"Vijana na Michezo" yazindua shughuli za kwanza za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili
Leo Jumanne, Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dokta. "Ashraf Sobhy" imezindua shughuli za kwanza za Udhamini wa Kiongozi " Gamal Abd El Nasser" kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili, chini ya kauli mbiu " Ushirikiano wa Kusini-Kusini" kwa kushirikiana na chuo cha mafunzo cha kimataifa, Wizara ya mambo ya nje ya Misri na taasisi nyingi za kitaifa, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi, Rais wa Jamhuri, kuanzia tarehe 1 hadi 16 Juni 2021, kwa ushiriki wa Viongozi Vijana 100 katika mabara ya ( Afrika, Asia,na Amerika kusini) kwa mahudhurio ya nchi 50 ( Liberia, Palastina,Mali, Togo, Yordani, Lebanon, Lesotho, Guinea, China,Brazil, Zimbabwe, Namibia, Mauritania,Afrika ya kati, Codevoire, Srilanka, Malawi, Burkina Faso, Colombia, Burundi, Saudi Arabia, Pakistan, Iraq,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia, Zambia, Bangladesh, Russia, Afghanistan, Uzbekistan, Azerbaijan, Cameron, Algeria, Libya, Ghana, Chad, Rwanda, Tanzania, Kenya,Uganda,Senegal, Sudan Kusini, Sudan, Morocco, Tunisia,Mexico, Ecuador.
Wajumbe hao wameanza ziara yao hii leo kwa kutembelea makumbusho ya Kiongozi " Gamal Abd El Nasser", walijua mwanzo halisi wa kugeuza nyumba kwa makumbusho mnamo 2014 baada ya Rais " Abd El Fatah El sisi" kushika madaraka kama Rais wa Jamhuri,
Wakielezea kuheshima Misri na wamisri kwa historia yao na mchango wa viongozi wao, wanaotoa uaminifu kwake, wakiashiria mnamo ziara yao kuwa hayati Rais " Gamal Abd El Nasser hakuwa Kiongozi wa Misri na Mwarabu tu bali alikuwa mmoja wa Viongozi mashuhuri katika historia ya Utu mzima mnamo karne ya 20.
Na pia walijua kiasi cha mafanikio ya kiutamaduni ya kitaifa ya Misri, ambayo yanaandika mwenendo wa Kiongozi Gamal Abd El Nasser, pia kiasi alichotolea na kutoa mhanga kiongozi huyo ambaye ni alama za kitaifa za Misri.
Wajumbe hao waliangalia sehemu zote za makumbusho yakiwemo lango la kuingilia, mapokezi na ukumbi wa makumbusho, na walishuhudia jengo hilo katika hali yake ya sasa ambapo makumbusho yana ofisi ya Rais, picha kubwa na mikusanyiko ya Kiongozi " Gamal Abd El Nasser, zawadi na barua na walipiga picha za kumbukumbu.
Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya Misri baada ya Urais wake wa Umoja wa Afrika mnamo 2019 katika kutekeleza jukumu lake katika kuimarisha mchango wa vijana wa Afrika kwa kutoa aina zote za msaada, ukarabati na mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika vyeo vya uongozi na kufaidi kutoka uwezo wa mawazo yao, Na pia inachukuliwa kama hatua za utekelezaji wa mtazamo wa Misri wa 2030, kanuni kumi za Shirika la Ushikamano wa Afro-Asia, Ajenda ya Afrika 2063, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ushirikiano wa Kusini-Kusini, Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji wa Vijana na Hati ya Vijana wa Afrika .
Ni vyema kuashiria kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi lilitekelezwa mnamo Juni 2019, likiwa na Ufadhili wa Dkt.Mustafa Madbouly Waziri Mkuu,lililokuwa likilenga Viongozi Vijana washawishi katika jamii zao; kuhamisha Jaribio la Misri la Maendeleo katika ukakamavu wa taasisi na kuandaa mhusika wa kitaifa.