote cha historia ya bara hili kuachwa ovyo, ikiwa ni pamoja na kipindi cha kabla ya ukoloni, na kushughulikia hatima ya Afrika kama sehemu muhimu ya hatima ya binadamu wote, kwa kuangazia uhusiano wake na mabara mengine na kuonesha mchango wa tamaduni za Kiafrika katika maendeleo makuu ya Utu.

Mkusanyiko kamili ulichapishwa katika juzuu nane, wenye vielelezo vingi vya ramani, chati, takwimu, michoro na uteuzi wa picha nyeusi na nyeupe, na maandiko mengi yametangazwa kikamilifu na kuambatana na yaliyomo na orodha kamili ya marejeleo.

Mnamo miaka ya hivi karibuni, UNESCO imeanza mchakato wa kuandaa na kuunda juzuu tatu mpya za Historia Kuu ya Afrika (juzuu ya tisa, kumi na ya kumi na moja).

Uafrika Duniani: Dhana ya Ubunifu

Afrika na makundi ya Waafrika walio ughaibuni mara nyingi yalionekana kama makundi mawili tofauti kabisa, na walipata mawasiliano machache wakati wa vipindi vifupi vya kihistoria. Kwa maana hii, waandishi wa juzuu mpya za Historia Kuu ya Afrika wanataka kukanusha mtazamo huu wa kidunia na wa juujuu wa uhusiano kati ya Afrika na Waafrika na Diaspora Duniani kote.

Kwa kuanzisha dhana hii ya ubunifu ya Kiafrika kuwa ya ulimwengu, Kamati ya Kimataifa ya Sayansi inataka kurekebisha uhusiano huo. Dhana hii inaruhusu uelewa mzuri wa mahusiano ambayo yamewaleta Waafrika na watu wenye asili ya Afrika pamoja katika historia, kwani ni mchakato unaotegemeana na unaoendelea unaojumuisha harakati za watu, kubadilishana maarifa, kujua na matukio ya kiutamaduni yanayotokana na urithi wa Kiafrika.

Dhana hii pia inazembea suala la rangi, badala yake inalenga sura tofauti za uwepo wa Waafrika katika maeneo mbalimbali Duniani na alama nyingi inazoziacha katika tamaduni nyingine. Kuzungumza kijiografia, dhana hii itachangia kuvunja mila potofu zinazotazama uwepo wa Afrika tu kwa mtazamo wa ulimwengu wa Atlantiki (Ulaya, Amerika, Caribbean) ili kushughulikia uwepo wa Afrika kwa njia inayoendana na enzi za utandawazi, kwa kuzingatia ughaibuni katika Bahari ya Hindi, Mashariki ya Karibu, Mashariki ya Kati na Asia.

Tangu nyakati za kale, uwepo wa Waafrika umekuwa kielelezo muhimu sana ya kufahamu zaidi kuhusu tofauti yanayotoka Afrika (utafiti na upanuzi wa Kiafrika nje ya bara, kuwarudisha Waafrika kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya dunia kupitia biashara haramu, mawimbi ya uhamisho yanayotokana na ukoloni, na harakati za kuhama baada ya ukoloni).Mbali na jukumu la dhana ya Kiafrika kuwa mali ya ulimwengu katika kuakisi utofauti wa mawimbi haya na mwendelezo wa mahusiano, pia inaruhusu uelewa mzuri wa matarajio ya vizazi vipya Barani Afrika na makundi ya Waafrika walio ughaibuni kuchangia ufufuo wa Afrika na ujenzi wa umoja wa Afrika katika karne ya 21.

Juzuu ya kwanza: Mbinu na Zama ya kabla ya Historia Barani Afrika

Juzuu ya kwanza ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inahusika na kabla ya Afrika na mbinu zake. Sehemu ya kwanza ya juzuu inatathmini mahali ambapo jamii za Kiafrika zinaambatanisha na historia yao, pamoja na kiwango cha ukuaji na maendeleo katika dhana ya kihistoria ya Kiafrika. Sehemu ya kwanza pia inajumuisha muhtasari wa vyanzo na mbinu.

Sehemu hii inafuatiwa na maelezo ya vyanzo vya msingi vya fasihi, mapokeo ya mdomo na hai pamoja na akiolojia na mbinu za Kiafrika. Sura ya 10, 11 na 12 zinashughulikia masuala ya lugha na masuala ya uhamiaji.

