Ziara ya eneo la Piramidi kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa
Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dkt Ashraf Sobhy, asubuhi ya leo Jumamosi, iliandaa ziara ya kiutalii kuelekea Piramidi za Giza na Saqqara, kwa wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika shughuli za siku ya kumi na moja ya Udhamini wa Kiongozi Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, walitembelea eneo la Piramidi za Giza ili kuona maeneo ya kiakiolojia katika eneo hilo na Piramidi tatu, kisha ziara hiyo ilielekea eneo la "Panorama" kuchukua picha za ukumbusho, nao walihitimisha ziara yao kutembelea eneo la Sanamu ya Abu El Hool, wakisifu ukuu wa Misri na Historia yake kale pia Ukale wake wa Ustaarabu.
Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu, walielezea furaha yao kubwa kuona moja ya maajabu saba ya Dunia na kile walichokiona juu ya hazina ya kiakiolojia kuhusu Ustaarabu mkale wa Misri na ukuu wa ujenzi wa Piramidi, wakisisitiza Shukrani zao kubwa kwa Rais Abdel Fattah Al-Sisi kwa mabadiliko ya kiutamaduni ambayo Misri inashuhudia katika ujenzi , ambapo uhalisi wa zamani unaungana na maadhimisho ya sasa.
Kwa upande wao, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , walitwiti kwenye kurasa zao za kibinafsi kwenye mitandao ya kijamii, wakimshukuru Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa huduma yake ya mara kwa mara ya kufadhili na kuwakaribisha shughuli za kimataifa ya vijana, na kufanya kila juhudi na ndugu katika nchi mbalimbali ili kufikia mwamko wa vijana katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande mmoja, Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alionyesha kuwa ziara na safari za kihistoria hupangwa ndani ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ili kutambua maeneo muhimu zaidi ya kiutalii na kiakiolojia, na majumba ya ustaarabu na utamaduni wa Misri, ambapo makumbusho la Hayati Kiongozi Gamal Abdel Nasser lilitembelewa, Baraza la Wabunge la Misri, Makumbusho ya Kitaifa ya Ustaarabu wa Misri, eneo la Piramidi, pamoja na maeneo mengine mengi yaliyopangwa kutembelewa siku zijazo.
Ni vyema kutambua kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, unalenga kuhamisha uzoefu wa Misri ya kale katika kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kufanya kazi ya kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi zisizofungamana na maoni sambasamba na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa dhima ya harakati Zisizofungamana.