Muungano wa Vijana wa Afrika
Imefasiriwa na / Mervat Sakr
Shirika mama la Vijana wa Afrika, liliundwa mwaka 1962 kabla ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, pamoja na jina la Harakati ya Vijana wa Pan-African kabla ya kubadilisha jina na kuitwa Muungano wa Vijana wa Afrika mwaka 2005.
Guinea Conakry, nchi ya kuanzishwa, ilikuwa mwenyeji wa makao makuu ya Muungano hadi 1980, kisha ikahamishiwa Algeria hadi 2006, na kisha Msumbiji hadi 2011 kabla ya makao makuu kuhamishiwa mji mkuu wa Sudan Khartoum mwaka 2011, na sherehe ya utiaji saini ilikuwa siku ya Afrika Mei 25, na Novemba 2021 hati hiyo ilisainiwa kuhamishia Muungano huo makao makuu yake mapya katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, na ilizinduliwa rasmi Februari 21, 2022.
Dhamira ya Muungano ni kukuza maadili na misingi yake ya Amani, Demokrasia na Maendeleo Endelevu kwa lengo la kufikia Ushirikiano wa Afrika.
Shirika hilo ni chombo kikuu cha vijana Barani humo na hufurahia nafasi maalumu ndani ya Umoja wa Afrika, na mara nyingi hushauriwa na Wakuu wengine wa Nchi na Serikali, Halmashauri Kuu na Mikutano ya Kudumu ya Umoja wa Afrika, kuhusu masuala kama vile Afya, Elimu, Vijana, Uhamiaji na Masuala ya jinsia katika masuala yanayohusiana na Vijana.
Shirika hilo linawaita Vijana waafrika na nchi za Afrika, kupitia mabaraza ya Vijana wa ndani, kusaidia ushiriki wa kisiasa na uwakilishi wa Vijana katika ngazi zote, na Shirika hilo lina mikataba kadhaa ya ushirikiano na mashirika ya Vijana, na Taasisi.
Ofisi ya Kiutendaji ina wawakilishi 2 kwa kila kanda pamoja na Rais na Katibu Mkuu, na Misri na Afrika Kaskazini ziliwakilishwa na mwanaanthropolojia Hassan Ghazaly, mwanzilishi wa Ofisi ya Vijana wa Afrika katika Wizara ya Vijana na Michezo, na Mwanzilishi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Kanda ya Afrika Kaskazini kutoka 2014 hadi 2017, na kisha kutoka 2017 hadi 2020 alishikilia nafasi ya Makamu wa Mkuu wa Shirikisho.