Baraza la Wawakilishi lapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Baraza la Wawakilishi lapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Baraza la Wawakilishi lapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Baraza la Wawakilishi lapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Baraza la Wawakilishi lapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa uliandaa ziara ya Bunge la Misri kwa wajumbe kadhaa walioshiriki katika Udhamini huo, kwa mahudhurio ya Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Mshauri Ahmed Saad, Naibu katibu wa Baraza hilo, na Mshauri Ahmed Manna, Katibu Mkuu wa Baraza hilo. Na hilo linatokea mnamo  siku mbili (ya tatu & kumi) za matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, wakati wa mkutano wake na washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwenye Bunge la Misri, alisisitiza kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za taifa la Misri za kufanya jukumu lake lililolengwa kuimarisha jukumu la Vijana waafrika kwa kutoa kila aina za msaada, kukarabati na mafunzo. Na ni moja ya nyenzo inayoendeleza juhudi za serikali ili kurejesha undugu pamoja na nchi zote za Afrika, ambayo huanza na suala la ushirikiano wa vijana, akiongeza kuwa thamani ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa inatokana na kuchukua jina la marehemu kiongozi Gamal Abd El Nasser, pamoja na kuungwa mkono na Ufadhili wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, ambaye ndiye mwendeshaji mkuu wa wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha matukio ya Udhamini huo.

Pia, Sobhy alionesha jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo katika kusaidia, kukarabati na kuwawezesha vijana na ukuaji uliotokea katika kuwawezesha vijana tangu Rais Abd El Fatah El-Sisi ashike Madaraka na nia yake ya kuendeleza na kusaidia uwezo wa vijana, iliyokuwa wazi katika uzinduzi wa Rais wa Mpango wa Urais wa Marekebisho ya Vijana, pamoja na uzinduzi wa makongamano na semina nyingi za vijana.

Kwa upande wake, Waziri huyo alipendekeza kuanzishwa kwa Taasisi ya Bunge la Vijana wa Afrika kutokana na Udhamini huo, akisisitiza kuwa serikali iko tayari kupokea mawazo yote ya vijana na alibainisha heshima ya taifa la Misri kwa ndugu wote kutoka nchi mbalimbali waliokuja kwetu kutokana na hali ambazo nchi zao zinapitia, na kuwajumuisha katika jamii ya Misri na kuishi nao, na kupatikana kwa programu zote, shughuli na huduma, haswa kuhusu vituo vya vijana na taasisi za Vijana na Michezo, akisisitiza kwamba hakuna neno "Mkimbizi" au "Makambi" na tunayakataa kabisa.

Pia, Naibu Katibu Mkuu wa Bunge, Ahmed Saad, alieleza furaha yake kubwa ya kuona wanamitindo hao waanzilishi wa vijana kutoka nchi mbalimbali Duniani, na wakati wa hotuba yake, aligusia kulitambulisha Bunge na jukumu la kutunga sheria na usimamizi wa Bunge, na kubainisha kuwa Bunge lilifikia asilimia kubwa ya uwakilishi wa Vijana ndani ya mfumo wa mpango wa serikali wa kuwawezesha vijana, na Saad aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za kufikia mahusiano ya ushirikiano kati ya nchi mbalimbali kutoka Duniani kote katika nyanja mbalimbali, haswa uwanja wa vijana, akiwa kinara kwa siku zijazo, na alizungumzia juhudi za serikali kuunda majukwaa na taasisi zinazofanya kazi ili kufikia ushirikiano wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Washiriki wa Udhamini huo walitembelea korido za Bunge la Misri na jumba la makumbusho liliko ndani ya Bunge, linalo kumbukumbu za vikao vya kihistoria na michoro mingi inayozungumzia historia ya Bunge la Misri.