Sehemu ya pili ya juzuu hiyo inaangazia kuibuka kwa mwanadamu na kabla ya historia Barani Afrika kulingana na maeneo ya kijiografia: Afrika Kaskazini, Kusini mwa Afrika, Afrika Mashariki, Afrika Magharibi, Afrika ya Kati na Bonde la Mto Nile. Baadaye sura zinajitolea kwa sanaa ya Kiafrika ya awali, mbinu za kilimo, na maendeleo na uenezaji wa madini. 

Juzuu ya Pili: Ustaarabu wa Afrika ya Kale

Juzuu hii inazingatia kipindi cha tangu mwisho wa kipindi cha Neolithic hadi mwanzo wa karne ya 7 ya zama yetu. Kipindi hiki cha miaka 9,000 kinagawanyika katika maeneo makubwa ya kijiografia kulingana na utafiti wa kihistoria wa Kiafrika. Sura mbalimbali katika juzuu hii zinashughulikia Bonde la Mto Nile, Misri, Nubia, nyanda za juu za Ethiopia, Morocco, na maeneo ya jangwa, pamoja na maeneo mengine ya Afrika na kundi la visiwa vya Bahari kuu ya Hindi.

Tunaona vizuri kwamba sehemu kubwa ya juzuu ya pili imejitolea kwa ustaarabu wa Misri ya kale kutokana na nafasi yake ya kifahari mwanzoni mwa historia ya Afrika.  

Juzuu ya Tatu: Afrika kuanzia Karne ya 7 hadi ya 11

Juzuu ya tatu ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inatoa historia ya Afrika kuanzia karne ya saba hadi ya kumi na moja.

Juzuu hii inachunguza harakati mbili zimezokuwa na umuhimu mkubwa na endelevu wa kiutamaduni, kisiasa, na kiuchumi katika historia ya bara la Afrika: kuongezeka kwa ushawishi, kuenea, na mwingiliano wa Uislamu na utamaduni wa jadi wa Kiafrika katika maeneo ya kaskazini na magharibi, pamoja na kuenea kwa watu wanaozungumza Kibantu katika mikoa ya kusini.

Mwanzoni mwake inaelezea Afrika ndani ya mfumo wa historia ya dunia mwanzoni mwa karne ya saba. Halafu inagusa athari ya jumla ya kuibuka kwa Uislamu, kuendelea kuenea kwa watu wanaozungumza Kibantu, na kukua kwa ustaarabu katika maeneo ya Sudan na Afrika Magharibi.

Juzuu hiyo pia ina sehemu za kina juu ya hatua za maendeleo ya Uislamu katika Afrika ya Kaskazini na athari zake, Christian Nubia, ustaarabu wa savanna, misitu na pwani ya Afrika Kusini, Pembe ya Afrika, pwani ya Afrika Mashariki, maeneo yanayoendelea, Afrika ya Kati, Afrika Kusini, na maendeleo ya ndani ya Madagaska na uhusiano wa nje. Sura tatu za mwisho zinashughulikia ughaibuni wa Kiafrika Barani Asia, uhusiano wa kimataifa na kuenea kwa teknolojia na mawazo katika bara la Afrika, pamoja na uchambuzi wa athari za jumla za kipindi hiki katika historia ya Afrika.

Juzuu ya nne : Afrika kutoka karne ya 12 hadi ya 16

Juzuu ya nne ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inahusika na historia ya Afrika kuanzia karne ya kumi na mbili hadi kumi na sita.

Kipindi hiki kinaashiria kipindi muhimu katika historia ya bara la Afrika kwani kilishuhudia maendeleo ya utamaduni wake wa Kiafrika na rekodi zake zilizoandikwa zikiwa maarufu zaidi. Eneo hili lina sifa ya mfululizo wa matukio mashuhuri kama vile: ushindi wa Uislamu, upanuzi wa mahusiano ya kibiashara, kustawi kwa mahusiano na watu na mabadilishano ya kiutamaduni, maendeleo ya falme na himaya.

Juzuu ya kwanza inaanza na maelezo ya "Dola ya Almohad". Halafu inagusa ustaarabu tofauti ambao umefanikiwa Afrika Magharibi (Mali, Songhai, Niger, Bonde la Volta, Chad na Hausa, pamoja na watu wa pwani kutoka Casamance hadi Cameron). 

