Vigezo vya kuwachagua waombaji Duniani kote kushiriki katika toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Vigezo vya kuwachagua waombaji Duniani kote kushiriki katika toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Tunafuatilia kwa kina matarajio yenu kwa awamu ya kisasa ya hatua za mwisho za kushiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, na kama kawaida yetu pamoja nanyi ya kila wakati – tangu Tangazo la toleo la kwanza la Udhamini huo- uwazi na kina ya kusambaza orodha za hatua za mwisho moja kwa moja, pia karibuni kwa maelezo zaidi   tutatangaza takwimu za waombaji wa Udhamini mwaka huu.

hiyo ni kama utekelezaji wa kanuni ya uwazi ambayo Maoni ya Misri ya 2030 inalenga, ambapo inaweka mfumo unaoizunguka unaobainisha kwamba taasisi zinafurahia usimamizi madhubuti, ufanisi, uhodari, haki, usikivu na ubora, uwajibikaji, na kuinua kuridhisha umma kupitia kuhudumia malengo ya maendeleo.

 

Kulingana na idadi ya juu na ushindani mzito huo , basi mchakato wa uteuzi kati ya waombaji unafanywa kwa kina na ufanisi, ili tuweze kufikia haki ya kuchagua waombaji bora kulingana na kupatikana kwa sifa na uwezo wa kibinafsi sawasawa na masharti na malengo ya Udhamini.

 Kutoka ufanisi wa juu,inaashiriwa  kwamba Udhamini huo uliweka vigezo kadhaa, kwa kuzingatia fursa sawa kati ya jinsia zote mbili, basi mchakato wa uteuzi unafanyikwa kama ifuatavyo:

 

1-Kwa kuzingatia kwamba washiriki wa Udhamini wanapaswa kuwa (50% wanaume na 50% wanawake), kwani kigezo hiki ni moja ya vitu muhimu katika hati ambazo tunazitegemea, sawa iwe Maoni ya Misri 2030 au hata ajenda za bara kama Afrika. Ajenda ya 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, ambapo Lengo la usawa wa kijinsia liko ndani ya lengo la tano la malengo yake, na hii inakuja ndani ya mfumo wa ibara ya 13, inayosisitiza kwamba "sera inahakikisha fursa sawa kwa vijana wa kiume na wa kike".

 

kuzingatia kuwa 5% ya washiriki wote ni watu walemavu, ambapo hiyo inahusishwa kwa karibu na Lengo Na. (10) la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusisha "kupunguza kutosawazisha kati ya wote".

2-Kuzingatia na kujaza vizuri kwa lugha ya Kiingereza, na kwa undani fomu ya maombi ya kielektroniki.

 Kwa mujibu wa Maoni ya  Misri ya 2030, yanayotafutia kukuza ubora wa elimu kwa mfumo wa kitaasisi bora na ulioelimika, unaoweza kutoa mtu mbunifu na anayewajibika, pia anayeweza kushughulika kwa ushindani na taasisi za kikanda na kimataifa.

 

3-Ubora wa video iliyoambatanishwa ya utambulishaji wa mwombaji wa ujuzi wake, uzoefu na matarajio mnamo dakika mbili, na jinsi vinaambatanaje pamoja  na fomu aliyoijaza.

 - Inahusiana kwa karibu na majukumu yaliyowekwa kwa vijana na Hati ya Vijana wa Afrika, inayosema kwamba "Vijana wawe na macho na akili timamu ya maendeleo yao ya kibinafsi na ukuzaji wa ujuzi wao".

 

4-Uwezo wa mwombaji kujieleza kwa Kiingereza, ili kuhakikisha urahisi wa mawasiliano kati ya washiriki kutoka Duniani kote wakati wa shughuli za Udhamini, pia tofauti ya lugha kadhaa inapendezwa lakini haitakuwa ya muhimu zaidi katika mchakato wa uteuzi.

- Ambapo kigezo hiki kinaambatana na Ibara ya (20) ya Hati ya Vijana wa Afrika, inayoeleza kuwawezesha vijana kueleza muunganiko huu kupitia sanaa, fasihi ya tamthilia, uandishi, muziki na aina nyinginezo za kiutamaduni na kisanii.

 Aidha, kigezo hiki kinahakikisha lengo la Ibara ya (20) pia kuhusu kukuza uelewa wa pamoja wa kiutamaduni kupitia programu za kubadilishana kati ya vijana na Taasisi za vijana ndani na kati ya nchi wanachama.

5-Maarifa za kiutamaduni, uzoefu wa ndani na kiwango cha ujihusishaji wa mwombaji katika kazi (sekta ya kibinafsi - kazi ya umma - kazi ya kiraia)

Ambapo hiyo iko ndani ya mfumo wa matarajio ya kwanza ya Ajenda ya 2063 ya Afrika, inayotegemea "raia walioelimika vyema na wenye ujuzi, pia sayansi, teknolojia na uvumbuzi ili kufikia jamii ya ujuzi".

6-Kutoa nafasi kwa watu wa maeneo ya mipakani na maeneo ya pembezoni, kwa kuzingatia mgawanyo wa kijiografia, na maeneo ambayo watu wake wanatafutia nafasi za kujifanikisha.ambapo huo ndio kiini cha matarajio ya tatu ya Ajenda 2063 ya Afrika, inayotamani "Bara la Afrika linalotawaliwa na utawala bora, demokrasia na kuheshimu haki za binadamu, Haki ya kijamii na utawala wa sharia".

