Kipindi cha kwanza "Uvumbuzi na kusaidia uwajibikaji wa kijamii kufikia mustakabali bora"

Programu ya Raia wa Ulimwengu mzima ilianza vipindi vyake vya kwanza kwa kumkaribisha kijana mhispania, Carlos Santos, mwenye miaka 31, mwanzilishi wa (World Impact Alliance) na mwanachama wa timu ya Jukwaa la uchumi la Dunia pia ni mhadhiri katika zaidi ya vyuo vikuu saba Duniani.

Na mwanzoni mwa mkutano huo, Carlos alielezea furaha yake kushiriki katika programu ya Raia wa Ulimwengu mzima na kuonyesha umuhimu wa programu hizo katika kusaidia lugha ya mazungumzo na mawasiliano kati ya vijana katika nchi mbalimbali ulimwenguni.

Akiashiria matokeo ya virusi vya Corona, Santos aliamini kwamba  kipindi cha marufuku kinazingatiwa kipindi cha kujitambua tena nafsi na aliwaalika watu wote kutumia kipindi hiki kwa njia bora zaidi na alisisitiza kuwa yeye anafuatia kwa ukaribu mabadiliko yaliyotokea katika sekta zote katika nchi mbalimbali za Dunia baada ya mlipuko wa Janga la Corona.

Na kwa kuzungumzia (World Impact Alliance), alisisitiza kuwa lengo kuu la Shirika hili ni kukuza uwajibikaji wa kijamii kwa makampuni na taasisi katika sekta zote mbili za umma na binafsi kupitia Shiriki kadhaa na serikali mbalimbali, vyama vya wenyewe kwa wenyewe na vyombo vya habari, alieleza kuwa njia ya kufikia lengo hilo si rahisi lakini pia linawezekana.

Wakati wa mkutano huo, Santos alizungumzia safari zake Duniani kote na ziara zake kwa zaidi ya nchi 30 akisisitiza kuwa kile kinachotuunganisha ni zaidi ya kile kinachotutenganisha.

Pia alizungumzia ziara yake ya mwisho nchini Misri wakati wa kushiriki kwake katika toleo la tatu la Jukwaa la Vijana Duniani kwa utunzaji wa Rais Abd El Fatah El-Sisi na alielezea furaha yake kubwa kuzungumza na Rais El-Sisi katika moja ya vikao vya Jukwaa na kusisitizia umuhimu wa kuunda viunganishi vya mawasiliano kati ya vijana na watunga maamuzi.

Mwishoni mwa mkutano, Santos ameshapeleka ujumbe kwa vijana katika nchi mbalimbali Duniani, akiwahimiza kuwasaidia wengine, kuwa na nguvu zaidi na kufurahia mambo mazuri ya maisha, pamoja na kuwahimiza wajitambue wenyewe, kuendeleza ujuzi wao na kuacha uvutano wazi na dhahiri.

Vipindi vya programu vinasimamiwa na Amira Sayed Mwandishi wa habari katika Gazeti la Al-Egyptian, ambalo linazingatiwa gazeti la kwanza linalozungumzia kwa lugha ya kiingereza katika Mashariki ya Kati, pamoja na kuwa mwakilishi wa Misri katika Bunge la vijana la maji Duniani na ameshiriki katika kusambaza shughuli nyingi za kimataifa ndani na nje ya Misri.

Orodha ya wageni wa programu inajumuisha idadi ya watunga maamuzi na viongozi vijana kutoka nchi mbalimbali Duniani na katika nyanja mbalimbali, na hilo kwa lengo la kueneza jumbe chanya kwa vijana wa Dunia kutoka  Kairo, pamoja na kuunda kiunganishi cha mawasiliano kati ya vijana na watunga maamuzi,

linalochangia kuandaa makada wa vijana wanaoweza kufanya mabadiliko yanayoonekana kwelikweli.

Inatajwa kwamba programu ya Raia wa Ulimwengu mzima  ni programu ya kwanza ya moja kwa moja inayolenga kuunga mkono dhana ya Umoja na Ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuonesha majaribio ya vijana wenye mafanikio Duniani kote.