Katika sura zinazofuata, Juzuu inahusika na maeneo ya Kaskazini Mashariki na Afrika Mashariki kutoka Misri hadi Nubia, Ethiopia, na nchi za Pembe ya Afrika. Juzuu hiyo inataja nyenzo kuhusu maendeleo ya ustaarabu wa Kiswahili. Juzuu hiyo kinahusika na maeneo ya Afrika ya Kati katika sura zilizojitolea kwa eneo kati ya pwani na maziwa makuu, mabonde ya Dhimbezi na mito ya Limpopo.
 
Pia kuna sura zilizowekwa wakfu kwa Afrika ya Ikweta, Angola, Afrika Kusini, Madagaska na visiwa jirani.

Juzuu ya tano: Afrika kuanzia Karne ya 16 hadi ya 18

Juzuu ya tano ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inahusika na historia ya Afrika tangu mwanzo wa karne ya kumi na sita hadi mwisho wa karne ya kumi na nane. Nayo inashughulikia mada kuu mbili nazo ni :
 Maendeleo endelevu ya ndani ya nchi na tamaduni za Kiafrika katika kipindi hiki, na kuongezeka kwa ushiriki wa Afrika katika biashara ya nje, iliyosababisha matokeo kwa ulimwengu wote ambayo hayakutabiriwa wakati huo.

Juzuu hiyo inahusika na ushindi wa Ottoman wa Misri katika Afrika ya Kaskazini na kuanzishwa kwa majimbo huko Tripoli, Tunisia, na Algeria. Juzuu hiyo kisha kinashughulika na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kuanguka kwa baadhi ya majimbo makubwa na ya zamani kama vile Chungai, Sudan Kusini, Ethiopia ya Kikristo, na kuibuka kwa misingi ya kisiasa ya kati (Ashanti, Dahomey, na Sakalava),  iliyosababisha kuibuka kwa matabaka tofauti ya kijamii na tabia ya wazi ya kishirikina. Dini za jadi ziliendelea na Ukristo na Uislamu.

Kando ya Sahel, haswa Afrika Magharibi, Wazungu waliunda mtandao wa biashara pamoja na maendeleo ya kilimo katika ulimwengu wa kisasa, ukawa lengo la biashara ya utumwa ya kimataifa. Juzuu hii inachunguza matokeo ya moja kwa moja ya biashara hii barani Afrika. Juzuu hiyo pia kinasema kuwa athari za muda mrefu duniani ni pamoja na kuanzishwa kwa uchumi wa sasa wa dunia na ukosefu wake wote wa usawa.

Juzuu ya sita: Afrika kuanzia Karne ya 19 hadi 1880

Juzuu ya sita ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inashughulikia historia ya Afrika tangu mwanzo wa karne ya kumi na tisa hadi mwanzo wa "mkanyagano" wa Ulaya katika nchi za makazi ya miaka ya themanini. 

Ingawa uwepo wa Ulaya kibiashara, kidini, na kisiasa ulipanuka wakati wa karne, athari za nje hazikuwa na athari kwa jamii za Kiafrika kwani kulikuwa na majaribio mbalimbali ya kiutamaduni ya kufanya upya, kupanua na kuendeleza misingi iliyopo. Kipindi hiki kilishuhudia matukio mawili muhimu: "Mifikani" ya Afrika Kusini na upanuzi wake kwa Afrika ya Kati na Mashariki, na harakati za mageuzi ya Kiislamu ya Afrika Magharibi,  sura nane za juzuu hii zimeyowekwa wakfu.

Juzuu inaanza na sura nne zinazoelezea watendaji wakuu katika jamii ya Kiafrika mwanzoni mwa karne, jukumu la Afrika kubadilika katika uchumi wa dunia, mwenendo mpya na taratibu, na athari za kukomeshwa kwa biashara ya utumwa. Kisha sura 23 zinaelezea mageuzi ya kila mkoa. Katika sura mbili za mwisho, juzuu hiyo inashughulikia ughaibuni wa Kiafrika na hupima hali ya maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ya bara hilo katika kipindi cha ushindi wa Ulaya.

Juzuu ya Saba - Afrika likitawaliwa wa kikoloni 1880-1935

Juzuu ya saba ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inahusika na kipindi cha kugawanya, ushindi na ukaliaji wa bara la Afrika tangu mwanzo wa utitiri wa Ulaya Barani Afrika hadi uvamizi kali wa Italia kwa Ethiopia mnamo 1935. Juzuu hii inalenga kwa upana majibu ya Waafrika wenyewe kwa tishio la ukoloni. 