 Jambo hilo pia linahusiana kwa karibu na malengo ya Ibara ya 10 ya Hati ya Vijana wa Afrika, inayoelekeza kuwezesha uanzishaji au uimarishaji wa majukwaa ya ushiriki wa vijana katika kuunda maamuzi katika ngazi za utawala wa kitaifa, kikanda na bara.

 7-Taasisi ambapo mwombaji anajihusisha, pia kiwango cha ushawishi wake ndani yake, hata ikiwa ni taasisi ndogo lakini yenye ufanisi kama dalili ya ushiriki wake katika maisha ya umma..

- Ambapo moja ya malengo ya matarajio ya sita yanatokana na Ajenda 2063, inayolenga "bara la Afrika lenye ushiriki mkubwa wa vijana na uwezeshaji na utekelezaji kamili wa Hati ya Vijana wa Afrika." Matarajio haya pia yanaweka mfumo wa jumla, ambao ni "Afrika ambamo watu huongoza maendeleo na kutegemea uwezo wa watu wa Kiafrika, haswa wanawake na vijana".

8 -Pengine Shahada ya sasa ya kitaaluma ya mwombaji, ikiwa ya ya kwanza, Uzamili au Uzamivu, wakati mwingine inaweza kuwa na mchango katika mchakato wa uteuzi ikiwa inalingana sambamba na uzoefu wa uwanjani.

Hiyo ndiyo inayoungana kwa karibu na Matarajio ya Sita ya Ajenda ya Afrika 2063, inayosema kwamba "Vijana waafrika watakuwa waundaji wa jamii ya maarifa ya Kiafrika, pia watakuwa na mchango maalum katika Uchumi".

9 -Uhusiano mwafaka kati ya uwanja wa sayansi ya mwombaji na mada zilizotolewa na Udhamini. (Maoni ya Misri 2063)

10-Pia tunajali sana kujua mwombaji ana mpango gani wa kufanya baada ya kuhitimu Udhamini kwa kuutumikia  kuhudumia jamii yake.

Ambapo Kigezo hiki kinaendana na malengo ya Ibara ya (10) ya Hati ya Vijana wa Afrika, inayosema "Nchi Wanachama zitahimiza Taasisi za vijana kuongoza programu za vijana na kuhakikisha utekelezaji wa haki yao ya maendeleo," pamoja na uhusiano wake na ibara Na. (11) ya Hati hiyo, inayopendekeza "kuchukua hatua Muhimu kwa ajili ya taaluma ya kazi ya vijana na kuanzishwa kwa programu za mafunzo husika katika elimu ya juu na taasisi nyingine za mafunzo".

 11-Mwingiliano wa mwombaji kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii (Twitter-Instegram-Youtube-Telegram) kiwango cha ushawishi wake, na mawasiliano yake na jamii yake na wafuasi kupitia kwake, ambapo inazingatiwa kama sura moja ya mshikamano Duniani.

12-Mwingiliano wa mwombaji kwenye majukwaa yetu rasmi kwenye tovuti za mitandao ya kijamii tunazozifuata kwa uangalifu, na kuweka kwa kauli mbiu "Mmoja kwa ajili ya  Wote, Wote kwa ajili ya  Mmoja"  -Tupo pamoja- kama njia mpya ya mawasiliano kati ya washiriki, na moja ya taratibu za maandalizi ya mkutano wao katika Udhamini, pia ni dalili, na kiashirio cha kujitolea kwao.

Na hilo ndilo linalohusiana na Ibara ya (11) inayopendekeza pande zinazohusika zichukue hatua za kuimarisha ushiriki hai wa vijana katika jamii, pamoja na uhusiano wake na lengo la 17 la maendeleo endelevu, ambalo ni kuimarisha njia na taratibu za kujenga ushirikiano.

 13-Pia Majibu wazi ya Barua-Pepe tunazozipeleka kwa waombaji katika hatua zote za Shughuli, na kujitolea kwao kwa kile tunachoashiria katika kila E-Mail, ni moja ya mambo muhimu ambayo huongeza tathmini ya mwombaji huo, na kiashirio cha ujuzi wake wa njia za kisasa za mawasiliano, ambayo inakuja ndani ya malengo ya Maoni ya Misri ya 2030 kuhusu  mabadiliko ya kidijitali, ukuzaji wa njia za mawasiliano na teknolojia ya Taarifa.

  _____

 Noti: vinyume viwili vinaweza kutuvutia (Wasomi wa kikaboni – waliojielimisha)

 Wa kwanza: Ana mradi wa maendeleo ya kiutamaduni wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika jamii, kuunganisha maadili ya juu na dhana za kisasa, na kushawishi kwa ufanisi na kwa kujenga katika jamii yake, na yeye ndiye mtengenezaji halisi wa usalama na amani katika jamii.

 Wa pili: Alijishughulisha sana katika kujifunza na kupatia vyeti, kozi na shahada, alifanya kazi ya kuviongeza huku na kule, na hakututajia hata hali moja iliyompata mtu maana mtu mhusika anayejitegemea, ana maarifa , anajitolea kwake mwenyewe, hajali mabadiliko ya jamii yake au maendeleo yake ni mbali na majukumu yaliyoainishwa katika Hati ya Vijana wa Afrika, (Kuhudumia Nchi- Kushiriki katika Maendeleo ya Jamii), na kwa hivyo tathmini yetu kwake itakuwa  kwamba sifa na ujuzi wake hauendani na mahitaji ya programu zetu.