Sura mbili za kwanza zimejikita katika mitazamo na utayari wa Waafrika kukabiliana na kipindi cha ukoloni pamoja na majaribio ya Ulaya katika ukoloni. Sura saba zifuatazo zinashughulikia mipango na athari za Kiafrika mbele ya ugawaji na ushindi hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Juzuu kisha hutoa uchambuzi wa kina wa kikanda wa kipindi hiki.

Sehemu ya Sura ya 13 hadi Sura ya 21 inashughulikia athari za kiuchumi na kijamii za tawala za kikoloni kwa Afrika kuanzia 1919 hadi 1935: utaratibu wa uchumi wa kikoloni katika maeneo ya Afrika Kaskazini yaliyokuwa chini ya ukoloni wa Kifaransa, Ubelgiji, Kireno na Uingereza, kuibuka kwa miundo mipya ya kijamii na idadi ya watu, na jukumu la imani za kidini na sanaa Barani Afrika wakati wa ukoloni. Sehemu ya mwisho ya juzuu hiyo inahusika na kuongezeka kwa harakati za kupinga ukoloni, kuongezeka kwa utaifa wa kisiasa wa Kiafrika na uhusiano kati ya Waafrika weusi na kama yao katika Ulimwengu Mpya. Juzuu hiyo kinatoa sura maalum kwa Ethiopia na Liberia.

Juzuu ya nane- Afrika tangu 1935

Juzuu ya nane na ya mwisho ya Historia Kuu ya Afrika ya UNESCO inashughulikia kipindi cha kuanzia 1935 hadi leo. Juzuu hiyo inahusika na vipimo vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni vya bara hili kwa kuzingatia maendeleo ya juhudi za ukombozi kutokana na utawala wa kikoloni.

Kwa Afrika, mwaka wa 1935 ulikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili Duniani kwa uvamizi wa Mussolini nchini Bulgaria. Sehemu ya kwanza ya juzuu hii inahusika na mgogoro wa kimataifa, ikielezea migogoro katika Pembe ya Afrika, Afrika Kaskazini, na maeneo mengine yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Ulaya.
 
Sehemu tatu zifuatazo zinazungumzia mapambano makubwa ya Afrika ya uhuru wa kisiasa kutoka 1945 hadi uhuru, ukuaji wa uchumi na uhuru, ujenzi wa taifa na mabadiliko ya miundo na maadili ya kisiasa. 

Sehemu ya tano inashughulika na mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni tangu 1935 kutoka dini hadi fasihi, kutoka lugha hadi falsafa, kutoka sayansi hadi elimu. Sehemu mbili za mwisho zinaangazia mageuzi ya Harakati ya Umoja wa Afrika na jukumu la Afrika huru katika masuala ya Dunia. Juzuu hiyo inaangazia uingiliano kati ya Afrika na Dunia nzima, ikikiri kwamba ubeberu wa Ulaya ulikuwa na jukumu muhimu katika kuamsha dhamiri ya Afrika. 

Juzuu ya tisa

Juzuu ya tisa inalenga kusasisha yaliyomo katika juzuu nane za kwanza za Historia Kuu ya Afrika kwa kuzingatia maendeleo mapya katika tafiti. Kwa kupitia upya mazoea ya kinadharia na mbinu za kuandika historia ya Afrika, juzuu hii inalenga kuangalia historia ndefu ya Afrika kwa mtazamo mpya, na kuongeza awamu nyingine kama vile historia ya awali ya Bara la Afrika. 

Sehemu ya kwanza inachunguza misingi ya kitaaluma, mbinu na nadharia inayozingatia historia ya Afrika na vikundi vya asili ya Kiafrika katika karne ya ishirini na moja. 

Sehemu ya pili inapitia maudhui ya juzuu nane za kwanza zilizochapishwa za Historia Kuu ya Afrika.

Sehemu ya tatu inatoa taarifa kuhusu historia ya awali ya bara hilo,  iliyojulikana kama kabla ya historia.

 Sehemu ya nne na ya mwisho inakagua maendeleo mapya katika masomo ya kihistoria (maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa katika ngazi ya bara) katika kipindi cha miaka 2,000. 

Juzuu ya Kumi 

Juzuu hii inatoa muhtasari muhimu wa mienendo ya uhusiano kati ya Afrika na Diaspora, harakati kati ya Afrika na ulimwengu wote, na jinsi Afrika inavyoungana na ulimwengu wote. Juzuu hii kinaweka dhana ya ubunifu ya Kiafrika kuwa ya ulimwengu katika moyo wa mtazamo wake. Zaidi ya mfumo wa juu wa Atlantiki, michango ya juzuu hii inategemea nadharia mpya za kitaaluma na mazoea ya kihistoria kama vile masomo ya wasifu ili kuelewa historia ya Waafrika walio ughaibuni kutoka ndani.

 Sehemu ya kwanza inajadili muktadha wa kihistoria ulioibua dhana ya rangi, ili kuelewa jinsi Waafrika na watu wenye asili ya Afrika wanavyojiona wao wenyewe na wengine.

Sehemu ya pili ni ramani ya kuelewa ilani ya Waafrika wanaoishi ughaibuni na inashughulikia mambo matatu kulingana na jiografia ya diaspora. Biashara ya watumwa Barani Afrika, bila kujali eneo, imehusishwa na mapambano ya uhuru. Sehemu hii pia inachunguza utambulisho wa kitamaduni na jinsi zilivyoundwa upya katika mifumo ya maarifa ya Kiafrika na maarifa ya kiteknolojia.
 
Sehemu ya mwisho ya juzuu inahusika na milia na wasifu wa wanaume na wanawake wa Kiafrika. Wasifu huu unatoa moja ya maono ya kibinadamu na uwakilishi wa Waafrika wanaoishi ughaibuni. 

Juzuu ya kumi na moja 

Juzuu hii inachunguza changamoto za kisasa zinazoikabili Afrika na makundi ya waafrika wanaoishi ughaibuni Duniani. Inaangalia kwa makini mabadiliko makubwa katika suala hili kutokana na mtazamo wa dhana ya Kiafrika kuwa mali ya ulimwengu. Katika kiini cha mtazamo wa uchambuzi unaowasilisha, majukumu ya wanawake na vijana, ubunifu, uzalishaji wa maarifa na mabadiliko ya kisiasa ni muhimu katika kujenga mustakabali wa Afrika na ughaibuni wa Afrika. 

Sehemu ya kwanza inajumuisha majadiliano ya kitaaluma yenye lengo la kuchunguza dhana ya Kiafrika kuwa mali ya ulimwengu.

Sehemu ya pili inaangazia uwepo wa Waafrika katika muktadha wa utandawazi, iwe barani au nje ya mipaka yake ya kijiografia. 

Sehemu ya tatu inaangazia mageuzi ya juhudi za Afrika kushiriki katika kushughulikia changamoto za ulimwengu wa kisasa. 

Juzuu tatu mpya: Juzuu ya 9,10, na 11. 

 Kama sehemu ya juhudi za kusasisha na kusasisha mkusanyiko mkuu wa Historia ya Afrika, UNESCO imeanza maandalizi na uandaaji wa juzuu tatu mpya.  Kupitia hatua hii, FAO inatamani kusasisha mkusanyiko kwa kuzingatia maendeleo ya hivi karibuni ya kijamii, kisiasa na akiolojia Barani (Juzuu ya Tisa); kuchora ramani ya usambazaji wa makundi mbalimbali ya Waafrika walio ughaibuni Duniani na kuchambua mchango wao katika ujenzi wa jamii za kisasa na maendeleo na maendeleo ya bara la Afrika Juzuu ya Kumi); na kuchambua changamoto mpya zinazoikabili Afrika na makundi ya ughaibuni ya Afrika Duniani, pamoja na fursa mpya zinazopatikana kwao (Juzuu ya kumi na moja ).

Juhudi zilizopelekea maandalizi na uandaaji wa juzuu hizo tatu mpya zinawakilisha pato kubwa la kisayansi lililofanywa na UNESCO ili kuelewa vyema historia ya Afrika na jinsi ya kuiandika. Juhudi hizi ni mchango mkubwa kwa UNESCO ndani ya mfumo wa Muongo wa Kimataifa wa Watu wenye Asili ya Afrika (2015-2024), uliotangazwa na Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa. Pia inajibu mipango iliyochukuliwa na serikali kadhaa za Amerika Kusini na Caribbean kukuza na kukuza urithi wao wa Kiafrika. 

Chanzo 

Tovuti ya UNESCO.